Glorious Rehobothi
Hello follower's habari
KWA NINI UNAPATA MAUMIVU CHINI YA KITOVU?
👉Kawaida husababishwa na gesi na choo kigumu
Wanawake wengi mnapata maumivu ya mara kwa mara chini ya tumbo kwa sababu
👉Matatizo ya Hedhi
👉Maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI)
👉Ugonjwa wa Pelvic Inflamatory (PID) ni maambukizi ambayo huathiri uterasi na mirija ya uzazi. Mara nyingi huhusishwa na magonjwa ya zinaa, lakini pia inaweza kuendeleza bila maambukizi ya zinaa.
Dalili zinaweza kujumuisha maumivu wakati au baada ya tendo la ndoa, kutokwa na damu kusiko kwa kawaida ukeni, na maumivu chini ya tumbo.
Unapopata Hali hii fanya vipimo vya uhakika na kupata tiba.
15/02/2023
*Je, Nini Chanzo Cha Mzunguko Mfupi Wa Hedhi?*
K**a mzunguko wako wa hedhi ghafla ukiwa mfupi, inaweza kuwa kwa sababu ya mambo haya yafuatayo;
👉. Mayai kushindwa kupevuka
👉. Kipindi cha kukoma hedhi kuanza
👉. Kuvunja ungo
👉. Uvimbe wa fibroid kwenye kizazi
👉. Vivimbe maji kwenye vifuko kwenye mayai
👉. Msongo wa mawazo
👉. Kuwa na uzito kidogo sana au uzito kuwa mkubwa
👉. Matumizi ya uzazi wa mpango
👉. Maradhi
👉. Tezi za thyroid kufanya kazi kupita kiasi
👉. Tezi ya thyroid kufanya kazi kwa kiwango cha chini sana
15/02/2023
Mazoezi Mepesi Ya Kusaidia Kizazi Kisiinamie au Kulalia Upande.
Kuinama kwa kizazi kwa majina mengine ya kitaalamu tunaweza kuita tilted uterus, retroflexed uterus, retroveted uterus au backward uterus ni namna mfuko wa mimba unapovutika kuelekea nyuma zaidi ya mlango wa kizazi badala ya kuvutika kuelekea mbele.
Uhakika zaidi wa kujua k**a kizazi chako kipo sawa ni kwa kufanya kipimo hospitalini japo unaweza kujigundua kwa dalili mfano k**a :
• Kupata changamoto kwenye kuweka pedi yako ili kuvyonza damu ya hedhi.
• Maumivu ukeni na nyuma kwenye mgongo wa chini wakati wa tendo la ndoa
• Maumivu makali kipindi cha hedhi kutoka
• Kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo (U.T.I) mara kwa mara
• Kushindwa kujizuia mkojo na Kuongezeka kwa eneo la chini ya tumbo.
Kumbuka siyo lazima kupata dalili zote kwa pamoja, k**a unapata dalili zisizo za kawaida ni vizuri kufika hospitali ili kufanya vipimo ukaanza tiba mapema.
â—Ź Nini Kinasababisha Kizazi kuinama
Mfuko wa mimba ambao ndio kizazi tunachozungumzia ni sehemu tupu ambayo inajiweka katika eneo la chini ya nyonga za mwanamke. Kazi yake ni kuhifadhi kichanga baada ya urutubishaji kufanyika.
Kizazi cha mwanamke kinaweza kuinama kutokana na sababu mbalimbali k**a
▪︎Kulegea kwa misuli ya nyonga:
Mwanamke akishafikia kukoma hedhi au baada ya kujifungua, misuli inayosapoti tumbo la uzazi hulegea na hivo kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma
▪︎Kupanuka kwa kizazi kutokana na ujauzito, ama vimbe mbalimbali k**a fibroids au vimbe ambazo si saratani (tumor) zinaweza kusababisha kuinama kwa kizazi.
▪︎Makovu ama msuguano kwenye nyonga
Mfuko wa mimba ama kizazi kinaweza kupata makovu kutokana na hali mbalimbali mfano , maambukizi k**a P.I.D, uvimbe (endometriosis) ama makovu kutokana na upasuaji uliowahi kufanyiwa kwa kipindi cha nyuma. Makovu haya yanaweza kufanya kizazi kuvutika kuelekea nyuma na kuinama.
Mazoezi Mepesi Ya Kufanya Ili Kuinua Kizazi k**a Kimeinama
Zoezi la kwanza ni KNEE CHEST
Lala kwenye sakafu (unaweza kutanguliza kipande cha nguo). Mikono ikiwa imeshika kichwa, kunja goti mpaka ikaribie kugusana na kifua, fanya k**a picha inaoeleza hapa chini. Tulia katika hali hiyo kwa sekunde 20 mpaka 30 kisha pumzika. Rudia zoezi husika mara 10 mapak 15 kwa kubadilisha miguu
Zoezi la Pili ni KEGEL au Pelvic Contraction
Mazoezi haya yanalenga kuimarisha misuli ya nyonga.
Jinsi ya kufanya zoezi hili lala kwenye sakafu huku mikono yako ikiwa imenyooka kuelekea kwenye miguu. Taratibu nyanyuka eneo la katikati na makalio kuelekea juu k**a picha inavyoonesha hapa chini.
Tulia ukiwa juu hivo hivo kwa sekunde 30 kisha pumzika (shusha kiuno chini sekunde kadhaa) rudia zoezi hili mara 10 mpakmwongozo wa milo na mambo muhimu kuzingatia ili upate matokeo mazuri zaidi.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mbeya