Taifa Digital Forum
"Tumewaahidi wananchi kuimarisha usimamizi wa sekta hii, na ni lazima ahadi hiyo itimie. Katika kulitekeleza hilo, Mheshimiwa Waziri pamoja na Menejimenti ya Wizara, kuna jambo nilikuwa nasikiliza kwa makini ulipokuwa ukizungumza. Niliposikia unasema... ‘tunafanya katika ngazi yetu, tunashirikiana...’ nilikuwa nasikiliza kwa makini, lakini kichwani kwangu nilikuwa nawaza jambo.
Ikiwa tumeweza katika upande wa uwekezaji kuweka huduma zote ndani ya nyumba moja—kuanzia upimaji, usajili, usimamizi wa ardhi hadi utoaji wa hati—nadhani hata hili linawezekana. Tunaweza kuwa pamoja, na hili litawezekana endapo mtakuwa na chombo kinachoitwa Kamisheni ya Ardhi.
Nimeona ndani ya wizara mna Makamishna na mna Kamishna Mkuu wa Ardhi, lakini ukweli ni kwamba kamishna hawezi kuwepo bila kuwa na kamisheni. Basi, nawaomba mkalitazame upya suala hili—muundo wake mpya. Katibu Mkuu Kiongozi yupo hapa, kaangalieni umuhimu wa kuwa na Kamisheni ya Ardhi na kubainisha vizuri majukumu yake. Nadhani hii itarahisisha zaidi utendaji wenu. Kwa hiyo, litazameni hilo kwa umakini."
Amesema Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Ardhi ya mwaka 1995, Toleo la mwaka 2023, leo Machi 17, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Dodoma