Wasafi FM
AMBAO HAWAJARIPOTI JKT WAITWA KWA MARA YA MWISHO
Baadhi ya vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini wakashindwa kuripoti kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali, wamepewa fursa ya mwisho ya kujiunga na mafunzo hayo kwa kuripoti katika makambi yaliyo karibu na maeneo wanayoishi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo JKT Brigedia Jenerali Peter Mnyani, amesema utaratibu huo umeelekezwa na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, ili kutoa nafasi kwa vijana ambao walikwama kufika katika makambi waliyopangiwa awali.
Afande Mnyani amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti kuanzia Juni 12 hadi Juni 15, 2026, katika makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo yao ya makazi ili kuendelea na mafunzo k**a ilivyopangwa.
Hata hivyo, amefafanua kuwa utaratibu huo hauhusishi Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, Kambi ya Makutupora JKT iliyopo mkoani Dodoma pamoja na Chuo cha Uongozi cha JKT kilichopo Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Amesisitiza kuwa vijana wote ambao bado hawajaripoti wanapaswa kutumia fursa hiyo ya mwisho kufika makambini ndani ya muda uliotolewa, kwani baada ya Juni 15 hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza wa kuripoti.
Ngonya
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Mbezi Beach
Dar Es Salaam