Alochick - alome chickens

Alochick - alome chickens

Share

07/01/2020

Je umeshaaanzisha mradi wako wa Kuku, Lakini hauna usaidizi wa Daktari anayekutembelea angalau Mara 2 kwa Mwezi,

Ili kukupatia Ushauri wa Mara kwa Mara kuhusu Namna ya Kuboresha mradi wako?

Ili uepukane na hasara mbalimbali zitokanazo na Magonjwa ya Kuku,

Ulishaji mbaya,

Matumizi mabaya ya Dawa au Chanjo.

Ili uweze Kuongeza KIPATO CHAKO!

Leo KPTL tumekuletea Huduma Bora ya Usimamizi wa mashamba (Farm Management)

Ambapo Daktari wetu atakutembelea mara 2 kwa Mwezi na kukupatia usaidizi wa mara kwa mara

Ili uboreshe mradi wako na uweze KUONGEZA KIPATO CHAKO.

K**a unahitaji huduma hii ya Usimamizi wa Mashamba (Farm Management)

Wasiliana nasi kupitia
0752 672 181

Karibu Ofisini kwetu

Dar, Kijitonyama Bamaga.

27/12/2019

MAZOEA YANAYOWAGHARIMU WAFUGAJI WA KUKU

Kuna baadhi ya wafugaji huwa wanafuga kwa kutegemea uzoefu walionao katika ufugaji bila ya kujali kuwa kuna mabadiliko kila siku katika sekta ya mifugo, wengi wao huwa wanatatua kesi mbalimbali zinazotokea katika ufugaji kwa kutumia uzoefu hali ambayo inawasababishia kupata hasara kubwa isiyo ya lazima. Yafuatayo ni baadhi ya mazoea yanayowagharimu wafugaji:-

1. KUINGIZA VIFARANGA BILA MAANDALIZI SAHIHI

Wengi wa wafugaji huwa wanaingiza vifaranga pasipo kufuata utaratibu wa kitaalam katika kuandaa banda pamoja na maandalizi ya kupokea vifaranga. Na k**a atabahatika kufanya usafi basi atafanya juujuu tu hali ambayo inasababisha banda kuhifadhi vimelea vingi vya magonjwa na kupelekea kuku kuugua na kufa kuanzia wanaingia hadi kufikia kuuzwa, na hatimaye mfugaji hupata hasara kwani hutumia pesa nyingi kwenye madawa kwa kutibu na pesa nyingi kwenye chakula kwa kuchelewa kukua kutokana na kuumwa.

2. KULISHA BILA KUFUATA MAELEKEZO SAHIHI
Kila aina ya kuku wanautaratibu wa ulishwaji chakula, utaratibu ambao ukikiukwa huwezi kupata matokeo mazuri ya mifugo yako, ila wafugaji wengi huwa wanalisha kwa utaratibu usio sahihi ambao wao wanadhani kwamba ndio wataongeza
uzalishaji wa mayai au watakuwa haraka kwa upande wa kuku wa nyama, na kuna wengine wanadiriki kutumia chakula aina moja mwanzo mwisho, yaan anaweza kutumia chakula cha
vifaranga wa nyama (SUPER STARTER) kuanzia mwanzo hadi anauza kuku bila kufaham kwamba kila aina ya chakula ina kazi yake katika kila hatua ya umri. Lakini pia bila kujali kwamba analisha kwa gharama kubwa hali ambayo itampunguzia faida.

3. KUTIBU KWA DAWA AMBAYO SI CHAGUO KWA UGONJWA HUSIKA
K**a inavyofahamika kuwa wafugaji wa kuku wengi wamebarikiwa kwa kufaham majina mengi ya dawa za kuku, na kwa kutumia uzoefu walionao huwa wanatibu kuku wao magonjwa mbalimbali bila kupata maelekezo kutoka kwa Dokta au Mtaalam wa mifugo. Kwa kufanya hivyo hutumia dawa nyingi tofautitofauti kwa kutibu ugonjwa mmoja bila mafanikio na kupelekea ugonjwa kuwa sugu na idadi ya vifo kuongezeka siku hadi siku.

USHAURI:
Sio kila mfugaji mzoefu anaweza kuwa Daktari, ila kila Daktari anaweza kuwa mzoefu.

UKIITAJI KITABU CHA UFUGAJI WA KUKU WASILIANA NASI 0746090774

HARDCOPY SH 10000
SOFTCOPY SH 5000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP

BY
ALOME BROWN

22/12/2019

[ KITINI BURE ] Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili (Kuku wa Kienyeji)

Bonyeza hapa Kukipata
>>http://www.tfcg.org/wp-content/uploads/2018/08/AVA-Improved-poultry-farming-training-materials-2017.pdf

Chanzo cha kitini hichi ni Tanzania Forest Conservation Group

Jumapili njema kwenu..

Want your restaurant to be the top-listed Restaurant in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Tunduma
Mbeya

Opening Hours

Monday 08:00 - 18:00
Tuesday 08:00 - 18:00
Wednesday 08:00 - 18:00
Thursday 08:00 - 18:00
Friday 08:00 - 18:00