Discipleship International Ministry - Dim

Discipleship International Ministry - Dim

Share

30/01/2023

TUNABADILISHWA KUTOKA UTUKUFU HATA UTUKUFU.
Apostle Elia.(c.mkuchu).

20/04/2018

Somo la leo:
Sharoom,sharoom, wanafunzi wa Yesu.Yesu Kristo asifiwe. Leo tutakuwa na somo linalosema:-ILI UISHI MAISHA YA USHINDI UNAHITAJI KUWA MTU WA KUSAMEHE.
Mathayo18:21"Kisha petro akamwendea akamwambia, Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimi nimsamehe?Hata mara saba?22Yesu akamwambia, sikuambii hata mara saba,hata saba mara sabini."
Yesu anajibu swali la petro juu ya kiasi gani naweza kumsamehe mdeni wangu(mkosaji).Yesu anampatia majibu ambayo hakuyatazamia-7*70!!hii inamaanisha kuwa kusamehe uwe ni mfumo rasmi ambao ni endelevu,kwasababu katika maisha tunayoishi tunakutana na vitu mambo na watu wa aina tofauti tofauti wenye mira na desturi tofauti tofauti ambapo kuishi pasipo kukoseana ni vigumu lakini kukiwa na mfumo wa kuchukuliana na kusameheana maisha yatasonga na wengi watapata kujirekebisha na kubadilika.
Kwa wanafunzi wa Yesu ni muhimu tena ni lazima kusamehe(hata k**a mkosaji hajaja kukuomba msamaha)kwaajili ya faida yako mwenyewe kwani pasipo kusamehe Mungu wa mbinguni hawezi kutusamehe wala kupokea na kuyajibu Maombi yatu.mathayo 6:12"utusamehe deni zetu(makosa)kam sisi nasi tunavyowasamehe wadeni wetu(wanaotukosea).mathayo 6:14"kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao,na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi! Kwahyo ili tupate msamaha mbele za Mungu lazima tusamehe waliotukosea.
Usiposamehe huwezi kuishi maisha ya ushindi kwani huwezi kumshinda adui yako. Kumbuka adui yatu mkubwa ni shetani kwahyo hata inapotokea mtu amekukosea siyo yeye aliyepanga kukufanya vibaya bali ni roho ya shetani nyuma yake iliyomsukuma kufanya vile,sasa huwezi kumshinda shetani kwa kumwekea mtu aliyekukosea kisasi lakini kwa njia ya kumsamehe na kumwombea utakutana na adui halisi na kumshinda na hatimaye hata yeye aliyekufanyia ubaya utakuwa umemsaidia kujitambua.Neno katika mathayo5:44"wapendeni adui zenu,waombeeni wanao waudhi ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni....! Umeona,tunaambiwa tuwapende adui zetu na kuwaombea wanaotuudhi kwanini, kwasaba

12/04/2018

NENO LA LEO:-
NGUVU YA UUMBAJI KATIKA KINYWA CHAKO.
Mithar18:20-21."Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake, Atashiba mazao ya midomo yake.Mauti na uzima huwa Katika uweza wa ulimi,na wao waupendao watakula matunda yake."
Nakusalimu mwanafunzi wa Yesu katika jina la Yesu Kristo aliye hai!
Utangulizi wa neo la Mungu unatuambia kuwa maisha ya mtu yatakuwa na utele(kushiba)katika kila eneo Kwa kutegemea namna ya kutumia kinywa chake(maneno) kwasababu ndani ya kinywa cha mtu kuna uwezo wa kuua(mauti)na pia kuna uwezo wa kuuisha(kufanya uhai hata kwa vitu vilivyo kufa) kwahyo namna unavyoweza kutumia kinywa chako ndo namna utakavyopata matunda yake!ndomana akasema wao waupendao watakula matunda yake.
Asilimia kubwa ya namna ilivyo hali ya watu iwe kiroho au kimwili ni matokeo ya namna walivyotumia vinywa vyao! Wewe hujawai kujiuliza kwanini ukiomba kazi katika taasisi nyingi watakufanyia usaili na moja kati ya kipengele watakachokufanyia ni kwenye eneo la kujieleza wakiamini kuwa maneno yako yanabeba utambulisho wa kuwa wewe ni nani na unauwezo gani hata kuwafaa Katika kufanya nao kazi!!
Ni namna gani maneno yana nguvu ya uumbaji?
Mwanzo1:1-3"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi, nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu,na giza lilikuwa juu ya vilindi vya uso wa maji,Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa Maji.Mungu akasema,iwe nuru, ikawa nuru."
Mungu alipoona nchi imekuwa ukiwa tena utupu(formless),giza limetanda,hakuna hali ya kuvutia,ingawa ndani yake(Mungu)alikuwa na picha ya vile anavyotaka dunia iwe.alikuwa na picha ya milima na mabonde,picha ya inchi kavu na bahari, jua na mwezi ...!lkn akaona kuwa ili iwe rahisi kuumbika lazima airuhusu Roho yake itulie juu ya uso wa maji kwani alijua kuwa Roho yake ikitulia juu ya uso wa maji haitakuwa kazi ngumu kuzitoa zile picha zilizopo ndani yake za namna anavyotaka dunia iwe kwani atazitoa nje Kwa kutamka neno tu,kwanini, kwasababu Roho wa Mungu(Roho Mt) tayari yuko juu ya uso wa Maji kwaajili ya kuumba.kumbuka k

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Iringa?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Iringa