UNI_Updates.tz
13/02/2023
To you all UNI_updates.tz members.... we love you and we serve with smile
12/02/2023
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili wanaosoma taaluma ya uandishi wa habari na mahusiano ya jamii(BAJP) katika chuo kikuu Cha Dodoma,wametembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo kilometa kadhaa kutoka chuoni kwao Kwa lengo la kufanya matendo ya huruma hospitalini hapo ikiwa ni SUPRA CHARITY SEASON 1.
Ikiwa ni siku hiyo ya tarehe 11 February 2023, mhadhiri msaidizi wa chuo hicho Ndg. Mary Kafyome aliyeambatana na vijana hao ameeleza kuwa tukio Hilo lililenga kuwaandaa vijana hao kuwa maafisa uhusiano Bora hapo baadae.
Mbali na kutoa vitu mbalimbali Kwa wagonjwa vya kuwasaidia,tukio lingine la msingi zaidi walilofanya hospitalini hapo ni kutoa damu ili kuokoa maisha ya watu wengine. Mkuu wa kitengo cha DAMU SALAMA Ndg. Kocy Kibaja amewashukuru Sana vijana hao na kuomba watu wengine pia waige mfano huo ili kuokoa maisha ya mamia ya watu wanaopoteza maisha Kwa kukosea damu.
_udom255
10/02/2023
Katika msimu huu wa valentine's Day, UDOM wameona ndio muda wao kuisimamisha semista, watu walambe glucose ndani ya siku moja ili wapate nguvu mpya kukabiliana na UE kwa kuja na kitu cha kujipoza na semista hii .Kitu chenyewe ni SCARLET FASHION SHOW itakayofanyika Pestana Siku ya kesho tarehe 11/02/2023.
Kwenye show hii kubwa sana na wakali wa comedy watakuwepo.
Subiri uone na kuthibitishaa kuwa "Burudani ni sehemu ya maisha"...Kwanini upitwe?
10/02/2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kukutana na Kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Wanafunzi, Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania TAHLISO February 11 Mwaka huu.
Mazungumzo hayo kati ya Rais na Vijana hao wasomi yanatarajiwa kufanyika Ikulu Jijini Dodoma.
TAHLISO ni jumuiya ya Vijana wasomi wa Vyuo vikuu na Vyuo vya kati Nchini.
09/02/2023
Afisa uhusiano wa umma wa Hospitali ya Benjamini Mkapa(BMH) jijini Dodoma Mheshimiwa Jeremiah Mbwambo alikutana na wanafunzi wa Bachelor of arts in journalism and Public relations(BAJP) wa mwaka wa kwanza na wa pili, wa Chuo kikuu cha Dodoma, februari 8,2023 chini ya usimamizi wa mkufunzi wa somo la uhusiano kwa umma yaani Public relations Mrs. Mary Hospicia Kafyome kwa lengo la kuwanoa vijana hao na kuwaandaa kuwa maafisa uhusiano wa umma bora hapo badae.
Aidha katika semina yake Mheshimiwa Jeremiah Mbwambo amebainisha kuwa Benjamin Mkapa hospital(BMH) ndiyo hospitali pekee inayopandikiza figo kwa kutumia madaktari wake wazawa. Lakini pia aliwaambia wanafunzi wawe wanaojituma katika kazi na kuwashauri kabla ya kuanza kufanya kazi katika ofisi watakazo chaguliwa ni heri wakajua ofisi vizuri kwani itawasaidia kulinda picha ya taasisi na hivyo taasisi itawategema.
Pia mkufunzi wa somo la uhusiano wa umma, Mrs. Kafyome alitoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Mbwambo kwa ushirikiano wake.
Pia Mrs. Kafyome kwa kushirikiana na wanafunzi wake wameandaa charity chini ya Students of UDOM Public Relations Association(SUPRA) katika hospitali ya Benjamin Mkapa siku ya jumamosi tarehe 11/02/2023 wakiwa na ujumbe unaosema UHUSIANO BORA, JAMII BORA.mia22
_udom255
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Dodoma