Famara Media

Famara Media

Share

07/07/2026

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeimarisha hali ya usalama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo.

​Kupitia taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa, aliyoitoa leo Julai 07.2026, amesema Jeshi la Polisi limeimarisha hali ya usalama kwa kuwapanga askari katika maeneo muhimu, lengo kubwa likiwa ni kulinda watu na mali zao.

​Katika maadhimisho ya Siku ya Maonesho ya Biashara na Maendeleo ya Kiuchumi (Sabasaba), Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi kutokuwa na hofu yoyote, kwani ni wajibu wa Jeshi la Polisi kulinda usalama wao.

Amesisitiza kuwa wasiogope kuona ongezeko la askari mitaani, bali wafurahi kwa sababu uwepo huo ndio unaohakikisha usalama wa maisha na mali zao.

​Aidha, Kamanda Mutafungwa ametoa wito kwa watu wenye nia ya kusababisha uvunjifu wa amani kuacha mara moja, kwani Jeshi la Polisi limejipanga imara na yeyote atakayejaribu atadhibitiwa kwa mujibu wa sheria.

​"Kwa kweli hatutaruhusu mtu yeyote afanye vitendo vya uvunjifu wa amani; atadhibitiwa kisheria na kwa nguvu kubwa," amesema Kamanda Mutafungwa.

​Pia, amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha usalama na kufuatilia kwa karibu taarifa za wahalifu zinazotolewa na wananchi wema.

Want your business to be the top-listed Media Company in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Nyamagana
Mwanza
994