Football Updates
28/05/2026
Taarifa zisizo rasmi zinadai vilabu kutoka Tanzania vinavutiwa na winga wa Al Hilal Omdurman, Jean Claude Girumugisha ingawa hakuna OFA rasmi..
Akizungumza na Uyui FM, Patrick Gakumba ambaye ni wakala wa winga Jean Claude Girumugisha anasema Tanzania hakuna timu inayoweza kumsajili mchezaji wake Jean Claude Girumugisha kutokana na ada yake.
Gakumba anasema ada ya winga huyo kwa sasa ni inaanzia Tsh Bilioni 03..🔥
Hata hivyo, winga huyo amekuwa bidhaa ya moto sokoni, vilabu mbalimbali vinatarajiwa kupigana vikumbo kuiwinda saini yake...📌
27/05/2026
Kulingana na kanuni za Shirikisho la soka la Uganda, mchezaji aliyecheza walau mechi tano kwenye klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uganda kisha akaondoka klabuni, mchezaji huyo ana haki ya kupata medali ikiwa timu yake itatwaa ubingwa..
Allan Okello atavaa medali 🥇 ya ubingwa baada ya klabu yake ya zamani,Vipers kutwaa ubingwa...
Okello aliifungia Vipers mabao 03 msimu huu (mzunguko wa kwanza) kabla ya kuondoka na kujiunga na Yanga SC.
Star boy 🥇
27/05/2026
Kwa tathmini ya haraka tu, Azam FC msimu huu wana defence nzuri..
Safu ya ulinzi inaundwa kuanzia kwa namba 6, full backs 2&3, center backs 4&5 pamoja na goli kipa..
Dimba lao la chini msimu huu limekuwa chini ya Himid Mao, mimi hupenda kumwita "Mzee Kigogo".
Himid anatoa darasa jinsi gani ya kucheza kwenye zone ile, anafanya kazi kubwa sana kupokonya mipira, anapiga pass kwa usahihi mkubwa na analinda vyema ukuta wake..
Kwenye full backs, imekuwa ni mwendelezo tu wa kile ambacho wamekuwa bora kwacho misimu kadhaa tangu wapandishwe senior team..
Captain Lusajo Mwaikenda mbavu ya kulia na Pascal Gaudence mbavu ya kushoto..🔥
Central defenders, bwana mdogo Twalib Nuru amekuja kutoa surprise kwa ma pro ambao tayari wana experience ya kutosha, ameaminiwa kucheza mechi nyingi ikiwemo za CAF pamoja na Fuentes Mendoza, huku Yoro Diaby, Landry Zouzou wakiingia pia mara chache kwenye kikosi.
Msimu bora kwao k**a idara ya ulinzi...
Golini pia wamekuwa wakigawana mechi, Aishi Manula, Zuberi Foba na Issa Fofana.
Wametoa mchango bora sana wakiihakikishia clean sheets 21 kwenye mechi 25 🔥
•Aishi Manula - 11 clean sheets
•Zuberi Foba - 09 clean sheets
•Issa Fofana - 01
Hili ni miongoni mwa maeneo ambayo Azam FC wako bora sana, hata kuwapo nafasi waliyopo sasa utagundua ni sare walizopata mechi za mwanzo kutokana na kukosa ufanisi wa kufunga..
Wakati huo bado Feisal na Iddi Nado hawaja waka k**a ilivyosasa..
Binafsi naona Azam FC watahitaji maboresho kidogo tu kwenye eneo hilo (ULINZI) kwaajili ya kuongeza nguvu zaidi📌
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Address
Dodoma