MBUKE TIMES

MBUKE TIMES

Share

26/06/2021

It won't be easy. You will need some waiting time. But if you wait long enough, and do what is required while you wait, you will get the reward. And that's Entrepreneurship.

31/12/2020

Kheri ya mwaka mpya 2021. Mungu akujalie furaha, na baraka tele.

27/11/2020

MITANDAO YA KIJAMII INAKUINGIZIA KIPATO?
Unachohitaji sio tuu kupost bidhaa au huduma zako.
Ili mitandao ya kijamii ikuletee faida, unapaswa ujikite kwenye kuwanufaisha walengwa wako kupitia machapisho yako.
Na kingine unahitaji kujikita kwenye kujenga brand bora ili uaminike, na uwafikie watu sahihi, na washawishike kufanya biashara nawe.
Kuna mengi ya kufanya ili ujiweke kwenye nafasi nzuri ya kuaminika, na kushawishi watu. Maandishi ya kile unachotaka kuwaambia watu, ubora wa picha unazotumia ni baadhi tuu ya mambo unayopaswa kuzingatia.
Kwa msaada zaidi tuwasiliane.

03/08/2020

NJIA ZA KUPATA JINA LA BIASHARA AU BRAND YAKO ( Sehemu ya 1)
Kwenye kupata jina la biashara kuna mambo mawili ya kufahamu. Kwanza kuna mitindo inayotumika kupata jina, halafu kuna vigezo vya kuzingatia jina unalolibuni linakua navyo ili liwe na mashiko na kukuletea manufaa.

Post hii inaangalia TUU MITINDO ya kupata jina, siku nyingine tutaangalie VIGEZO vya kuzingatia. Post hii ni muhtasari wa mojawapo ya sura za kitabu chetu cha MUONGOZO WA BRANDING KWA MJASIRIAMALI.

Ni muhimu upate nakala yako ya hicho kitabu kina mambo mengi sana yatakayokufanya ujenge brand bora kwa ajili ya biashara yako.

1. Tumia lugha ya kilatini kutafsiri maana fulani
Njia hii inakutaka kwanza uwe na wazo fulani kuhusu jina la biashara. Mfano unawaza kuwa ufungue kampuni ya utalii ambayo itajikita pia na kuhakikisha unatunza mazingira.

Hivyo basi kwakua wazo kuu ni kutunza mazingira, unaingia mtandaoni na kusearch maana ya neno mazingira kwa kilatin, unakuta kuwa na AMET, hivyo unaamua kuiita kampuni yako AMET ADVENTURES. Huu ni mtazamo tuliotumia kumtengenezea mteja wetu wa Kenya hilo jina la biashara yake, ikaitwa Amet Adventures.

Mifano mingine, bila shaka umeona magari yanayotumia jina la AUDI. Hili jina ni la kilatin, ambalo ni tasfiri ya jina ukoo la mwanzilishi wa hiyo kampuni ya AUDI. Yeye mwanzilishi anaitwa August Horch, hivyo alitamani aite kampuni yake Horch ila kwa kilatin, ndio maana akaiita AUDI.

--Somo litaendelea. Na waweza jipatia kitabu chetu cha BRANDING ujisomee mengi kuhusu branding.

Want your business to be the top-listed Business in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Soweto
Moshi
00255