Ofisi ya Rais - Tamisemi

Ofisi ya Rais - Tamisemi

Share

Prime Minister’s Office, Regional Administration, and Local Governments (TAMISEMI) is a government Ministry under the Prime Minister’s office.

Photos from Ofisi ya Rais - Tamisemi's post 06/07/2026

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Matavilla atembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI lililopo viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam leo juni 6,2026

Photos from Ofisi ya Rais - Tamisemi's post 28/06/2026

SIMIYU,MWANZA MABINGWA MPIRA WA WAVU

Na OWM-TAMISEMI,Iringa

Timu ya Mpira wa Wavu Wasichana kutoka Mkoa wa Simiyu, imetetea ubingwa wake baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa fainali ya UMISSETA iliyochezwa leo tarehe 27 juni 2026.

Mchezo huo wa fainali umechezwa katika viwanja vya Chuo cha ualimu Kleruu Manispaa ya Iringa Mkoani humo, ambapo mashindano ya mwaka huu yanafanyika kitaifa.

Simiyu imeifunga timu ya Mkoa wa Mbeya Seti 3-0, katika mchezo ambao ulikuwa wa kusisimua muda wote.

Kwa upande wa Wavulana mkoa wa Mwanza umetwaa ubingwa kwa kupata ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Mbeya.

Mkoa wa Mbeya uliingiza timu mbili katika hatua ya fainali, hali inayoashiria kukua kwa mchezo huo mkoani humo kwa miaka ya hivi karibuni.

Fainali hiyo inahitimisha rasmi michezo ya mpira wa Wavu katika UMISSETA 2026, mashindano ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 28 Juni 2026.

27/06/2026

Songwe Yatwaa Ubingwa wa Handball UMISSETA 2026

OWM-TAMISEMI,Iringa

Timu za Mpira wa Mikono (Handball) wavulana na wasichana kutoka Mkoa wa Songwe, zimeibuka kuwa mabingwa katika mashindano ya UMISSETA 2026.

Fainali ya michezo hiyo imechezwa leo tarehe 27 Juni 2026 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Iringa Wasichana.

Kwa upande wa wavulana, Mkoa wa Songwe umeshinda magoli 30-29 dhidi ya Morogoro katika mchezo uliokuwa wa kasi na kuvutia kwa dakika zote.

Nayo timu ya wasichana kutoka mkoa wa Songwe, ilifuata nyayo za kaka zao, kufuatia ushindi wa magoli 24-15 ilioupata dhidi ya timj ya Mkoa wa Tabora.

Fainali hiyo imehitimisha rasmi michezo ya Handball katika mshindano ya UMISSETA 2026, ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Iringa.

Emmanuel Majura Mratibu wa Handball amesema Mkoa wa Songwe umeweza kupata ushindi huo kutokana na maandalizi mazuri iliyoyafanya.

Pia amezungumzia juu ya ushindani mkubwa ulioshuhudiwa mwaka huu, akieleza kuwa ulitokana na kuongezeka kwa hamasa ya mchezo huo katika mikoa mbalimbali.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Goverment City, Mtumba. TAMISEMI Street
Dodoma