Simulizi Zetu

Simulizi   Zetu

Share

31/01/2024

Stori ipo hewani hadi sehemu ya sita [ MOYO WA MASIKINI ]

31/01/2024

MOYO WA MASIKINI πŸ’”πŸ˜’

sehemu ya 6πŸ’“

Simulizi pageπŸ’

Usiku wa manane REHEMA alishtuka usingizini na kumuona kiba bado yupo macho , kiba alimwambia REHEMA

" wew mwanamke unakoroma k**a jenereta , usiwe na hofu lala tu nimesha ongea na kaka yako "
Ila kiba alionekana kutokuwa sawa kabisa ilimbidi rehema asogee karibu kwa kiba na kumuuliza

" yule ndio ADA mwenyewe mnaependana mbona k**a ni mke wa mtu , ila sio mbaya mimi nipo karibu yako "

Kiba alitabasamu tu sababu rehema ndio maneno yake ya kila siku ,

Siku hiyo ilipita

Siku nyingine tena kiba yupo mgahawani asubuhi na mapema akifanya usafi linakuja gari na anashuka yule jiDada wa rich anaonekana kuwa na hasira sana

Anasogea mbele ya kiba na kumpiga Kofi kwa hasira
" kwanini unakuwa kikwazo kwenye mahusiano yangu na rich"

Kiba hakulipa Kofi alimshika mkono na kumvuta sehemu waongee

" Dada yangu Leo ngojaa nikwanbie kitu , rich anamdogo wake na pia na yatima hawa ,, ndugu zao waliwatenga zamani sana , wewe una mama na baba unandugu wanao kupenda unamume tajiri na mkorofi wewe mwenyewe unamjua Leo rich akifa dogo lake ataishi maisha gani , nafanya haya sio kwamba namuonea wivu hapana , nalipa fadhila aliniokota mtaani hapa nilikuwa nikija kuomba chakula ndio maana namuona wa muhimu sana katika maisha yetu "

Waliongea mengi sana siku hiyo ilipita , inakuja Siku nyingine usiku rich akiwa njiani anarudi nyumbani alitekwa na watu wasio julikana , rehema na kiba walitafuta sana walikataa tamaa baada ya muda kupita

Rehema anapigiwa simu kutoka hospital wanaenda na kiba wanamkuta rich yupo hali mautiuti kaharibika usoni kavunjwa vunjwa mifupa anapumulia kwa machine "

Kiba alipata hasira alitoka pale hospital na kumfuata yule Dada nyumbani kwake , alifika getini alizuiliwa kuingia na mlinzi alisubiri sana mwisho gari likaonekana likitoka alilisimamisha ,

Gari lilipo shushwa vioo alionekana yule Dada akiwa na mumewe aliwasalimu na kuwaambia

" tuna shukuru hatuta kuja kuwasahau katika maisha yetu "

Siku hiyo usiku wakiwa hospitali rehema alikuwa akilia tu , alikuja yule Dada kiba alimfukuza k**a mwizi

Baadae siku nyingi kupita rich alionekana kupata hafadhali walipiga stori nyingi sana mwisho rich alimuomba kiba

" kiba naomba muangalie mdogo wangu ,k**a nisipo kuwepo sababu mnapendeza sana mkiwa pamojaa najua utawezana nae sababu huyo yupo hivyo kutokana na mazingira aliyo lelewa , muangalie vizuri ndio malipo yangu nakuomba "

Kiba hakujua aliongea hivyo kwanini alikuja rehema akiwa amebeba chakula alikuwa na furaha sana kwa sababu kaka yake amepata hafadhali rehema alienda kununua hadi shati na suruali k**a zawadi ya kaka yake akitoka hospital

Siku hiyo ilipita siku ya pili asubuhi , mungu alimchukua rich hakuna aliye fikilia wala kuzania

Rehema alikuja hospital akiwa amebeba chai na kiba alikuwa amelala pembeni , rehema alikuwa na kelele

" kaka kaka Leo , nataka nikuambie kitu "

Kiba alimkatisha njiani kwa kumwambia

" amepumzika mwache bhna"

Rehema alimuandalia chai kiba walikunywa kwa pamojaa wakipiga stori kwa kunong'ona wakipiga utani muda huo hawakujua k**a kaka yao amesha fariki 😒

Baada ya muda kidogo alikuja nesi alipomgusa rich alishtuka na kutoka nje mbio kumwita dokta kiba na REHEMA walitolewa njee wote walikuwa wamepigwa na butwa

Dokta anarudi na kuuliza nani ndugu mtu wa karibu na Richard nelsoni kiyako rich na REHEMA walijitokeza dokta aliwaitia pembeni na kuwaambia ukweli

Aise ! Ilikuwa huzuni sana rehema alilia sana 😭😭

BAADA YA MIEZI MINNE

USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA
Tutaendelea na stori yetu usisahau kufuatilia simulizi zetu page kwa stori nyingi nyingi siuzi story zangu , mtazipata bure kabisa ninacho kihitaji kutoka kwenu ni saport tu comment ,like , share pia follow page hii ili uendelee kupata stori kwa urahisi

13/01/2024

NILIKATA TAMAA. 🎸🎷🎀🎼

Sehemu ya pili πŸ”ˆπŸ”‰πŸ”Š

Ukurasa wa Simulizi zetu πŸ“’πŸ““

Njombe Tanzania πŸ–‹πŸ“¨πŸ“€

🌹🌹

BAADA YA MALAIKA KUSHUKA KUMBARIKI YULE MTOTO inaendelea

Malaika alimwambia yule mtoto " ishi k**a zawadi , wafariji watu wetu , utunze nyota na kipaji kwa sababu kila mtu anatamani awe k**a wewe"

Wazazi wa mtoto walimpa jina mtoto KINETIANI " faraja yetu"

Najua wewe msomaji ulitamani uwe k**a huyo mtoto , uwe mtu maalumu .

Tunaendelea .
Ilipita miezi kadhaa mtoto akiwa anakuwa kwa afya njema na uangalizi wa wazazi hao

Mtoto alikuwa wa ajabu sana hasa upande wa muziki maana hata awe na maumivu kiasi gani , ukimwimbia tu anaacha kulia

Alipo kuwa akitembea , walikuwa nae makini zaidi kwa hatari zote , walihofia zaidi mtoto kupotea alikuwa na tabia ya kufuata watu wanao imba hasa wapiga ngoma " kijijini hapo walikuwa na utaratibu wa kupiga ngoma na kuimba kila baada ya siku saba, siku za ndoa , siku za msiba , walikuwa wakizunguka kila kitongoji "

Mtoto huyo alikuwa akipenda wanavyo imba na kupiga ngoma zile

Mtoto alipo fika miaka sita ndio kipaji na nyota vikaanza kuonekana , hicho kipaji walikuwa wakijua wanafamilia tu

Mama alimkataza mwanae kuimba mbele za watu akiofia watu wenye wivu , kwa hiyo mtoto alikuwa akitaka kuimba anasubiri afike nyumbani aanze kuimba na atakaye mkuta nyumbani aliendelea hivyo hadi alipo fika miaka kumi .

BAADA YA MIAKA MINNE

MAMA " wewe mwanangu kula taratibu Leo mwalimu wenu atachelewa kuja kuwafundisha

KINE " mama mwalimu alisema nikiwahi nifanye mazoezi na wenzangu hata k**a yeye hayupo si unajua Mimi naweza kuimba kuliko watoto wote hapa kijijini "

MAMA " hahaha mwanangu na EMA mtoto wa SIKU NNE yule nae si anaweza k**a wewe"

KINE " mama , EMA anaweza ila kwangu Mimi hanifikii hata robo sababu Mimi na sauti nzuri ya kuimba kuliko yeye "

MAMA " hamna wote mpo sawa , hakuna binadamu aliye zaidi ya mwenzak kwa kila kitu ,kwa sababu sisi sote mungu wetu mmoja "

KINE " alinambia mwalimu , Mimi na kipaji cha tofauti ndio maana hata shuleni mimi ndio mwimbaji ninaye tegemewa japo kuwa kuna wanafunzi wakubwa zaidi yangu "

MAMA " kula huendage , maana unanizidi kiswahili ila uwi kurudi umpitie baba yako bustanini si unajua muda wa kumwagilia baba yako anapenda sana uwepo wewe kuliko Mimi "

KINE " EEH , alinambia kwa sababu mwanamke ni wakulinda nyumba na Mimi ni mtoto wa kiume natakiwa kujifunza kazi nikiwa mdogo "

MAMA " kaone k**a baba yake hivi "

Yalikuwa maongezi ya mama na mtoto baada ya mtoto kutoka shuleni na muda huo huo alitakiwa kwenda kanisani kufanya mazoezi ya kuimba

KINE anafika kanisani anamkuta EMA mbele akiwa bado ananguo za shule , inamaana EMA hakupitia nyumbani

KINE " wewe EMA umewahi kuliko Mimi unataka kuwa mwimbaji mzuri ?"

EMA " ndio nataka kuwa k**a wewe , mwalimu alinambia nifanye mazoezi sana "

KINE " mmh , umewahi mno , ila kwa upande wa nyie wasichana hakuna anaye kuzidi kuimba

EMA " hahaha, kweli ila Mimi njaa inaniuma , nisindikize kwenye bustani ya masista nikachume matund "

KINE " naogopa , ila twende si unanjaa "

Walienda kuiba matunda , wakiwa wanachuma walitolewa mbio na sista aliye kuwa akisafisha mazingira , yule sista alikuwa na hasira sana sababu imezoeleka kila siku matunda yanahalibiwa

Siku hiyo aliona asiwaachie watoto hao, wakina KINE walikimbia sana mwisho walifichama sehemu , sista alipo wakosa aliondoka

EMA alikuwa muoga sana KINE ALIMUULIZA

KINE " unaogopa "

EMA " ndio "alijibu huku analia

KINE " usiogope , bado unanjaa?"

EMA " ndio , "

KINE " usijali Leo tusiende kwenye mazoezi tumesha haribu yule sista atakuja kututafuta hapa twende kwenye bustani ya baba yangu , kuna matunda pia"

Wakati wanataka kuondoka EMA alishindwa kusimama kwa sababu alikuwa ameumia mguuni kwe harakati za kukimbia KINE alipiga hesabu ya haraka akaona bora ambebe tu

Wakiwa njiani walipiga stori nyingi huku EMA akiwa mgongoni mwa KINE " sababu ya EMA kuto rudi nyumbani kwao mchana huo , anaishi na mama wa kambo ambaye huwa anamzuia kwenda kuimba na kumpa kazi nyingi "

Walifika bustanini EMA akiwa hana kiatu mguu mmoja, alimshusha EMA na kumwambia atulie yeye atamtafutia matunda wakati huo baba alikuwa akiwaangalia tu .

ITAENDELEA USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA HAPO KESHO

Ukurasa Simulizi zetu tunaitaji sapot yako kwa kucomenti na kushare

17/09/2021

KAENI MACHO FANS WANGU
nipo free kwa sasa baada ya kuwa chini ya sheria muda wote niliokuwa kimya sasa tunaendea na stories zetu simulizi zetu drama ,love , comedy stories naanza na hiyo hapo '' saport yenu naitaji

Want your business to be the top-listed Engineering Company in Njombe?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Njombe