Mlewa Electronics

Mlewa Electronics

Share

06/05/2021

IJUE "APP" BORA YA SIMU KWA WANANDOA KULIKO ZOTE.

✍️

INAITWA 👇
"Period Tracker Flo, Pregnancy & Ovulation Calendar"

Hii ni programu ambayo mara nyingi hutumiwa na wanawake au wanaume ambao wapo katika mahusiano ili kupata taarifa sahihi kuhusu mzunguko wa hedhi wa wapenzi wao. Kwa mara ya kwanza utakapo ifungua programu hii utatakiwa kuweka tarehe ya hedhi.

Pia inakupa maelezo kuhusu uwezekano wa kupata ujauzito. Kwa hiyo mbali na taarifa za hedhi, pia ni programu nzuri k**a unahitaji kupata mtoto, itakujulisha siku ambayo kuna *uwezekano mkubwa wa kupata mtoto, na itakwambia jinsia ya mtoto, tabia, na vingine vingi ikitegemea vile ulivoweka taarifa zako.*



NI MABINGWA WA VIFAA VYOTE VYA UMEME

| *WINDOWS ZOTE ZIPO*


N.k

0766199564 / 0622986231
IRINGA TOWN


#(ICT)2021

02/05/2021

WAFAHAMU "VIRUS" 10 WA COMPUTER WALIOTISHA DUNIANI.

(KUNA VIRUS MOJA ILIITWA "I LOVE YOU" ILI KUSHAWISHI WATU KUBOFYA.

✍️

*1.Code Red*

Kirusi cha Code Red kiliibuka mnamo mwaka 2001 na kubainiwa na wafanyakazi wawili wa eEye Digital Security. Kirusi hiki kiliitwa Code Red kwa sababu wafanyakazi hao walikuwa wanakunywa “Code Red Mountain Dew” wakati walipokibaini.

Kirusi hiki kilipoibuka kililenga seva za Microsoft IIS, na kilijizalisha kwa kiasi kikubwa ili kuteka mfumo mzima wa kompyuta. Kirusi hiki kilisambaa kwa kasi hadi kufanikiwa kuathiri seva za ikulu ya Marekani.

Ndani ya muda usiozidi wiki moja, kirusi hiki kilikuwa kimeshazima seva 400,000 na kompyuta milioni moja duniani kote. Inakadiriwa kuwa kirusi hiki kilisababisha hasara ya takriban dola milioni 2.6 za Marekani.

*2. CryptoLocker*

Hiki ni kirusi kilichokuwa kinaathiri kompyuta za Window, kirusi hiki kilificha mafaili ya mtumiaji na kumtaka alipe kikombozi (Ransom) ili apate tena mafaili yake.

Virusi vya aina hii bado vinaendelea kutumiwa na kutengenezwa na wadukuzi duniani. Virusi hivi hudai malipo ya fedha ili kufungua tena mafaili ya mtumiaji; ikiwa hatalipa pesa hizo kwa wakati atapoteza mafaili yake daima.

*3. MyDoom*

Hiki ni kirusi kilichoibuka manamo mwaka 2004 na kuathiri kompyuta zilizokuwa zinatumia programu endeshi ya Window; kirusi hiki kilikuwa kikisambaa kwa kasi sana kwa njia ya barua pepe baada ya kile cha ILOVEYOU.

Inaaminika kuwa kirusi hiki kilitengenezwa na mtu aliyelipwa kwani kilikuwa na maandishi “Andy; I’m just doing my job, nothing personal, sorry,” – (Andy; Ninafanya kazi yangu, hakuna kitu binafsi, samahani)

Inakadiriwa kirusi hiki kilisababisha hasara ya takriban dola bilioni 38.

*4. Melissa*

Kirusi cha Melissa kilitengenezwa na David L. Smith mwaka 1999. Kirusi hiki kilianza kusambaa kupitia faili la Microsoft word lililokuwa linadaiwa kuwa na nywila (password) za tovuti za ngono. Inadaiwa kuwa mtumiaji alipopakua faili hili na kulifungua ndipo kirusi hiki kilipoingia kwenye kompyuta yake.

Kirusi hiki kilituma barua pepe kwenda kwenye orodha ya watu wote walioko kwenye barua pepe ya mwathirika ili kujisambaza. Kirusi hiki kiliathiri taasisi za kiserikali, benki na hata watu binafsi.

Taasisi mbalimbali za kiusalama zilifanikiwa kumk**ata David L. Smith ndani ya kipindi kisichozidi wiki moja tangu kutengenezwa kwa kirusi hiki. Inakadiriwa kuwa kilisababisha hasara ya dola milioni 80.

*5. Sasser*

Kirusi hiki kiliibuka mnamo mwaka 2004, na kilibuniwa na mwanafunzi wa sayansi ya Kompyuta Sven Jaschan aliyebuni pia kirusi cha Netsky.

Kirusi hiki kiliathiri mfumo wa uwakaji wa kompyuta na kuifanya izime mara kwa mara. Kirusi hiki pia kilijizalisha na kujisambaza kwa kasi kupitia mtandao; inakadiriwa kuwa kilisababisha hasara ya dola bilioni 18.

*6. Stuxnet*

Inaaminika kuwa kirusi hiki kilitengenezwa na jeshi la Israeli kwa kushirikiana na Marekani, Stuxnet ni mfano wa silaha ya kivita ya kompyuta (Cyberwarfare).

Kirusi hiki kililenga kuathiri mfumo wa kompyuta wa viwandani (Programmable Logic Controller – PLC) wa vinu vya nyukilia vya Iran.

Inadaiwa kuwa kirusi hiki kililenga kuharibu mfumo wa vinu hivyo na kuvifanya viongeze kasi ya utendaji na hatimaye kulipuka. Mfumo uliolengwa ni ule uliotengenezwa na Siemens; hata hivyo baadae Siemens walikabili kirusi hiki.

*7. Conficker*

Kirusi hiki kinafahamika pia k**a Downup au Downadup, kilibainika mnamo mwaka 2008. Kirusi hiki kiliathiri kompyuta kwa njia ya kuifanya iwe botnet. Botnet ni watumiaji bandia wanaotengenezwa ili kufanya uvamizi wa DDoS.

Uvamizi wa DDoS ni udukuzi unaohusisha kuzalisha maelfu au mamilioni ya watumiaji bandia wanaotembelea tovuti fulani kwa wakati mmoja; hili huifanya tovuti husika ishindwe kuwahudumia wote na kusababisha tovuti hiyo isipatikane.

Inakadiriwa kirusi cha conficker kilisababisha hasara ya takriban dola bilioni 9.

*8. Zeus*

Kirusi hiki kililenga kufanya matendo mbalimbali ya kihalifu kwenye tarakilishi ya mhanga. Kirusi cha Zesus kiliiba taarifa za siri na kumdanganya mtumiaji kufanya mambo mbalimbali ambayo kiuhalisia yangeweka usalama wake hatarini zaidi.

*9. Flashback*

Kirusi hiki kilichoibuka mnamo mwaka 2011, hakikuwa maarufu sana lakini kilidhihirisha udhaifu kwenye kompyuta za Mac. Kirusi hiki kilimdanganya mtumiaji kusakinisha (install) programu ya Flash, kisha kuivamia kompyuta yake na kuifanya kuwa *botnet.*

*10. ILOVEYOU*

Hiki ni kirusi cha kompyuta kinachoaminika kusababisha athari kubwa sana duniani. Kirusi hiki kilibainika mnamo mwaka 2000 na kuanza kusambaa kwa kasi kubwa kupitia barua pepe.

Inakadiriwa kuwa kirusi hiki kilisababisha athari ya dola zaidi ya bilioni 15, pia inaaminika kuwa asilimia 10 ya kompyuta zote zilizokuwa zimeunganishwa kwenye mtandao duniani ziliathirika.

Kutokana na athari za kirusi hiki, mashirika na taasisi mbalimbali zikiwemo za kiserikali zilizima kompyuta zake ili kukabiliana na kirusi hiki.

KARIBU IRINGA TOWN UKUTANE NA "MlewaElectronics".


+WINDOWS MPYA KUFANYA computer yako kuwa nyepesi.



N.k

0766199564 / 0622986231

(I.C.T)

16/04/2021

Je! COMPUTER YAKO IPO "SLOW"? FANYA HIVI ILI IWE NA KASI "IWE FASTA"

✍️

*1. Weka Anti Virus.*

"NB: Virusi vya kompyuta vitatumia sehemu kubwa ya RAM na HDD katika kutekeleza majukumu yake.

*2. Futa Temporary Files*

Kwa watumiaji wa Windows unaweza ukafungua my computer=>Nenda local disk C: au disk yenye Windows=> Fungua Users => Chagua User k**a jina la mtumiaji lipo => AppData=> Local=>Temp

Hapo unaweza ukafuta mafaili yote yaliyomo kwenye hilo folder la temp, kisha restart kompyuta yako.

*3. Punguza vitu katika Hard Drive yako*

*4. RAM ya kompyuta yako ni ndogo, ongeza RAM*

📌Windows XP kiasi kidogo cha RAM kiwe 1GB

📌Windows 7 kiasi kidogo cha RAM kiwe 2GB

📌Windows 8, 8.1 na 10 kiasi kidogo cha RAM kiwe 4GB

*5. Funga baadhi ya Programs k**a unarun Programs nyingi kwa pamoja*

*6. Update Windows yako (Mfumo endeshi)*

Ni muhimu sana kuupdate windows yako kila updates zinapotoka sababu updates zinakuja na maboresho mengi hasa ya kuisalama katika kompyuta yako.

*7. Punguza Add-Ons kwenye browser (kivinjari) yako*

Wingi wa Add-on kam vile youtube downloader, ruler, games, znet hupunguza ufanisi wa kompyuta kwa kiasi kikubwa sana, hivyo hakikisha unaunistall baadhi ya add-on ambazo huzitumii mara kwa mara.

KUTANA NA "Mr: MLEWA" MTAALAMU WA TEHAMA (ICT), IRINGA TOWN.

0766199564 / 0622986231


#(I.C.T)

25/03/2021

UTATA JUU YA KIFO CHA RAIS "JF KENNEDY" WA MAREKANI

✍️
...Risasi hii ilipigwa katika muda ambao Rais Kennedy, mkewe Jackie na Gavana Connally wote walikuwa wamegeukia mkono wa kushoto kupungia wananchi na ghafla wote wakageuka mkono wa kulia kupungia wananchi walio upande huo.

Ni muhimu kukumbuka kwamba katika muda huu walikuwa wekwisha lipita Jengo la *Texas School Book depository,* na wamelipa mgongo kwa kuliacha umbali wa takribani mita 81.

Risasi ya pili kupigwa (risasi ya kwanza nitaiongelea baadae) ilifyatuliwa sekunde ambayo Rais *Kennedy* ameinua mkono mmoja juu akiwapungia wananchi.

Risasi hii ilimpenya nyuma yake katikati kabisa ya shingo na nyama ya juu ya bega na kusababisha uharibu Mdogo kwenye uti wa mgongo, na kisha kupenya ndani na kuharibu sehemu ya juu kabisa ya pafu la kulia na kutokea kooni ikiharibu sehemu kubwa ya koromeo.

Baada ya kupigwa na risasi hii, katika kipande cha video unaweza kumuona Rais Kennedy akiwa amekunja ngumi na kuelekeza mkono mbele ya uso wake usawa wa mdomo k**a vile anakohoa na kuinama kwa mbele kidogo akiegemea upande wa kushoto aliko mkewe.

Pia unaweza kumuona mkewe akiwa anamkumbatia kwa kuzungusha mkono wake mabegani kwa Kennedy kumuuliza k**a yuko 'OK'! (Mpaka muda huo hakujua k**a mumewe amepigwa risasi).

Risasi hii hii ya pili iliyompiga Kennedy, ilipotoka kooni kwa Kennedy ilienda moja kwa moja ya kumpiga Gavana Connally!
Risasi hii ilimpiga Gavana Connally mgongoni chini kidogo ya kwapa upande wa kulia na kutengeneza tundu la umbo la duara na kuharibu kiasi cha inch 4 cha mbavu yake ya tano upande wa kulia na kisha kutokea kifuani katika chuchu.

Risasi hii hii baada ya kutoka kifuani kwa Gavana Connally kupitia kwenye chuchu ilitua kwenye mkono wa kulia wa Gavana Connally, juu kidogo ya kiganja na kuvunja vunja sehemu hiyo katika vipande vinane.

Risasi hii hii, hatimaye ikatua kwenye paja la kushoto la Gavana Connally.

(Nitaeleza huko mbeleni kuhusu utata wa risasi hii ya pili iliyompata Kennedy na Gavana Connally kwa pamoja na ile Risasi ya kwanza ambayo haikuleta madhara yoyote).

Risasi ya pili kumpata rais (ambayo ilikuwa ni risasi ya tatu kupigwa) ilimpata kichwani upande wa juu kulia.

Risasi hii ilifumua kabisa eneo hilo la kichwa na kusababisha sehemu ya ubongo wa mbele kumwagika.

Damu nyingine ikaruka nyuma ya gari kwenye 'trunk' na nyingine kutua mpaka kwenye mkono wa kushoto wa afisa wa *Secret Services* aliyekuwa anaendesha gari ya wanausalama waliokuwa gari ya nyuma ya Rais.

Ndani ya sekunde mbili baada ya mumewe kufumuliwa na risasi kichwani, First Lady Jacqueline Kennedy akaruka kutoka kwenye siti yake na kuanza kuparamia nyuma ya gari kwenye trunk.

Tofauti na wengi wanavyodhani kwamba alikuwa anajaribu kukimbia kuokoa maisha yake, ila ukweli ni kwamba alikuwa anaokota kipande cha mfupa wa fuvu la kichwa kilichodondoka kwenye nyuma ya gari kwenye trunk baada ya mumewe kufumuliwa kichwa na risasi. Baada ya kukichukua haraka haraka akarejea kwenye siti yake. (Tafuta kipande cha video na ujoridhishe zaidi).

Sekunde hii hii ambayo First Lady alikuwa anaparamia gari kwenye trunk, katika gari ya nyuma (follow up car), Special Agent Clint Hill ambaye alikuwa ananing'inia kwenye mlango wa mbele kushoto akaruka na kuanza kuikimbilia gari iliyombeba rais na first lady.
Dereva wa gari la rais alikuwa ameongeza mwendo baada ya mushkeli kutokea na dhahiri kuonekana kwamba rais yuko hatarini.
Hivyo basi ilimbidi Clint Hill kujaribu kuparamia gari mara kadhaa mpaka alipofanikiwa kuidandia gari na mara moja kuwafunika rais na first lady akiwakinga kwa kutukia mwili wake k**a ngao.

Baada ya Agent Clint Hill kuwakinga Rais na mkewe dhidi ya shambulio lingine lolote la risasi kuwafikia, gari ya rais liliendeshwa kwa kasi kubwa likifuatiwa na pikipiki za pembeni na ile follow up car ya maafisa usalama.

Wakati haya yote yanatokea zilikuwa zimebaki takribani dakika tano pekee kufika walikokuwa wanaelekea, *Trade Mart.*
Kwahiyo baada ya gari iliyombeba rais kuanza kuendeshwa kwa kasi, takribani saa 6 na dakika 35 walipita eneo la Trade Mart na kuelekea moja kwa moja hospitali ya Parkland Memorial Hospital ambako waliwasili majira ya saa 6 na dakika 38 na kupokelewa kisha *Rais Kennedy* alipelekwa moja kwa moja chumba cha dharura.

Licha ya watu wa usalama kujitahidi sana kuratibu taaarifa za kilichotokea zisivuje kabla ya taarifa rasmi ya serikali, lakini majira ya saa 6 na dakika 40 kituo cha televisheni cha CBS kikakatisha Igizo lililokuwa linaonyeshwa kwenye televisheni yao na kutoa *"Breaking News" kuwa msafara wa Rais WETU KIPENZI umeshambuliwa huko Dallas.*

Baadae k**a muda wa saa 6 na dakika 45, Dan Rather mwandishi wa habari wa kituo cha CBS alifanya mawasiliano kwa siri sana na daktari anayemfahamu hapo hospitalini na kuvujishiwa taarifa kuwa kuna uwezekano mkubwa Rais Kennedy hayuko hai.

Ifahamike kwamba maafisa wa Secret Services waliwaleta hapa viongozi wengine wote wakuu waliopo kwenye msafara, yaani First Lady Jacqueline Kennedy, Makamu wa Rais Johnson, Mkewe Lady Bird na Gavana Connally ambaye alikuwa chumba cha wagonjwa mahututi.

Ilipofika saa 7 kamili madaktari wakatoa taarifa yao kwa viongozi wa serikali na wanausalama waliokuwepo hapo kwamba, licha ya kutumia ujuzi wao wote na maarifa yao yote, *wameshindwa kuokoa maisha ya Rais JF Kennedy, kwamba Rais Kennedy amefariki.!!*

Huko mtaani habari zilikuwa zinaenea kwa kasi k**a moto wa kifuu, kuwa Rais Kennedy amefariki, hivyo kwa busara watu wa usalama wakashauri kuwa itolewe taarifa rasmi kuhusu kifo cha Rais Kennedy ili kuepusha mkanganyiko na taharuki iliyopo mtaani.

Makamu wa Rais Johnson akakubali hilo lakini akaamuru taarifa hiyo itolewe kwa umma mara baada ya yeye kuondoka hapo hospitali kwa sababu ya usalama wake, kwamba hataki yeyote ajue kuwa yuko hapo hospitali kwa kuwa kwa vile Rais ameuwawa tayari yawezekana yeye k**a Makamu wa Rais akawa ni "next target"!

Saa 7 na dakika 26 Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson akaondolewa kwa siri kubwa kutoka Parkland Memorial Hospital na kupelekwa uwanja wa ndege wa Love Field ambako Airforce One ilikuwa imepaki.

Baada ya Makamu wa Rais kuondoka tu, dakika saba baadae yaani saa 7 na dakika 33 Katibu Msaidizi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Malcolm Kilduff ya Marekani akafanya mkutano na waandishi wa habari hapo hapo hospitali na *kuutangazia rasmi ulimwengu kuwa Rais JF Kennedy amefariki baada ya kudunguliwa na risasi na mtu asiyejulikana.*

Bw. Kilduff hakujibu swali lolote la waandishi wala kutoa taarifa nyingine yoyote. Alipotoa taarifa hii tu akaumaliza mkutano na wanahabari.

Baada ya waandishi wote kuondoka na kubakia watu wa serikali pekee na wanausalama ndani ya Hospitali kulitokea kisa ambacho naamini wengi hawajawahi kukisikia.

Ni kwamba, katika sheria za Marekani kipindi hicho zilikuwa zinaelekeza kwamba, endapo Rais atafariki akiwa jimbo Fulani.. Mwili wake unakuwa chini ya mamlaka ya jimbo na sio serikali kuu.

Sasa, yule bwana swahiba wa Rais Kennedy na Katibu wake wa teuzi Kenneth O'Donnell, yule ambaye alimuamuru Afisa wa Secret Services, Agent Kellerman kuwa gari la Rais liondolewe paa na kubaki 'kibnda wazi', akatoa tena maelekezo kwa wanausalama wauondoe mwili wa Rais Kennedy kutoka hapo hospitalini na kuipeleka uwanja wa ndege wa Love Field na kuipakia katika Air Force One.

Lakini madaktari walikataa mwili huo kuondolewa hospitalini bila kufanyiwa 'Autopsy' (uchunguzi wa kina wa kidaktari kuhusu chanzo cha kifo) ukizingatia kuwa Rais Kennedy amekufa kwa mauaji ya kukusudiwa.

Bw. Kenneth O'Donnell akasisitiza kuwa hakuna muda wa kutosha kufanya Autopsy kwani Air Force One inatakiwa iondoke mara moja kuwarudisha Makamu wa Rais na First Lady Washington kwa sababu za kiusalama na First Lady amekataa kuondoka bila mwili wa mumewe....INAENDELEA.


*NB.* HAJAWAHI TOKEA RAIS WA MAREKANI ALIYEPENDWA NA RAIA WAKE KUMZIDI HUYU "JF KENNEDY" ALIONGOZA NCHI KWA MIAKA MIWILI NA NUSU TUU!!! MWAKA WA *(1961-1963)*

KUTANA NA "MlewaElectronics" MAGWIJI WA...*👇

📌 *COMPUTER*
📌 *Tv*
📌 *SIMU*
📌 *RADIO & Vifaa Vyote Vya Umeme

#0766199564 / 0622986231
IRINGA TOWN | JIRANI NA UWANJA WA MWEMBETOGWA

#(I.C.T)

Want your school to be the top-listed School/college in Iringa?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Iringa