VETA
08/07/2026
VETA Yaanza Mafunzo ya Uchimbaji Madini Chini ya Ardhi, Wataalamu Wazawa Kuongezeka
Tanzania inatarajia kuongeza idadi ya wataalamu wazawa wenye ujuzi wa kisasa katika sekta ya madini baada ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuzindua mitaala sita ya mafunzo ya uchimbaji wa madini chini ya ardhi, hatua inayolenga kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika miradi ya madini na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Akizungumza Julai 8, 2026 wakati wa kupokea rasmi mitaala hiyo na mpango wa utekelezaji wake, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi Tanzania (TCM), Mhandisi Philbert Rweyemamu, amesema sekta ya madini inaendelea kuwa mhimili muhimu wa ukuaji wa uchumi kupitia uzalishaji, ajira, mapato ya Serikali na maendeleo ya viwanda, hivyo inahitaji nguvu kazi yenye ujuzi unaokidhi matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchimbaji wa madini chini ya ardhi.
Amesema kwa miaka mingi kampuni za madini zililazimika kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi kutokana na uhaba wa wataalamu wa Kitanzania, lakini kupitia Mradi wa Mafunzo ya Ufundi wa Madini (IMTT), VETA imeanza kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kufanya kazi katika migodi ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Abdallah Ngodu, amesema mitaala hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa VETA na wadau wa sekta pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), ili kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.
Amesema, kwa hatua ya awali, utekelezaji wa mitaala hiyo utaanza katika Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Moshi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Migodi Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, amesema kuanza kutumika kwa mitaala hiyo kutaimarisha utekelezaji wa sera ya ushiriki wa Watanzania katika sekta ya madini (Local Content) kwa kuzalisha wataalamu wazawa watakaopunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje ya nchi.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kaskazini, Monica Mbelle, ameeleza kuwa mitaala hiyo inahusisha mafunzo ya Uendeshaji wa Mitambo ya Kubeba na Kusafirisha Miamba Migodini; Uendeshaji wa Mitambo ya Kuchimba Mahandaki; Uendeshaji wa Mitambo ya Kuchimba Mashimo Marefu; Uendeshaji wa Mitambo ya Kuchimba Mashimo ya Ndani ya Miamba; Maandalizi ya Ulipuaji wa Miamba Chini ya Ardhi pamoja na Matumizi Salama ya Vifaa vya Kunyanyua na Kufunga Mizigo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
VETA Head Office, 12 VETA Road, 41104 Tambukareli, P. O. Box 802, Dodoma Tanzania, Email: Info@veta. Go. Tz Telephone: +255 26 2963661 Fax: +255 22 2863408 Url: Www. Veta. Go. Tz
Dodoma
PLOTNO.18
Opening Hours
| Monday | 07:30 - 21:30 |
| Tuesday | 08:00 - 21:30 |
| Wednesday | 07:30 - 21:30 |
| Thursday | 07:30 - 21:30 |
| Friday | 07:30 - 21:30 |
09/07/2026