SokaPlace
🎙️ Afisa Habari wa Tanzania Prisons, Alexander Ngelela, amesema uongozi wa klabu hiyo umeamua kuwaongezea hamasa wachezaji kwa kuwaahidi bonasi nono katika michezo mitano iliyobaki ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ngelela amesema bonasi hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha timu inapambana kwa nguvu zote katika mechi zilizosalia ili kujinusuru na hatari ya kushuka daraja. Kwa sasa Tanzania Prisons ipo kwenye vita ya kusaka pointi muhimu katika hatua za mwisho za msimu.
"Uongozi umeweka mazingira mazuri kwa wachezaji na umeahidi bonasi nzuri ili kuongeza morali na ari ya kupambana katika michezo iliyobaki. Kila mmoja anatambua umuhimu wa mechi hizi kwa mustakabali wa klabu," amesema Ngelela.
Tanzania Prisons inakabiliwa na michezo muhimu ya mwisho ya ligi ambayo itaamua hatma yao ya kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Sponsored by
04/06/2026
🔵 RASMI: Azam FC Yaongeza Mkataba wa Florent Ibenge hadi 2028
Baada ya kuzagaa kwa tetesi zinazomuhusisha kocha Florent Ibenge na uwezekano wa kujiunga na Timu ya Taifa ya Mali, Azam FC imeweka wazi msimamo wake kwa kumuongezea mkataba kocha huyo hadi mwaka 2028.
Uamuzi huo unaonesha imani kubwa ambayo klabu hiyo inaendelea kuwa nayo kwa kocha huyo raia wa DR Congo, huku ikisisitiza kuwa ni sehemu muhimu ya mradi wa muda mrefu wa Azam FC kuelekea mafanikio makubwa zaidi.
Ibenge ataendelea kuiongoza Azam FC katika safari ya kutimiza malengo yake ya ndani na kimataifa. 🔥💙
Sponsored by
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mbeya