Kasherente TV
🚨 MLIMA EVEREST SI SEHEMU YA UTALII WA KAWAIDA... NI ENEO LA MAPAMBANO YA MAISHA NA KIFO! 🏔️🥶💔
Kila mwaka mamia ya watu husafiri kwenda kupanda Mlima Everest wakiamini ndoto zao zitatimia, lakini wengi hukutana na hali za kutisha ambazo hawakuwahi kuzifikiria. Upepo mkali wenye kasi kubwa unaweza kumwangusha mpandaji ndani ya sekunde chache, huku nyufa kubwa zilizofunikwa na barafu (crevasses) zikimeza watu bila onyo.
Katika maeneo ya juu, joto kali la baridi na ukosefu wa oksijeni humfanya mtu ashindwe hata kufikiri vizuri.
Wapo walioteleza na kusombwa na miteremko ya barafu, huku wengine wakipotea kabisa ndani ya nyufa za barafu ambazo ni vigumu kufikiwa.
Everest ni mlima wa ndoto kwa wengi, lakini pia ni moja ya maeneo hatari zaidi duniani. Kila hatua inapigwa kwa umakini, kwa sababu kosa moja dogo linaweza kubadilisha safari ya mafanikio kuwa simulizi la kusikitisha milele.
13/07/2026
Lionel Messi ameonesha hasira yake kwa mwamuzi wa Ureno, João Pinheiro, na kumtaka ampe heshima wakati wa mechi kati ya Argentina na Uswisi.
Wakati wa mchezo huo Messi alionekana kuchoshwa na namna mwamuzi alivyokuwa akizungumza naye ndipo akaamua kumtolea uvivu moja kwa moja.
🗣️ "Ongea nami kwa heshima, tafadhali!"
"Usinikosee heshima. Mimi ninazungumza nawe kwa heshima." alisema Messi
Lionel Messi ni miongoni mwa wachezaji wanaojulikana kwa utulivu wao wanapokuwa uwanjani, hivyo kumuona akipandisha hasira na kumkabili mwamuzi si jambo la kawaida.
Tukio hilo limewashangaza mashabiki wengi na kuzua mjadala mkubwa mitandaoni.
✍
| |
Timu ya Urusi ya ulinzi wa anga ya mkononi (mobile air defense) iliyokuwa ikifanya mazoezi na bunduki ya mashine ya YakB-12.7 iliishia kwenye vurugu na mtafaruku mkubwa baada ya mfyatuaji (gunner) kukaribia kumuua mwalimu wake mwenyewe.
Sababu ya tukio hili ni rahisi ya kushangaza:
Kuna mtu aliona ni wazo zuri kuifunga YakB-12.7 — bunduki ya mashine inayozalisha nguvu kubwa ya mtikisiko wa nyuma (recoil force) wa karibu kilo 1,400 (k**a tani 1.4) — kwenye mnara unaozunguka (turret) ambapo mhimili wa mtungi wa bunduki (barrel's axis) umepishana na mhimili wa mzunguko wa mnara huo. YakB-12.7 ndiyo silaha kuu ya mfumo wa USPU-24 unaotumika kwenye helikopta ya mashambulizi ya Mi-24.
Tuandikie Maoni Yako juu ya tukio hili 👇👇 usisahau kutufollow Kamusi Ya Mtaa
This video doesn't support violence it's for give people awareness only and not spreading violence
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Moshi