Mwenebato

Mwenebato

Share

Photos from Mwenebato's post 04/10/2019

Wagoma, Ba'ôma, Bagoma ni kabila la kimanyema kutoka Kigoma, asili yake mtambazo wa magharibi wa ziwa Tanganyika kwa mkabala sawa na mji wa ujiji na kigoma, urefu wa zaidi ya maili 70 ilikuwa ndiyo nchi ya Goma kwa upande wa DRC.

Mji wao wa asili katika Ujiji ni Kigoma-Mjini, kuja k**ini hadi katosho na burega, halafu ng'ambo ya luiche kuambaa mwambao kasaba, kaseke, kisha katika mkoa wa rukwa maeneo ya utinta, msamba, kipili na kisiwa cha manda, msimulizi anatueleza kwamba jina 'Burega' (ni jina la Babu wa Babu wa Abdul Nondo), miji ya Wagoma kihistoria ni vifungo "enclaves" kwasababu ya kuhamahama kwa shughuli za uvuvi na miji ya Kigoma-k**ini ilianza k**a miji ya kikambi na baadae wengi walirudi Ujiji.

Lusambo ambapo sasa panaitwa Shede au Kigedeko ndipo Wagoma walipofikia na maeneo yao mengine ni pamoja na Bangwe-Burega mpaka ujiji, Wazee wa kabila la 'Waha' wengi wao walikuwa ni wakulima, na wazee wa Kabila la Wagoma wao shughuli zao ilikuwa ni uvuvi na utengenezaji wa mitumbu ambapo biashara ilikuwa ikifanyika baina yao kwa kubadilishana bidhaa za mazao na uvuvi. Msimulizi anatueleza yakwamba kutokana na ukarimu waliokuwa nao wazee wa pande zote mbili wazee wa kiha walikuwa wakitembeleana na wagoma, ''Tugende kwa Bhagoma' (Twende kwa wagoma) ni maneno ambayo waha walikuwa wakizungumza, na ndiko jina Kigoma lilikopatikana. haswa wakimaanisha eneo lile la Kigoma Mjini.

Msimulizi anatueleza kwamba mji wa ujiji ulifahamika tangu karne ya 9.
Mfalme wa Wagoma alifahamika k**a 'Sultan Simba' ambae alikuwa ni mkarimu na mpenda undugu.

Ukoo mkubwa wa Wagoma ni 'Wene mbago' "Bene mba'o" ambapo wengine hudhani ni lakabu ya Wagoma wote, lakabu ya Wagoma "Ba'oma bakatan(d)a...", Ndugu zao katika asili ni Wabuyu, Waluba (Katanga) na Wazoba kiujumla ijapo wengi wengine ni Wapwa wa Wang'anja.

Msimulizi anatueleza kwamba, kwa dini Wagoma wa Ujiji takribani wote ni waislamu.
Lugha yao ni Kigoma ijapo hakizungumzwi kila siku kutokana na matumizi ya kiswahili kwasababu ya historia ya biashara ya utumwa na muingiliano na waarabu tangu karne 19. Kwasasa lugha ya Kigoma kinazungumzwa na watu wachache sana huko ujiji maeneo ya Kazaroho na baadhi ya maeneo ya Kabondo na Majengo, hii ni kutokana kwamba makabila yote ya kimanyema yaliacha mila zao za 'MWAMI SING' na 'BAMI PLU' na makabila yote ya Kimanyema yalijikita katika uzungumzaji wa lugha ya kiswahili, na ndio maana mara nyingi 'waha' hupenda kuwaita wamanyema 'Waswahili' sababu kubwa ni hiyo.

26/07/2019
Want your hotel to be the top-listed Hotel in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


ILEMELA
Mwanza