Knews24

Knews24

Share

10/05/2025

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema hivi karibuni wakati likiendelea na uchunguzi wa tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mpaluka Said Nyagali maarufu Mdude na watu wasiofahamika na kisha kutoweka naye kusikojulikana, wamejitokeza baadhi ya watu na viongozi wa CHADEMA na kutoa matamko mbalimbali ikiwemo kutaja baadhi ya majina ya Askari wakiwatuhumu kuhusika na tukio hilo bila kuwasilisha ushahidi wowote.

Kupitia taarifa ya leo Mei 10, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga Jeshi hilo limetoa onyo kali kwa mtu au kikundi chochote cha watu wenye nia ovu kutojaribu wala kuthubutu kujihusisha na uhalifu wa aina yoyote ikiwemo kudhuru Askari ama familia za Askari.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeeleza kuwa kabla ya mtu au kikundi cha watu kufikiria kufanya hivyo, wajionye sana na wasifikiri kufanya kitendo hicho ni rahisi kwao huku likisisitiza kuwa halitasita kumchukulia hatua za kisheria na kumshughulikia mtu au kikundi chochote cha watu watakaojaribu kufanya uhalifu kutokana na matamko au kauli hizo zinazotolewa.

08/05/2025

Kadinali Robert Prevost ametangazwa kuwa Papa mpya.
Na kuanzia leo anajulikana k**a Papa Leo XIV.
-
Robert Kardinali Prevost anatokea Chicago nchini Marekani, na hadi kuchaguliwa kwake alikuwa akihudumu k**a mkuu wa Dicastery wa kanisa kwa Maaskofu
-
-

04/05/2025

Jeshi la Polisi nchini limeanzisha uchunguzi rasmi kufuatia tuhuma nzito zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya askari wake wawili wanaodaiwa kuhusika na mazingira ya kutoweka kwa mwanaharakati Mdude Nyagali.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, mwananchi mmoja ambaye jina lake bado linafuatiliwa kwa uchunguzi, alidai kuwa askari hao walimfuata na kumtaka kushiriki kwenye shughuli za kijajusi kwa ahadi ya malipo ya kifedha. Tuhuma hizo zimezua mjadala mpana miongoni mwa wananchi na wanaharakati wa haki za binadamu, wakitaka ukweli wa suala hilo kuwekwa wazi.

Taarifa kutoka Makao Makuu ya Polisi zimeeleza kuwa, tayari kikosi kazi maalum kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kimepelekwa katika mkoa wa Mbeya, ambako sakata hilo linadaiwa kutokea, ili kufanya uchunguzi wa kina.

"Wakati uchunguzi unaendelea, tunatoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa muhimu kuhusu tukio hili kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kusaidia kufanikisha upatikanaji wa ukweli," imesema sehemu ya taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo.

Mdude Nyagali, anayefahamika kwa sauti yake ya ukosoaji dhidi ya viongozi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii, amewahi kuripotiwa kushikiliwa na vyombo vya dola katika nyakati tofauti. Tukio hili jipya limezusha maswali kuhusu usalama wa wanaharakati nchini na nafasi ya vyombo vya dola katika kulinda haki za kikatiba.

Mpaka sasa, bado haijafahamika rasmi mahali alipo Mdude wala hali yake, jambo linaloendelea kuzua hofu na wasiwasi kwa familia yake na jamii ya watetezi wa haki za binadamu.
tanzania

Want your business to be the top-listed Media Company in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address


Mbeya
53121