Mbeya Press Club

Mbeya Press Club

Share

Photos from Mbeya Press Club's post 12/10/2025

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UYOLE AFANYA KAMPENI MGUU KWA MGUU

Mgombea ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Ipyana Samson Njiku, ameendelea na kampeni zake za mguu kwa mguu kwa wananchi wa Jimbo la Uyole, ambapo leo ametembelea maeneo ya Kata ya Itezi na Igawilo akiwahamasisha wananchi kujiandaa kwa mabadiliko chanya kupitia uongozi makini na wenye dira ya maendeleo.

Akizungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali , Njiku amesema kuwa endapo atapata ridhaa ya wananchi wa Uyole, ataweka kipaumbele katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo:

Ujenzi wa Soko la Kisasa na Kimataifa litakalowezesha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi kwa urahisi, kuongeza ajira na kipato cha wananchi.

Soma zaidi kupitia blog ya Mbeya Press Club.

31/08/2025

Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC akizungumza kuhusu malengo ya msingi ya Mdahalo wa Kitaifa kuhusu ulinzi na usalama kwa Waandishi wa Habari.

Hata hivyo amesema kuwa msingi wa Midahalo uliyofanywa hapo hawali na jeshi la polisi ndio ambayo imetufikisha hapa leo hata tukaweza kukutana tena katika Ngazi ya Kitaifa.

Mdahalo huu umefanyika leo Agosti 29 katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la UNESCO jijini Dar es Salaam.tanzania

31/08/2025

Mkuu wa Polisi Tanzania, IGP Camilius Wambura amewahakikishia ulinzi na usalama Waandishi wa Habari katika kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya uchaguzi, huku akiahidi Jeshi la Polisi litaendelea kufanya midahalo na waandishi wa Habari katika masuala yanayohusu ulinzi na usalama wao.

IGP Wambura ameeleza hayo wakati akifungua Mdahalo wa kitaifa kuhusu Ulinzi na Usalama wa waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mdahalo huo wa kitaifa ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya UTPC, THRDC na UNESCO ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Waandishi wa Habari ili Jamii iweze kupata Taarifa, Unaotekelezwa na Umoja wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la International Media Support(IMS) kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Uswizi na Umoja wa Ulaya (EU).

Mdahalo huo umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 100 kutoka katika Taasisi za Kihabari, Vyombo vya Habari, Waandishi wa Habari, Wahariri, Wawakilishi kutoka taasisi za Serikali, Jeshi la Polisi, Wawakilishi kutoka balozi mbalimbali nchini na wadau wa maendeleo.


tanzania

26/08/2025

WALIMU JIMBO LA UYOLE KUPEWA ‘IPHONE MACHO MATATU’

Mgombea Ubunge Jimbo la Uyole Jijini Mbeya kupitia tiketi ya chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Ipyana Njiku jana Agosti 25, 2025 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya wananchi wa jimbo hilo katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Uyole iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Akizungungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi hizo Njiku ametaja baadhi ya vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kuboresha sekta ya elimu nchini kwa kuhakikisha anagawa kompyuta mpakato (Laptop) mashuleni pia kila kila mwalimu wa shule ya msingi na sekondari Jimboni humo atapata simu janja aina ya iPhone macho matatu.

Want your business to be the top-listed Media Company in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Sokoine
Mbeya