Pastor Xavier
25/03/2025
KILA MTU ATABEBA MZIGO WAKE.
Ezekieli 18:20
[20]Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.
Kila mtu atalipia gharama ya matendo yake mwenyewe mbele za Mungu.
Kila mtu atatoa maelezo kuhusu maisha yake alipokuwa hapa duniani siku hiyo mbele za Mungu.
Hakuna ambaye atasimama badala ya mtu mwingine.
Kuwa mcha Mungu ni swala binafsi na ni swala la kuamua wewe mwenyewe, siyo swala la kuangalia mbona fulani hamwabudu Mungu, la hasha.
Ezekieli 18:21
[21]Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.
Kwa kuwa Mungu ni wa msamaha, huwa anasamehe watu ambao wako tayari kumrudia yeye Kwa kuziacha njia zao mbaya(dhambi).
Mungu anataka kutenda Kwa halali na haki, siyo Kwa dhuluma na kuzishika amri zake.
Ezekieli 18:22
[22]Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi.
Mungu anapomsamehe mtu, huwa anaamua kuziweka mbali kabisa dhambi hizo za awali na kuamua kuanza ukurasa mpya na mtu aliyefanya toba, hivyo ni wajibu wa mtu husika kufanya toba ya kweli na kuamua kuishi Kwa kumwelekea Mungu.
Exavery Nduye
0757-754176
Mchungaji
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Dodoma
255