Islamic knowledge Tanzania

Islamic knowledge Tanzania

Share

A PAGE CREATED FOR PROVIDING SOCIAL NETWORKING ISLAMIC REMINDER'S DAILY FROM QURAN-L -MAJID. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Amesema Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 89:

“Iwapo mtu atanunua bidhaa katika vyakula ambavyo ni muhimu katika jamii na akakificha kwa siku arobaini kwa matumaini kuwa bei yake itapanda miongoni mwa Waislam, na k**a atafanikiwa kukiuza kwa bei ya juu hicho chakula basi k**a f

27/09/2025

Maasha Allah karibu sana Ustaadha & Ustaadhat kwapamoja katika lengo la jifunza na kujikumbusha yale aliotuamrisha na kutukataza mwenyezimungu katika kuiendea pepo yake siku ya mwisho: Mohamed Kazungu, Husna Chota, Minaaa, Rama Hamisi

18/03/2025

Usiku wa Qadr unakuwa katika zile nyusiku kumi za mwisho Ramadhaan

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya I´tikaaf lile kumi la katikati la Ramadhaan. Mwaka mmoja akafanya I´tikaaf mpaka ilipofika usiku wa tarehe ishirini na moja, asubuhi ambayo kikawaida ndio anatoka kwenye I´tikaaf yake,

*akasema: “Yule mwenye kutaka kufanya I´tikaaf basi afanye I´tikaaf katika zile siku kumi za mwisho. Nimeota juu ya usiku huo kisha nikausahau. Nimejiona asubuhi nikisujudu ndani ya maji na udongo. Utafuteni katika zile siku kumi za mwisho na utafuteni katika zile nyusiku za witiri.”*

Usiku huo kukanyesha. Msikiti ulikuwa k**a paa na maji yakanyesha juu yake. Nikaona namna ambavo paji la uso la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lilikuwa na athari ya maji na udongo baada ya asubuhi ya tarehe ishirini na moja.”
Hadiyth hii inajulisha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya I´tikaaf zile siku kumi za katikati za Ramadhaan ili kutafuta usiku wa Qadr.

Muundo huu unaonyesha kwamba alifanya hivo mara nyingi.
al-Bukhaariy na Muslim wako upokezi mwingine unaosema kwamba alifanya I´tikaaf zile siku kumi za mwanzo halafu ndio akafanya I´tikaaf katika zile siku kumi za katikati.

Kisha akasema:
*“Nimejiwa na kuambiwa kwamba ni katika zile siku kumi za mwisho* *Yule miongoni mwenu anayetaka kufanya I´tikaaf basi afanye hivo.”*

Haya yanajulisha kwamba yalifanyika kabla ya kubainikiwa kwamba ni katika zile siku kumi za mwisho. Baada ya kubainikiwa alikuwa akifanya I´tikaaf katika zile siku kumi za mwisho mpaka alipoondoka duniani.”

Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Latwaa’if-ul-Ma´aarif, uk. 242
Imechapishwa: 16/05/2020
https://firqatunnajia.com/usiku-wa-qadr-unakuwa-katika-zile-nyusiku-kumi-za-mwisho-ramadhaan

al-Firqah an-Naajiyah 18/03/2025

01. Hukumu ya Tarawiyh na idadi ya Rak´ah zake

Aliulizwa muheshimiwa Shaykh al-´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) swali lifuatalo: Ni ipi hukumu ya swalah ya Tarawiyh? Ni ipi Sunnah juu ya idadi ya Rak´ah zake?

Akajibu ifuatavyo: Swalah ya Tarawiyh ni Sunnah aliyoisunisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya ummah wake. Alisimama kuswali na Maswahabah zake nyusiku tatu lakini baadaye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaacha kufanya hivo kwa kuchelea isije kufaradhishwa juu yao.

Kisha baada ya hapo waislamu wakabaki katika hali hiyo katika zama za Abu Bakr na katika uongozi wa ´Umar. Baada ya hapo kiongozi wa waumini ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) akawakusanya kwa Tamiym-ud-Daariy na Ubay bin Ka´b. Wakawa ni wenye kuswali kwa mkusanyiko mpaka hii leo na himdi zote anastahiki Allaah.

Kwa hivyo imependekezwa katika Ramadhaan.
*Kuhusu idadi ya Rak´ah zake ni Rak´ah kumi na moja au Rak´ah kumi na mbili. Hii ndio Sunnah katika jambo hilo. Lakini endapo mtu atazidisha juu ya hizo hakuna neno wala ubaya*

Kwa sababu kumepokelewa juu ya hilo kutoka kwa Salaf aina mbalimbali katika kuongeza na kupunguza. Hakuna baadhi ambao waliwakemea wengine. Kwa hivyo asikaripiwe yule ambaye atazidisha ijapo bora ni kwa yule ambaye atakomeka na ile idadi iliopokelewa.

Isitoshe Sunnah pia imejulisha kwamba hakuna ubaya kuzidisha. al-Bukhaariy na wengineo wamepokea kupitia kwa Ibn ´Umar ambaye amesimulia kuwa kuna mtu alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu swalah ya usiku ambapo akajibu:
“Ni [Rak´ah] mbilimbili. Atakapochelea mmoja wenu Subh basi ataswali [Rak´ah] moja ili kuwitirisha yale aliyoswali.”[1]

Hakuweka kikomo cha idadi maalum (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambacho mtu atafupika kwacho. Lakini lililo muhimu katika swalah ya Tarawiyh ni unyenyekevu na utulivu katika Rukuu´, Sujuud na wakati wa kuinuka kutoka katika Rukuu´ na Sujuud.

*Mtu asifanye ile haraka ya spidi inayofanywa na baadhi ya watu ambayo inawakosesha waswaliji kufanya yale mambo yaliyosuniwa*

Bali huenda spidi yake ikawakosesha kufanya yale mambo yaliyowajibishwa kwa ajili ya kupupia awe wa kwanza kutoka kwenye misikiti ili watu wapate kukusanyika kwake kwa wingi zaidi. Kitendo hichi ni chenye kwenda kinyume na yale yaliyowekwa katika Shari´ah.

Ni lazima kwa imamu kumcha Allaah juu ya wale walioko nyuma yake na asirefushe urefushaji ambao unawatia uzito unaotoka nje ya Sunnah k**a ambavo pia asiwepesishe uwepesi ambao unaharibu yale mambo ya wajibu au yaliyosuniwa kwa wale walioko nyuma yake.

Kwa ajili hii wanachuoni wamesema:
“Imechukizwa kwa imamu kufanya haraka itakayowakosesha waswaliji kufanya yale yaliyopendekezwa.”
Tusemeje kwa wale wanaofanya haraka inayowakosesha waswaliji kufanya yale ambayo ni ya wajibu?

Hakika haraka k**a hii ni ya haramu juu ya imamu huyu. Tunamuomba Allaah atupe sisi na ndugu zetu msimamo na usalama.

[1] al-Bukhaariy (990) na Muslim (1695).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 05-06
Imechapishwa: 02/04/2022
https://firqatunnajia.com/01-hukumu-ya-tarawiyh-na-idadi-ya-rakah-zake/

al-Firqah an-Naajiyah Uislamu kwa ufahamu wa Salaf

Home - al-Firqah an-Naajiyah 20/03/2024



*al-Waadi´iy mgonjwa wa pumu kutumia sprei mchana wa Ramadhaan*

*Swali:* Ni ipi hukumu ya kutumia sprei kwa watu wanaopata ugumu wa kupumua?

*Jibu:* Udhahiri ni kwamba sio chakula wala kinywaji. Kwa hivyo sitambui kuwa inaharibu swawm.

*Mhusika:* ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
*Mfasiri:* Firqatunnajia.com
*Marejeo:* Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 80-81
*Imechapishwa:* 18/03/2024

https://firqatunnajia.com/al-waadiiy-mgonjwa-wa-pumu-kutumia-sprei-mchana-wa-ramadhaan/

Home - al-Firqah an-Naajiyah Sasa Jiunge na sisi Previous Next [metaslider id=”92474″] Makala Makala zaidi … Darsa Darsa zaidi … Video Video zaidi … Dawrah/Nad-wah Dawrah/Nad-wah zaidi … Khutbah Khutbah zaidi … Mihadhara Mawaidha zaidi … Ruduud Ruduud zaidi … [metaslider id=”27421″] Ratiba ya Darsa za live...

Want your establishment to be the top-listed Arts & Entertainment in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


FaruHost, Rock City Mall, 2nd Flor, Mwanza Ilemera
Mwanza