Matukio Halisi
18/12/2021
MIAKA 700 YA WACHAGGA - 58
ANGUKO LA MIFUMO YA UTAWALA KILIMANJARO.
ELIUFOO SOLOMON, KIBARAKA WA CHAMA CHA TANU ALIYETUMWA KUIDHOOFISHA KILIMANJARO.
Miaka ya 1950’s wachagga tayari walikuwa wamejenga mifumo imara sana ya kiuchumi na kisiasa kwa zaidi ya miaka 30, tangu miaka ya 1920’s na tayari walikuwa mbele sana kimaendeleo ukilinganisha na jamii nyingine Afrika kwa nyakati hizo.
Kufikia miaka ya 1950’s wachagga walikuwa kati ya jamii zinazojitambulisha k**a nchi au taifa japo hawakuwa wamepata uhuru kutoka kwa Waingereza lakini wakiwa wamepiga hatua kubwa kiuchumi na kuimarisha taasisi za kiuchumi na kiutawala wakiendelea kupiga hatua kwa kasi kubwa.
Ni katika miaka hii ya 1950’s wakati wachagga tayari hata kisiasa wakiwa wameshakomaa sana ndipo maeneo mengine hususan makao makuu ya serikali ya kikoloni Dar es Salaam ambapo watu walikuwa wanaendelea kuimarisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika yote.
Harakati hizi za uhuru wa Tanganyika kupitia vyama mbalimbali k**a chama cha United Tanganyika Party(UTP), TAA na baadaye TANU ambacho kilianzishwa Dar es Salaam na kuenea baadhi ya maeneo ya nchi kilishindwa kuingia kujiimarisha Kilimanjaro kwa sababu wachagga walijiona tayari wao ni taifa na wana nchi inayofanya kazi kwa usahihi kabisa ikisubiri kupatiwa uhuru wake na hivyo hawakuhitaji taasisi nyingine yoyote inayofanya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kuingia Kilimanjaro kwa sababu maisha yenyewe ya wachagga yalikuwa tayari ni mazuri na maendeleo yalikuwa yakienda kwa kasi kuliko eneo jingine lolote.
Kwa kuwa pia mfumo wa kisiasa ulikuwa imara hakuna mtu aliyejihangaisha na harakati nyingine za kisiasa zaidi ya siasa za ndani ya Kilimanjaro lakini zaidi wachagga walijihusisha na shughuli za kiuchumi na maendeleo ya Kilimanjaro.
Chama cha TANU kilipojaribu kuingia Kilimanjaro bila mafanikio na kuona kwamba aidha kinaweza kushindwa kukabidhiwa uhuru wa Tanganyika au kukabidhiwa uhuru wa Tanganyika huku Kilimanjaro ikiachwa nje ya Tanganyika ndipo kilitengeneza agenda ya siri ya namna kuidhoofisha Kilimanjaro kwa kutumia makada wa chama cha TANU kutoka Kilimanjaro waliokuwa nje ya Kilimanjaro kimasomo.
Eliufoo Solomon alikuwa ameshawishiwa kujiunga na tawi la TANU akiwa anasoma chuoni Makerere Uganda wakati huo kabla hajaenda kusoma Marekani na hivyo baada ya kutoka Marekani ilikuwa rahisi kumshawishi kujipenyeza ndani ya siasa za Uchaggani, Kilimanjaro akiwa k**a kada wa TANU na akifanya kazi kwa maslahi ya chama cha TANU badala ya maslahi ya wachagga Kilimanjaro.
Hivyo mara baada ya Eliufoo Solomon kuingia kwenye nafasi ya urais wa Wachagga na kutakiwa kutoa mwongozo kwa baraza la halmashauri kuu ya wachagga ndipo nia yake na agenda zake za siri alizobeba na chama cha TANU zilianza kuonekana wazi. Kwa wale waliopigia kura chama cha kiliberali cha (CDP) kwa kuvutiwa na sera zao dhidi ya chama kikongwe zaidi cha wachagga wahafidhina (KCCU) walikuwa na matarajio makubwa zaidi na matumaini makubwa zaidi ya ustawi wa Kilimanjaro kuliko kipindi kilichoisha cha Mangi Mkuu wa wachagga, lakini hata hivyo mambo yalienda tofauti na matarajio yao ambapo kimsingi ilikuwa ni kinyume chake.
Ilikuja kuwa wazi kwamba Eliufoo Solomon alikuwa anatumiwa na watu kutoka nje ya Kilimanjaro kwa maslahi yao akiwa k**a kibaraka na kada wa chama cha watu hao. Licha ya kampeni kubwa alizofanya kupitia chama cha CDP, Eliufoo Solomon hakuwa na maono yoyote ya kisiasa wala kiuchumi kwa wachagga Kilimanjaro na hakuwa na jambo lolote alilokuwa amepanga kusaidia juu ya wachagga katika mipango yake.
Baada ya kufanikisha alichokuwa ametumwa na watu wa kutoka nje ya Kilimanjaro aliacha kujihusisha na siasa za Kilimanjaro mara moja na pia kuacha kushiriki mikutano ya baraza la halmashauri kuu ya wachagga na hata kutelekeza ofisi aliyokabidhiwa na wachagga ya urais wa wachagga bila kusema lolote, kitu ambacho kilionekana ni usaliti mkubwa sawa na kosa la uhaini kwa wachagga.
Badala yake Eliufoo Solomon aliondoka na kuelekea Dar es Salaam kujihusisha na shughuli za chama cha TANU akiwa k**a kada wake na hivyo kuacha ombwe la uongozi akiwa k**a kiongozi mkuu aliyechaguliwa na wachagga Kilimanjaro.
Mfumo wa uongozi wa wachagga chini ya Mangi Mkuu wa wachagga na baraza la Halmashauri kuu ya wachagga ulikuwa ni mfumo bora sana wa kisiasa uliloleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kisiasa na wa kupigiwa mfano ukilinganisha na sehemu yoyote Tanganyika na hata katika bara la Afrika, lakini waliokuwa wanafikiri kunahitajika mabadiliko ni watu ambao hawakuwa na uelewa mpana wa hatua kubwa ambayo wachagga walikuwa wamepiga kupitia mfumo huu.
Hivyo kitendo cha Eliufoo Solomon kutelekeza wachagga na kuwaacha kwenye mataa akiwa k**a Rais wa serikali ya wachagga ilikuwa ni kitendo cha kuhujumu mfumo uliokuwa na nguvu na uliokuwa na manufaa makubwa kwa watu wa Kilimanjaro.
Wachagga wengi na hasa watu wazima walikasirishwa sana na namna Eliufoo Solomon alivyofanya baada ya kupewa nafasi ya kuwa Rais wa wachagga na baadhi ya waliomuunga mkono kwenye harakati za mabadiliko walilalamika kwamba wametumika katika kumsaidia kufanikisha agenda zake binafsi.
Baadhi ya wazee waliomlaani na kumuona k**a msaliti na mhuni walisema sio kwamba walikuwa wanapingana na yeye kushiriki kwenye harakati za TANU bali namna alivyotumika na watu wa TANU alifanya wachagga waonekane ni wajinga, kwani angeweza kuchagua kimojawapo cha kufanya badala kuwafanya watu wajinga na kuwaacha kwenye mataa kwa sababu baada ya Mangi Mkuu aliyekuwa anajituma sana na aliyekuwa anapambana sana kwa ajili ya maendeleo ya Kilimanjaro kuondoka kwenye kiti hicho wachagga waliachwa njia panda kwani hakukuwa na kiongozi mwenye maamuzi ya mwisho wa kuonyesha njia.
Kitendo cha kwamba watu wa chama cha TANU walikuwa wakifanya kazi nyuma ya Eliufoo Solomon na chama cha CDP kikiwa k**a tawi dogo la TANU wakiwa na agenda za kuhujumu maendeleo ya Kilimanjaro moja kwa moja kwa maslahi yao binafsi hakikumpa nafasi Eliufoo ya kuweka akili yake katika maendeleo ya Kilimanjaro na kuishia kufanya kinyume chake.
Wazo pia la kuwa na Rais wa wachagga lilikuwa wazo geni kutoka nje ya Kilimanjaro, lisiloendana na tamaduni, mila na desturi za wachagga na ambalo wachagga wengi walikuwa bado hawawezi kulihisi k**a lina mamlaka fulani k**a jinsi lilivyokuja tofauti na cheo cha umangi ambacho ni cha asili ya wachagga kwa karne nyingi nyuma.
Hata madhara ya kukosekana kwa uongozi imara na thabiti Kilimanjaro yalianza kuonekana huku baraza la Halmashauri kuu ya wachagga likijiongoza lenyewe. Kukosekana kwa uongozi thabiti kulipelekea ari na hamasa kupungua kiasi na kasi ya maendeleo pia kuanza kupungua. Kilimanjaro ilikuwa ni sehemu ya mwisho ambayo chama cha TANU kilikubaliwa kuingia baada ya njama za kisiasa zilizosukwa kuangusha utawala wa Mangi Mkuu kufanikiwa na hivyo kuwa sehemu ya Tanganyika.
Wafuasi walipiga kura ya maoni kuunga mkono sera za chama cha CDP pamoja na wachagga kwa ujumla wakiwa na hamasa na matumaini makubwa kuliko siku bora zilizopita na kutegemea umoja zaidi, mshik**ano zaidi demokrasia na ustawi zaidi Kilimanjaro.
Lakini Eliufoo Solomon hakujihangaisha kuchukua muda kupitia sera zake na kuishauri serikali ya Tanganyika baada ya uhuru ambayo alipewa zawadi ya uwaziri wa elimu kutekeleza baadhi ya ahadi zake Kilimanjaro. Eliufoo Solomon alipaswa kufanya hivyo akishirikiana na baraza la Halmashauri kuu ya wachagga baada ya uhuru wa Tanganyika lakini badala yake alijikausha na kuendelea kufanya mambo mengine kabisa.
Hata mfumo wa utawala wa umangi ambao Eliufoo Solomon alitumika kuudhoofisha akishirikiana na chama cha TANU ambapo ulikuwa umeiletea Kilimanjaro maendeleo makubwa na ambao ulikuwa umeboreshwa na kuwa wa kidemokrasia kwa kiasi kikubwa sana mpaka kufikia miaka ya 1950’s ulikuja kufutwa mwaka 1962 mara baada ya waingereza kukabidhi uhuru wa Tanganyika kwa chama cha TANU na kuondoka.
Kulitengenezwa propaganda nyingi sana za chuki dhidi ya mfumo wa utawala wa umangi kwa ajili ya kuudhoofisha bila kujali kwamba mpaka kufikia miaka ya 1950’s mfumo wa utawala wa umangi ulikuwa tayari umeboreshwa sana na ulikuwa tayari ni mfumo wenye demokrasia kubwa na huru kuliko hata Tanzania ya leo.
Japo aliyekuwa Mangi Mkuu wa wachagga alipeleka kesi mahak**ani kuishtaki serikali juu ya kuondolewa kwa mfumo wa umangi na akashinda kesi hiyo, serikali ya awamu ya kwanza ya Tanganyika chini ya Rais Nyerere iliamua kufuta mifumo ya tawala zilizokuwepo kwa ajili ya kupoteza uhalali wa ushindi wa kesi mahak**ani aliyoipeleka Mangi Mkuu wa wachagga juu ya utawala wa umangi.
Hivyo mfumo wa utawala uliokuwepo Kilimanjaro uliokuwa umechanganyika na tamaduni za kichagga na demokrasia ndani yake ambayo k**a tulivyoona ilikuwa ni demokrasia yenye uwakilishi madhubuti kuannzia ngazi za chini kabisa za kiutawala iliyokomaa kuliko hata demokrasia iliyopo Tanzania ya karne ya 21, lakini ilifutiliwa mbali bila huruma bila hata kujali mapinduzi makubwa ya kihistoria ya kiuchumi na kisiasa iliyoyaleta Kilimanjaro kabla ya uhuru wa Tanganyika.
Baada ya mfumo wa kisiasa wa wazawa uliokuwepo kuondolewa mara baada ya uhuru wa Tanganyika ndio ukawa mwanzo wa Kilimanjaro kuletewa viongozi wa kuwaongoza na Rais wa Tanganyika kutoka maeneo mengine ya nchi k**a vile mkuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, makatibu tarafa n.k.,.
Viongozi hawa wa kuletwa na Rais wa Tanganyika/Tanzania kutoka nje ya Kiilimanjaro hawafahamu chochote kuhusu Kilimanjaro kuanzia historia yake katika nyanja zote za kijamii mpaka tamaduni zake na wakiwa hawajachaguliwa na wananchi wa Kilimanjaro hivyo hawana malengo wala maono yoyote juu ya Kilimanjaro zaidi ya kutimiza maslahi na matakwa ya kisiasa na ya kibinafsi ya aliyewaleta Kilimanjaro ambaye ni Rais wa Tanganyika/Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa kwanza Kilimanjaro baada ya uhuru wa Tanganyika aliyeitwa Edward Barongo alikuja na mfumo mpya wa Tanganyika baada ya uhuru na hata mpaka leo Kilimanjaro haijawahi kabisa kuwa na mkuu wa mkoa ambaye ni mzawa wa Kilimanjaro na hata ikitokea akawepo bado ataishia kuwa kibaraka wa aliyemweka hapo madarakani kwa sababu atakuwa ameletwa tu na hajachaguliwa hivyo atalipa fadhila kwa aliyemleta.
Mfumo huu mpya wa utawala wa serikali ya Tanganyika/Tanzania nao umekuwa ni k**a tu ule wa kikoloni wa kuletewa viongozi wa kuwatawala badala ya kuchagua magavana wenu wenyewe kutoka hapo hapo Kilimanjaro ambao ni wazawa wenye kujua historia na tamaduni za Kilimanjaro na wenye uzalendo wa dhati kwa Kilimanjaro na ambao wako kwa ajili ya maslahi ya wananchi wenyewe wa Kilimanjaro tofauti na wale wa kuletewa.
Hata hivyo pamoja na kwamba mfumo wa wakoloni waingereza nao ulikuwa wa kuletewa gavana wa kuwatawala k**a jinsi ulivyo huu wa Tanganyika/Tanzania lakini bado mfumo wa kikoloni wa waingereza ulikuwa na nafuu kuliko huu wa serikali ya Tanganyika/Tanzania kwani angalau ule wa wakoloni waingereza haukuingilia moja kwa moja utawala wa ndani wa wazawa wala kuwaletea viongozi kutoka serikali kuu walioteuliwa na gavana wa Tanganyika k**a ilivyoanza kufanywa na Rais Nyerere baada ya uhuru wa Tanganyika, badala yake serikali ya wakoloni iliwaacha wazawa kutengeneza mfumo wao wenyewe wa kiutawala na kuchagua viongozi wao wenyewe.
Uhuru huu wa wachagga kujitawala wenyewe wakati wa serikali ya waingereza uliwapa fursa wachagga kupiga hatua kubwa kimaendeleo na Kilimanjaro kustawi vizuri na kwa viwango vya juu sana vilivyoweza kuteka umakini wa vyombo vya habari vya kimataifa kabla ya anguko kubwa la kiuchumi lililokuja baada ya uhuru wa Tanganyika kutokana na serikali pamoja na zile taasisi za wazawa zilizoleta maendeleo makubwa Kilimanjaro kuondolewa na kufutwa kabisa kwa hoja kwamba mambo yote yaliyofanyika kabla ya uhuru wa Tanganyika ni ya kikoloni na hivyo kila kitu kinatakiwa kufanyika upya bila kujali ni hatua kubwa kiasi gani ilikuwa imepigwa hapo kabla.
Hata suala la kusifia yaliyofanyika kabla ya uhuru wa Tangayika ilionekana ni kukosa uzalendo kwa serikali mpya ya Tanganyika/Tanzania na watu kwa kuogopa aibu ya kushutumiwa kwamba sio wazalendo waliacha kuzungumzia mambo mazuri yaliyokuwa yamefanywa na wachagga miaka ya kabla ya uhuru wa Tanganyika.
Lakini pamoja na yote hayo yaliyotokea sambamba na propaganda nyingi za kisiasa za kupuuza na kubeza yaliyokuwa yamefanyika, hata hivyo kamwe haziwezi kusahaulika hatua kubwa za kimaendeleo katika kila nyanja ya maisha ambazo wachagga walikuwa wamepiga chini ya utawala wa Mangi Mkuu wa wachagga akishirikiana kwa ukaribu na baraza la Halmashauri kuu ya wachagga.
Walisukuma mbele agenda nyingi za kimaendeleo kuanzia kiuchumi, kijamii na hata kutunza na kupigania utamaduni asili wa wachagga. Walijitahidi katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya barabara, mashule, vituo vya afya, tafiti mbalimbali za kisayansi juu ya kilimo, vyuo vya kisasa, miundombinu ya maji, umeme pamoja na kuwekeza kwenye biashara k**a za hoteli kwa ajili ya utalii wa mlima Kilimanjaro uliokuwa unaendelea kukua kwa kasi. Haya yalikuwa ni maendeleo makubwa kwa kipindi hicho kabla ya uhuru wa Tanganyika ambayo kamwe hayawezi kusahaulika wala kubezwa.
Chama cha kisiasa cha CDP kilichoongozwa na Eliufoo Solomon kilikuwa na sera zilizoweza kurubuni watu kwa maneno na ahadi kedekede zilizoweza kuhadaa wachagga kuunga mkono sera hizo kwa kupiga kura ya maoni dhidi ya sera za chama cha wachagga wahafidhina (KCCU) na kufanikiwa kushinda.
Hata hivyo Eliufoo Solomon na vijana wengine hawakuwa na sera zinazoeleweka kwa usahihi, na wala hawakuwa na maono wala mpango wa kufanyia kazi sera hizo baada ya kushinda kura husika ya maoni.
Licha ya kuzungumzia demokrasia ambayo tayari ilikuwepo kwa kiwango kikubwa Kilimanjaro kuliko hata iliyopo Tanzania ya leo, Eliufoo pamoja na watu wote wa chama cha TANU waliokuwa nyuma yake hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na uzoefu wa kiuongozi katika nchi hapo kabla k**a alivyokuwa Mangi Mkuu wa wachagga, na wakafanya kazi katika hiyo demokrasia waliyokuwa wanainadi tofauti na chama cha (KCCU) waliokuwa wananadi mambo yaliyokuwa yanaendelea Kilimanjaro kwa wakati husika.
Pengine kukosa uzoefu kabisa ukichanganya na nguvu iliyokuwa nyuma yake vilichangia yeye Eliufoo Solomon kushindwa kufanya chochote baada ya kupewa ofisi ya urais wa wachagga na badala yake aliitelekeza ofisi aliyopewa na wachagga na kukimbilia Dar es Salaam ili kujumuishwa kwenye baraza la mawaziri la kwanza chini ya serikali ya awamu ya kwanza ya Tanganyika baada ya waingereza.
Kitendo cha Eliufoo Solomon kuondoka Kilimanjaro na kutelekeza ofisi aliyochaguliwa kilionyesha kwamba hakuwa na nia yoyote ya kukuza ustawi wa Kilimanjaro k**a alivyojinadi badala yake alikuwa ametumwa tu na hivyo kuhesabiwa k**a msaliti na zaidi mhaini.
Shutuma hizi za Eliufoo Solomon kuonekana k**a msaliti zilijidhihirisha wazi mwaka 1965 aliporudi Kilimanjaro kugombea ubunge wa jimbo la Hai kwa tiketi ya chama cha TANU ambapo kwenye kampeni zake huko Machame wapiga kura walimzomea na kumwita majina mbalimbali k**a vile msaliti, mhaini, mtu asiyeaminika, mtu asiyefaa wala wa kutegemea, ambapo yeye mwenyewe binafsi alishindwa kuwashawishi watu kwa hoja kuwa yeye sio msaliti kwa kitendo alichofanya cha kuhadaa wachagga na kuhujumu maendeleo ya Kilimanjaro.
Hali hii ilimtokea Eliufoo Solomon kwa sababu wachagga walitegemea kwamba baada ya chama cha CDP kupigiwa kura na kupewa ridhaa ya kukalia ofisi kubwa zaidi ya wachagga Kilimanjaro angekuja na mipango mikakati ya namna Kilimanjaro itasonga mbele kutokea pale ilipofika baada ya Mangi Mkuu kuondoka madarakani.
Hili ni jambo ambalo watu wengi walitarajia litatokea hata ikiwa Tanganyika itapata uhuru na Kilimanjaro ikiwa ndani yake kwani mfumo huo ungeweza kufanya kazi k**a vile ulivyokuwa unafanya kazi wakati serikali ya waingereza ikiwa katika madaraka na pengine mambo walitegemea yangekuwa mazuri zaidi kwao baada ya uhuru kwani serikali mpya ya Tanganyika/Tanzania ilipaswa kuja na mipango bora zaidi kwa maendeleo ya wazawa Kilimanjaro kuliko kipindi cha wakoloni k**a jinsi walivyokuwa wanaahidi kwa wananchi kabla ya uhuru wa Tanganyika.
Hata hivyo mambo yalienda kinyume chake k**a ilivyotokea baada ya uhuru wa Tanganyika ambapo hali ya kiuchumi Kilimanjaro ilidorora na kuendelea kuwa mbaya siku hadi siku mara baada ya uhuru wa Tanganyika.
Wachagga katika miaka ya 1960’s hawakuweza kumuelewa Eliufoo Solomon aliyejiunga na serikali ya Tanganyika/Tanzania ambayo ilipelekea maendeleo ya Kilimanjaro kudumaa tofauti na yalivyokuwa kabla ya uhuru wa Tanganyika kinyume na walichokuwa wanaahidi kabla ya uhuru wa Tanganyika.
K**a hiyo haitoshi serikali mpya ya Tanganyika/Tanzania pia ilifuta vyama vyote vya kisiasa ndani ya Tanganyika/Tanzania mara baada ya uhuru wa Tanganyika na kubakiza chama cha TANU peke yake ambacho kilikuwa kimekabidhiwa madaraka na waingereza na hivyo hata ile demokrasia ambayo Eliufoo Solomon na washirika wake waliitumia k**a propaganda ya kuingia na kuharibu mfumo wa uchumi Kilimanjaro ilidorora sana hata ndani ya Tanganyika yenyewe na hivyo ule uhuru wa kisiasa uliondoka sio tu Kilimanjaro bali hata ndani ya Tanganyika yenyewe chini ya Rais Nyerere mambo yaliharibika sana.
Eliufoo Solomon mwenyewe alikuja kufariki miaka kumi baadaye mwaka 1971 akiiacha nchi ya Tanganyika na hususan Kilimanjaro ikiwa katika sintofahamu kubwa kiuchumi na hata kisiasa kukiwa hakuna demokrasia aliyoitumia k**a propaganda sio tu ndani ya Kilimanjaro bali hata Tanzania kwa ujumla na hata maendeleo ya kiuchumi kudorora sana.
Ahsanteni.
CREDIT@ URITHI WETU WACHAGGA FACEBOOK PAGE
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Himo
Moshi