Malenga Tazz
SHARI:NIKULIPE NINI?
MTUNZI:MALENGA PANGA LA MOTO
HAFSAH:Ewe mliwazi wangu,Nina jambo nikwambie,
HAFSAH:Uhimayani mwangu,kwani nikufichie!?
PANGA:Naam kipenzi changu,la moyo nifungulie.
P:Wewe kwangu ja zawadi,kukutunza ni wajib
P:Tusije ifanya ndoano,kwa kujaza ATI ATI,
H:Sijakuona mfano,we wakwangu tofauti.
P:Sinipambe kwa kangano,kaja nipiga kibuti
H:Huba lako so mfano,sijui nikulipeni!?
H: Nyongo lonithaminisha,Leo mke wa thamani.
P:Nyonda menifurahisha,ndimi Yako asmini
H:Likofishwa menivusha,najihisi nipeponi
P:Wewe kwangu ja zawadi, kukutunza ni wajib.
P: Mapenzi linikatili,kanipotosha Imani,
P:We kwako menikabili,kwa busara na hisani
H:Labda niseme kwa Siri,siniibie jirani
H:Wewe fundi so mfano,sijui nikulipeni!?
H:Umekuwa k**a tiba, hosipitali ya Nini!?
H:Nikiona nashiba,chakula Cha KAZI Gani!?
P:Kukuweka wa akiba !na wakwanza awe nani!?
P:Wewe kwangu ja zawadi, Kukutunza ni wajib.
P: Na wewe Najivunia,ubavu wangu wa kweli,
P: Heshima menitunzia ,lotangulia tapeli,
H:Bora ishirini so mia,ya simango na kejeli.
H:Wewe fundi so mfano,kwako komo mefikia.
H: Na ndoa nimeridhia, niwe wako wa milele,
H: Nyongo ushanikalia,zinawiri mbelewele
P: Ahsante maridhia,lobaki vigelegele,
P:Wewe kwangu ja zawadi, kukutunza ni wajib.
P:Wataarifu mandugu, rafiki na majirani,
P:Tumeuunga udugu,wasubiri mkekani,
H:Na mafisi Wala njugu, Panga yupo himayani
P:Menitunuku zawadi,H: YARABI nikulipeni!?
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Website
Address
Moshi