Shamba digital
WAFUGAJI CHATO WAIOMBA SERIKALI KUFANYA TAFITI ZA KINA KABLA YA CHANJO ZA MIFUGO
Wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Chato mkoani Geita wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Uvuvi na Mifugo kufanya tafiti za kina kabla ya kutoa chanjo kwa mifugo yao, wakidai kuwa baadhi ya chanjo zilizotolewa hapo awali zimesababisha kuibuka kwa magonjwa yasiyofahamika na kusababisha vifo vya mifugo wao
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara, wakulima hao wakiongozwa na Mbunge wa Chato Kusini, Pascal Lutandula, pamoja na simoni kondera walisema kuwa mwaka juzi mifugo mingi ilipoteza maisha huku mingine ikiugua magonjwa ambayo wafugaji hawajawahi kuyashuhudia awali, hali iliyosababisha hasara kubwa kiuchumi.
Mbunge Lutandula aliitaka Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuhakikisha tafiti za kisayansi zinafanyika kikamilifu kabla ya chanjo yoyote kuletwa kwa wafugaji, ili kuondoa hofu na kulinda mifugo dhidi ya madhara yasiyotarajiwa.
“Hatupingi chanjo, tunachohitaji ni uhakika wa kisayansi kuwa chanjo hizo ni salama na zinaendana na mazingira ya mifugo yetu,” alisema Lutandula.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Bashiru Ally Kakurwa alisema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kufanya maboresho makubwa katika sekta ya uvuvi na mifugo, ikiwemo kuimarisha tafiti za chanjo na kuweka ruzuku ili kuwasaidia wafugaji.
Waziri Kakurwa aliongeza kuwa tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ili kuhakikisha chanjo zinazotolewa zinakuwa salama, zenye ufanisi na zinazolenga kuongeza tija kwa wafugaji pamoja na kuimarisha uchumi wa sekta ya mifugo nchini.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Busanda/Geita
Geita