De Opera
20/01/2026
Hakuna aliyemkamilifu ila kuna mambo hayana budi kukamilika abadani.
De Opera/
on social networks.
Siraj Kingi
11/12/2025
KABLA HAMJAWEKA AGANO, NG'AMUA HILI.
Kiapo ni nini?
Hii ni ahadi ya kuonesha ukweli au uaminifu, inayotamkwa mbele ya mtu, watu, au mamlaka fulani. Ni maneno yanayoweza kutamkwa kwa sababu yoyote, hata bila ukweli wa moyoni.
Agano ni nini?
Ni kubaliano maalum kati ya pande mbili au zaidi, lenye masharti, ahadi, na wajibu ambao kila upande unakubali kuufuata. Ni k**a mkataba, lakini mara nyingi huwa na uzito wa kiroho, kiimani, au uaminifu wa juu.
Kuna mtu mmoja aliniuliza, "Wanandoa hula kiapo au hufanya Agano?"
Jibu langu ni kwamba:
Soma hapa... https://deoperahub.blogspot.com/2025/12/kabla-hamjaweka-agano-ngamua-hili.html
10/12/2025
NAMNA YA KUJITOA KWA WATU SAHIHI (A true selfless sacrifice)
Mwenye njaa hawezi kukaa ndani, hata akizuiwa lazima atatoka tu. Akitaka kutoka akaambiwa rudi ndani, lazima atauliza 'mpaka muda gani'? 'Nitatoka saa ngapi?', 'Mi sijazoea kukaa ndani' na mara nyingi utamkuta yupo dirishani anachungulia nje. K**a hawezi kulifikia dirisha, basi yeye hukaa mlangoni akisikiliza k**a kuna mtu anakuja kufungua na hapo ukienda kufungua mlango ghafla, atapata umemng'oa kucha.
Hii inatufunza nini?
kuna baadhi ya watu wakiwa na nia huwa hawana subira, na mara nyingi huonekana wasumbufu na ndio hufanikiwa. Unaweza ukaminya mwisho wa siku utakubaliana.
Watu wengi wenye mipango thabiti, huwapima watu kwa nia na uwajibikaji.Hii ni k**a kumpa au kumuahidi chakula aliyeshiba. Hawezi kuona kinachelewa, hata ukimuambia atakula wakati mwingine, yupo tayari kusubiri. Hawezi kukusumbua. Unaweza dhani ni mtulivu, la hasha! hakuna utulivu penye njaa. Kwa hiyo k**a ni mtu mwenye malengo huangalia mwenye njaa kwa sababu huyo atakuwa na moyo wa kupambana na mwenye kuleta mipango mipya njinsi ya kuidhibiti njaa.
SOMA ZAIDI... https://deoperahub.blogspot.com/2025/12/namna-ya-kujitoa-kwa-watu-sahihi-true.html
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Mwanza