TCCIA Mbeya
25/03/2024
CHEMBA YA WABIASHARA, WENYE VIWANDA NA WAKULIMA MKOA WA MBEYA (TCCIA)🌍. Imepokea
Ugeni kutoka kampuni ya Kampuni ya ORBIT SECURITIES COMPANY LTD yenye makao jijini Dar es Salaam wanajishughulisha na ushauri wa uwekezaji, kuuza na kununua dhamana za Serikali, Resources mobilisation, usimamizi wa mitaji, uuzaji wa hisa na uanzishwaji wa makampuni ya umma Pichani kutoka kushoto, Gideon Ligate Mkurugenzi ORBIT SECURITIES, Eric Sichinga Mwenyekiti TCCIA MBEYA, Justin Amos afisa mauzo wateja wakubwa ORBIT SECURITIES na Eng. Maneno Sanga Makamu Mwenyekiti viwanda TCCIA MBEYA.
18/03/2024
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Mbeya katika maadhimosho ya wiki ya kumlinda mlaji Duniani wamepata mafunzo namna ya kumlinda mlaji katika Uchumi wa soko, kujua,haki za mlaji na wajibu wa mtumiaji. Pia ilielezwa wafanyabiashara wawe na utayali wa kutumia akili mnemba kuhakikisha wanaendana na akili mnemba kuongeza maarifa na jitihada namna ya kumlinda mlaji katika Uchumi wa soko.
18/03/2024
TCCIA kwa kushirikiana na Rikolto pamoja na 360 connect kupitia mradi wa USIMAMIZI JUMUISHI WA MAZINGIRA KWA USTAHIMILIVU WA HALI YA HEWA unaotekelezwa katika halmashauri za Rungwe Busokelo na Kyela tulifanikiwa kufanya mkutano wa wadau wa Mazingira waliopo katika mnyororo wa thamani wa mazao ya mpunga, kakao , mboga na matunda uliofanyika katika ukumbi wa KBC Kyela. Mkutano ulilenga kukujadiliana pamoja matokeo ya utafiti kuhusu hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika halmashauri hizo. Majadiliano ya kina yalifanyika na wadau kwa pamoja walikubaliana kuwa na mkakati wa pamoja katika kukabiliana na mabadiliko haya. Kila Halmashauri iliweza kuweka vipaumbele kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kulindwa. #360-connect
31/01/2024
Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima mkoa wa Mbeya Tccia Mbeya ili fanikiwa kuandaa chakula cha jioni (Dinner Gala) na wafanyabiashara mkoa wa katika ukumbi wa Eden Highland hotel.
Kwenye tukio hilo meneja wa Tanzania investment Center mkoa wa Mbeya (TIC) alipata nafasi ya kuwaalika wafanyabiashara wa mkoa kuwekeza katika mkoa wa Mbeya.
Pamoja na hayo mwenyekiti wa Tccia Mbeya Ndg. Erick Sichinga alipata fursa ya kuwaalika wafanyabiashara katika maonesho ya Mbeya city expo yatakayo tarajiwa kufanyika mwezi wa Mei mwaka 2024.
13/09/2023
Leo tarehe 13/09/2023 Tccia Mbeya Tumepokea mwanachama mpya ( TUMAINI HONEY)
Ambaye anauza asali lishe pia na asali ya kawaida anapatikana mbeya karibuni sana.
08/09/2023
Today 08/09/2023 the Founder/CEO of Agromovil Mr. Andrew Mack (left) and The Country Manager Mr. Mdete (right) met with TCCIA Mbeya in a pleasant setting to discuss strengthening market access through Agromovil.
07/09/2023
Katibu wa TCCIA Mbeya Ms christina Joseph akiwa kwenye ziara ya kuwatembelea wanachama wa Tccia Mbeya. Lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto zinazo wapata wanachama.
07/09/2023
Mwenyekiti wa TCCIA Mbeya na kaimuMakamu wa raisi Biashara akiwa na wanachama wapya 21 wa Tawi jipya la Chalisuka-Madibira katika wilaya ya Mbarali mara baada ya kulifungua na kusimamia uchaguzi Leo tarehe 06/09/2023
01/09/2023
Rikolto kwa kushirikiana na TCCIA pamoja na 360 Connect wameanza utekelezaji wa mradi wa mazingira.
Mkutano wa kwanza wa wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na mazao ya kokoa, mpunga,mboga na matunda ulifanyika siku ya jana kujadiliana kwa pamoja masualabalimbali yanayochangia kuboresha mazingira na ustahimilivu wa hali ya hewa. Jumla ya wadau 65 walishiriki katika mkutano huu na kitoka michango yenye tija ili kiendelea kuokoa uharibifu waazingira katika wilaya za Kyela, Busokelo na Rungwe
Mradi wa usimamizi jumuishi wa mazingira kwa ustahimilivu wa halo ya hewa
30/08/2023
Mwanachama wa TCCIA na Mfanyabiashara Mkubwa Mkoa wa Mbeya Given Tughimbage akikabidhiwa bidhaa baada kikao chenye tija cha kuwa msambazaji mkuu wa bidhaa za kampuni ya Sungold Food Processing Ltd.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
P. O. Box 882 Mbeya
Mbeya
53107