Majengo

Majengo

Share

18/10/2024

Hello habari

12/10/2021

JE UNAFAHAMU KUNA MAKUNDI KADHAA YA KUUMA KICHWA❓*

Na makundi hayo yamegawanywa ifuatavyo kutokana na visababishi.

¶. Maumivu ya kichwa ya awali (Primary headache)
- Haya ni maumivu ambayo husababishwa na kuongezeka kwa hisia za maumivu katika viungo vinavyotaambua maumivu ndani ya ubongo.

Maumivu haya ya awali hayamaanishi kuwa kuna ugonjwa unaendelea.

Mfumo wa kemikali katika ubongo, mishipa ya fahamu, mishipa ya damu ya nje ya fuvu ama misuli ya shingo na kichwa huchangia katika kusababisha maumivu ya kichwa ya awali.

Baadhi ya watu wamebeba vinasaba vinavyosababisha wao kupata maumivu haya maishani mwao.

Aina hii ya maumivu ya kichwa nayo imegawanyika katika makundi makubwa mawili

1. Kipandauso (Migrain)
- Aina hii ya maumivu ya kichwa ya awali ndiyo iliyoenea sana na watu wengi wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara huwa na tatizo hili.
- Maumivu haya yanaweza kuwa ya upande mmoja; lakini yanaweza kuwa katika paji la uso pia na kusikika katika eneo lote la paji la uso, na shingo.

Aina hii ya maumivu ya kichwa huwa ni ya “kichwa kugonga” (throbbing pain) na huambatana na dalili k**a vile kichefuchefu au kutapika, kizunguzungu, macho kushindwa kuona vizuri, macho kuuma yanapoangalia mwanga.

- Aina hii ya maumivu ya kichwa huzidishwa na kutembea au kujisogeza kwa namna yoyote, na mgonjwa hujisikia nafuu akipumzika/kulala kwa kawaida, maumivu haya huwa makali kwa muda wa masaa 1-2, na yanaweza kuchukua kati ya saa 4 hadi 72.

Vitu ambavyo huweza kusababisha mtu mwenye tatizo la migraine kuanza kuumwa kichwa (triggers) ni k**a vile vinywaji vyenye kemikali ya caffeine au pombe/sigara, mawazo, uchovu/usingizi, hasira, kwa kinadada k**a akiwa anakaribia siku zake, au kwenye siku zake, mwanga mkali/sauti.

- Aina hii ya maumivu ya kichwa pia huwasumbua zaidi wanawake ambao wako katika umri wa kuweza kushika mimba ambao ndio wameanza kupata hedhi zao kipindi cha karibuni.

Pia migraine huweza kurithiwa kutoka kwa wazazi kwa sababu mara nyingine husababishwa na vitu ambavyo viko kwenye vinasaba (genetics) za uzao husika.

Pia aina hii ya maumivu ya kichwa mara nyingi hutanguliwa na dalili za kabla (aura), ambazo hutokea kwa kati ya dakika 5-20, na hudumu si zaidi ya dakika 60; dalili hizi za kabla zinaweza kuwa kizunguzungu, kichefuchefu,mwili kukosa nguvu, n.k.

Maumivu mkazo (Tension Headache
Aina hii ya maumivu ya kichwa kwa kawaida huwa ni ya ‘kugandamiza/kukaza (pressing/tightening), na huwa yanatokea kwenye pande zote za paji la uso kuelekea utosin (frontal-occipital) na hayazidi pale mgonjwa anapotembea/kujisogeza (tofauti na migraine).

Aina hii ya maumivu ya kichwa yanaweza kudumu kwa kati ya dakika 30 hadi siku 7; Na hayaambatani na dalili za kichefu-chefu/kutapika/kizungu-zungu k**a ilivyo kwa migraine!! Pia hakuna dalili za awali (aura).

Mara nyingi maumivu haya huanza pale mtu anapokuwa na msongo wa mawazo; na huambatana na kukosa usingizi (insomnia).

2. Maumivu ya kichwa ya upili (Secondary headache)
- Aina hii ya maumivu ya kichwa husababishwa na tatizo lingine amblo lipo ndani ya mwili na mgonjwa hupata maumivu haya k**a matokeo ya tatizo hilo lingine mwilini.

Maumivu ya kichwa ya aina hii kwa kawaida huambatana na dalili zingine ambazo nazo zimekuwa zimesababishwa na tatizo la msingi.

Dalili hizo ni;

~ Maumivu ya viungo/mifupa
~ Kuishiwa damu
,~ Homa,
~Kupungua uzito
~Dalili za mfumo wa fahamu (kuchanganyikiwa, kuzimia, kupungua kwa hali ya ufahamu, macho kushindwa kuona, mwili au sehemu ya mwili kupooza)
~ Maumivu mapya ya kichwa kwa mtu mwenye umri wa miaka 50 na zaidi ambaye hakuwahi kuwa na tatizo la maumivu ya kichwa
Historia ya kuwahi kuumia kichwa/kupata ajali ya kichwa.

Mara nyingi, visababishi vya maumivu ya aina hii ya kichwa huwa ni k**a ifuatavyo,

~ Presha ya kupanda/kushuka,
~ matatizo ya mishipa ya fahamu,
~ Maambukizi ya bakteria/virusi
~ Upungufu wa maji mwilini (dehydration)
~ Saratani ya ubongo,
~ Matatizo ya macho,
~ Kiharusi.
~ Damu kuvilia kwenye ubongo

⚠️TUNALO SULUHISHO...NIELEZE NIKUSAIDIE

Piga simu 0623992857 au njoo moja kwa moja WhatsApp

09/07/2019

KUIJENGA NAFSI KIROHO ... HUSUSAN KWA MASHEIKH:
__MASHEIKH WALIO WENGI WANAFELI WAPI?!
Nadhani ni hapa: Masheikh wengi Duniani wanafeli kwa sababu ya kutokujiimarisha KIROHO na kupuuza ujenzi huo wa Kiroho.
Ujenzi wa ROHO au NAFSI ni jambo muhimu sana ... bali Uislamu umeupa ujengaji wa nafsi/roho daraja ya juu sana .. Kwa sababu:
Tabia Njema
Hupatikana kwa mja kupitia kuijenga vyema nafsi ... K**a alivyosifiwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w):
"وَ إِنَّکَ لَعَلى خُلُقٍ عَظيمٍ"
Aya hiyo Tukufu ipo katika kuisifu Akhlaq ya Mtume (s.a.w.w) ili WAISLAMU wasome SIRA YAKE na wajipambe kwa Akhlaq yake nzuri.
Unapoijenga nafsi/roho ... Inakuwa na tabia ya Kumuogopa Allah (s.w) kwa kila kitu ... Sababu umeipa malezi hayo ikatambua kuwa hapa katika hili au lile baya nikilifanya Allah (s.w) ananiona.
بناء النفس Maana yake:
Wewe Mja umechagua Kumcha Allah (s.w) katika kila jambo lolote na unataka moyo wako uwe laini na ukae tayari kufuata maelekezo yote ya Allah (s.w).
Hivyo ndivyo alivyokuwa Mtume wetu Muhammad (s.w) na Maimam wetu watukufu (a.s).
Kwa mantiki hiyo:
Tukijua WAISLAMU kuna umuhimu wa kuijenga Tabia njema kupitia kuzijenga nafsi zetu ziimarike KIROHO ... Tutatambua na kufuatilia vitu au matendo ambayo ni msaada mkubwa katika kuijenga nafsi k**a vile: ✅Kusoma sana Dua mbalimbali zilizojaa ndani ya vitabu vyetu vingi vya dua.
Zinajenga nafsi ya mja na kuikomoza Kiroho na kuivusha kuipeleka katika level nyingine kabisa ya mbali mpaka kuwa karibu zaidi na Allah (s.w).
✅Kuisoma sana mara kwa mara Qur'an Tukufu.
✅Kuvisoma sana mara kwa vitabu vya Maulamaa vilivyoandika katika AKHLAQ.
✅Tukiweza tusome sana kitabu kinachoitwa:
Jaamius_Saadaat👇🏽
جامع السعادات
✅Swala nyingi ambazo sio za wajibu/bali Mustahabu tuzifanye kwa wingi sana ... Zinajenga nafsi na kuzitakasa. Na mengine yasokuwa hayo.
Masheikh wengi Duniani hufeli kwa kupuuzia kwao ujenzi wa nafsi bali utakaso wa nafsi ... Wakiamini inatosha kwao kuwa Masheikh na kwamba ndio basi wamemaliza kila kitu!. Kuwa Sheikh ni jambo lingine ... na kuutwabikisha Usheikh katika matendo yetu ya kila siku katika maisha yetu ni jambo lingine ... Hata Masheikh wapo wengi sana watakao tumbukia motoni ... Atakaye faulu ni yule tu aliyejikurubisha kwa Allah (s.w) kwa kuitaka nafsi yake.
\Na ndio katika Qur'an Tukufu Allah (s.w) hasemi atakaye kuwa Sheikh amefaulu sana ... Bali Aya imesema kuhusu nafsi kuzitakasa kwamba:
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا
"Kwa hakika ... Atakuwa amefaulu atakaye itakasa nafsi[yake]."
Kwa nini ni muhimu sana Masheikh kuzijenga NAFSI?! Ni ili wawe mwanga kwa wasio kuwa na elimu ... Vinginevyo: Sheikh / Aalim akiacha mfano Swala za Sunna asiyekuwa Sheikh ataacha swala za wajibu ... Au Sheikh akitukana mtu ... Asiyekuwa Sheikh ndio ataua kabisa mtu ... Hivyo kwa daraja ya kwanza: Sheikh kuijenga nafsi / ujenzi wa Kiroho ni muhimu mno kabla ya mtu yeyote yule ... Sababu Aalim ndiye anayetegemewa na mwenye wadhifa mkubwa wa kuiongoza Jamii Kiroho.
BY USTADH SHABANI NDOGHWE

Want your organization to be the top-listed Government Service in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Moshi