Isaiah The JUDGE
17/12/2025
2026, UTAKUWA JUU TU, wala huwi chini;
(Torati 28:13)
Kwanini Mungu anainua watu ni swali muhimu zaidi KATIKA ulimwengu wa maendeleo na hatua mpya.
Maandiko yanaonesha Mungu Yuko juu, na wazo lake Kwa mtu aliyemuumba Kwa sura na mfano wake ni kumweka juu.
Tangu mwanzo mtu aliumbwa awe mtawala, na hii inamaanisha kuwa juu ya vitu vyote vya uumbaji wa Mungu duniani. Yaani Mtu ni bwana wa vyote na vyote ni watumishi wa mtu.
Kumbukumbu la Torati 28:13
___"BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe UTAKUWA JUU TU, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;"
Fedha, mali, ndege, wanyama, mimea, madini na vitu vingine vyote viliumbwa vimtumikie mtu kwaajili ya kusudi alilobeba. Vinapaswa kuhangaika kwaajili ya kurahisisha maisha ya mtu na si mtu kuvihangaikia k**a njia ya kupata unafuu wa maisha. Vinapaswa kutii bila shuruti! Hayo ndiyo mapenzi kamili ya Mungu.
Mathayo 6:31-34
_____"Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake."
(Kusumbukia ufalme wa Mungu, ni kuifanya kesho Yako ijipangilie).
Ni vyema ufahamu kuwa viumbe vyoote, vimeumbwa kutii sauti na mamlaka ya Mungu tu. hivyo Ili vikutii wewe mwanadamu lazima uwe na sauti pamoja na Mamlaka uliyopewa na Mungu.
Mungu asipokupa mamlaka yake, hutaweza kutawala viumbe vyake! Na kupewa mamlaka ya Mungu ndiko kuinuliwa kwenyewe ninakozungumzia.
Luka 19:15-17
____"Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi."
Hapo tunaona, MTU huyu alipewa mamlaka ya kutawala miji kumi. Hivyo hii miji ulimtii SI Kwa Sababu ni mzuri, ana vitu au chochote kile, Bali Kwa Sababu tayari ameshapewa mamlaka na Bwana wake juu ya hiyo miji kumi.
Ndiyo maana unaweza kushangaa kwanini baadhi ya watu wana vitu, uwezo, na vigezo mbalimbali lakini hawainuki kwenye maisha haya? Uwepo wa vitu au watu bila mamlaka ya Mungu inayoinua ni sawa na kujaribu kuendeshwa gari isiyo na injini.
Mungu ni bwana (mtawala) wa MTU, na MTU ndiye mtawala wa Vitu vyote juu ya nchi. Maana yake KAZI yetu ni kumtumikia Mungu, na KAZI ya vitu k**a pesa na mali ni kututumikia sisi.
Maana yake Mungu akikuinua, amekuinua kwaajili ya kutimiza ajenda zake Wala si kwaajili Yako. Ndiyo maana watu wengi wasiofahamu, hukengeuka pale wanapopata mamlaka na kuanza kuwa jeuri k**a Nebkadreza wasijue kuwa Mungu ndiye huinua watu.
Danieli 4:24-27
_____"tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani k**a ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala. Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha."
Muda wote, watu wa Mungu wakiwa chini Yako, ni ushahidi kuwa hapo ulipo umewekwa na Mungu, na WALINZI watakatifu wa Mungu wanakuangalia Kwa Umakini na kukuhukumu.
Shalom!
[Mchungaji Isaiah Imani]
13/12/2025
MAPENZI YA MUNGU KWA MWOMBAJI.
Ni habari njema, kusikia kwamba ni mapenzi ya Mungu tupate. Yaani kwaa lugha nyingine Mungu yuko upande wako k**a mwombaji ili kuhakikisha unapata haki yako unapoomba.
Uadui wa shetani hauna mafanikio kinyume na maombi yako, kwa sababu Mungu anataka upate. Ufahamu huu ni muhimu sana, dumu kujiambia "Mungu anataka nipate", Mungu ananiunga mkono.
Watu wengi pamoja na kuomba kwao kwingi, wengi hawapokei kwa kuwa tu hawajui ni haki zao na ya kwamba Mungu anataka wapate. Na ndiyo sababu utakuta mambo mengi ambayo yamewashinda wanaishia kusema "ni mapenzi ya Mungu".
Sikatai ukweli kuhusu mapenzi ya Mungu ila najua pia hata watumiaji wengi wa kauli andiko hili la hawajui kwa undani wanamaanisha nini kusema ni mapenzi ya Mungu..
Hivi, mapenzi ya Mungu ni yapi?
Mapenzi ya Mungu ni Ni mambo yote ambayo Mungu anataka kwaajili yetu.
Ni kila jambo ambalo Mungu anafurahia likifanyika kwako.
Ni Kila jambo lenye hadhi ya KUFANYIKA mbinguni aliko Mungu. Mathayo 6:10
"Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani k**a huko mbinguni."
Ni jambo ambalo Mungu amethibitisha kwa neno lake kuwa linatufaa.
Ni jambo lolote ambalo Mungu amelinena au kuliahidi kwaajili yetu wala si kinyume chake.
Unapoomba usisahau kuwa "Mungu anataka upate!
Shalom
[Mchungaji Isaiah Imani]
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Mbalizi
Mbeya