Layers Pro

Layers Pro

Share

19/04/2026

haiwezekani kuku ana siku 35 awe hivo ukitembelea mabanda ya wafugaji wengi kuku k**a hao unakuta wana miez miwil had nanusu

πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½

Nitaweka picha ya hao kuku wa siku 35 ili uwaone, tuliwapost Alhamisi trh 26 March 2026

Tuendelee kujibu hii hoja...

Iko hivi Ukuaji wa kuku unategemea mambo haya makubwa matatu : aina ya kuku, chakula na mfumo wa ulishaji

1.Aina ya kuku

aina tofauti za kuku chotara zina ukuaji tofauti mfano aina hii kwenye picha huwezi kulinganisha ukuaji wake na chotara wengi wanaofahamika, kiukuaji Hawa ukuaji wao uko juu

Hapa kwenye aina ya kuku ongezea na ubora wa vifaranga, yaani aina inaweza kuwa ile ile ila vifaranga wasiwe na ubora

Kwenye picha Hawa ni kuku wapya kwahiyo bado hawajafamika k**a hao wengine [sitaki kuwataja kwa kuheshimu majina ya biashara za wengine] sisi wenyewe tumewafuga wakati tunafanya majaribio ya formula ya vifaranga kuanzia trh 5 January 2026

2.Chakula kutegemeana na unatumia chakula gani itaathiri ukuaji wa kuku wako hapa hata k**a ni Cha kununua dukani au kuchanganya mwenyewe vyakula havifanani

3.Mfumo wa ulishaji kuanzia kiwango cha chakula, masaa ya mwanga, aina ya ufugaji [k**a ni huria,nusu huria au wanafungiwa bandani] na nafasi bandani hivi vyote vinaathiri ukuaji wa kuku

Kwenye comment nitakuwekea video ya Tanbro, kwa mwaka Jana tumefuga sana Tanbro mpaka wafugaji wakawa wanahisi labda CFP ni kwa ajili ya Tanbro ndio maana tulipoanza kutoa darasa kuhusu formula ya vifaranga mwaka huu tukaamua kutumia vifaranga wa hii kampuni ya SQ ili kuondoa dhana kuwa CFP ni kwa ajili ya Tanbro

πŸ‘‰ Muhimu Post zetu tunaweka picha kwa ajili ya kujifunza sio kwa lengo la kutangaza biashara ya vifaranga wanaonekana kwenye picha kumbuka sisi Hatuuzi vifaranga ❌ [Effect inaweza kuwepo ila hii inaitwa unintended project goal]

Hivyo amua wewe mwenyewe utafuga vifaranga wa chotara wa kampuni gani kulingana na sababu zakoβœ…

πŸ‘‰Kuonesha umri wa kuku kwenye Picha tunaandika hivi k**a hii imeandikwa " DAY 35 " maana yake kuku huyu ana siku 35, k**a hatujaweka umri kwenye picha usitusingizie 😊

Sasa Angalia hii video ya Tanbro wa siku 43 kwenye comment section kwasababu wakati tunawafuga Hawa Tanbro wafugaji walikuwa wanabisha kuhusu umri wao k**a ambavyo Leo baadhi wanakataa kuwa Hawa kwenye picha sio kuku wa siku 35 πŸ˜ƒ

Want your business to be the top-listed Business in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Weyula
Dodoma
41201

Opening Hours

Monday 07:30 - 19:00
Tuesday 07:30 - 19:00
Wednesday 07:30 - 19:00
Thursday 07:30 - 19:00
Friday 07:30 - 19:00
Saturday 09:30 - 19:00