Pastor Elisha M Mapande

Pastor Elisha M Mapande

Share

26/11/2025

‎MUNGU ANA MPANGO NA WEWE.

Katika hali ya kawaida una weza kuona k**a Mungu ame kuacha na kuku telekeza.Hata k**a hauja tenda dhambi au kuanguka kiroho.
‎Mungu ana jivunia juu yako hata jinsi unavyo shinda majaribu na kupambania Imani yako.

‎Ayubu 4:7
‎[7]Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia?
‎Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi?

‎Wakati mwingine unapo pita kwenye changamoto fulani.Adui ana jitahidi kukufanya uone ubaya zaidi ya matendo makuu ya Mungu aliyo wahi kukutendea usikate tamaa.

‎Changamoto na mapito k**a haya ambayo tuna yaona kwenye kitabu cha ayubu ni Mungu anajivunia mtoto wake alivyo mwaminifu kwake hata kwenye tabu.

‎Yakobo 1:12
‎[12]Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

‎Nipo hapa kuku tangazia kwamba Mungu anakupenda na ile Kazi njema aliyo anzisha kwenye maisha yako ata itimiza.

‎Hivyo ukipita kwenye hali ya kujaribiwa uone ng'ambo ya jaribu lako ambayo ni taji ya uzima.Usione jaribu k**a teso na maumivu bali ngazi ya kupandishwa kwenda hatua nyingine.

‎Amini kwenye mchato wa Mungu kuifundisha mikono yako vita k**a Daudi semavyo (Zaburi 18:34
‎[34]Ananifundisha mikono yangu vita,
‎Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.)

Hakika utashinda kwa msaada wa Bwana na kuingia viwango vingine.

‎Mwisho haya yote ni kwa wale walio mpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao.Mpokee Yesu wewe k**a bado ili uwe mrithi wa ahadi hizi amen amen.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Moshi