Christ Embassy Tanzania - Virtual Church
06/06/2026
RHAPSODI YA UHAKIKA
Jumamosi, June 6, 2026
Mchungaji Chris

UKWELI KUHUSU ADUI YETU
Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa msh*taki wenu Ibilisi, k**a simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze (1 Petro 5:8).
Kuna mitazamo na dhana nyingi kuhusu Shetani, adui yetu, lakini ni Neno la Mungu pekee ndio hufunua utambulisho wake halisi. Biblia ndio kitabu chenye mamlaka zaidi ya vyote kuhusiana na kweli za kiroho, kwa kupitia Biblia, Mungu anafunua alikoanzia ibilisi, jinsi alivyo, na utendaji kazi wake. Pasipo kuwa na maarifa haya, watu hutembea katika ujinga; lakini ukiwa na maarifa haya, unatembea katika nuru , ufahamu, na utawala.
K**a unaamini katika Mungu, ni lazima pia uamini kile Alichosema. Mungu uyu huyu aliyejifunua kwetu katika Maandiko pia anatuambia waziwazi kwamba ibilisi yupo. Hivyo basi, kukataa kuwa Shetani yupo, ni kukataa ushuhuda wake Mungu mwenyewe. Maandiko hayamsemi ibilisi kuwa ni wazo la kufikirika; maandiko yanamuonyesha kuwa ni kiumbe wa kiroho mwenye nafsi halisi.
Tena Biblia pia inatuambia kuhusiana na mwanzo wake. Aliwahi kuwa malaika aliyekuja kumuasi Mungu na kuwa adui. Mtu anapopuuzia uwepo wa Shetani, mara nyingi hujikuta akishindwa kubaini tabia na njama zake za uovu za kujaribu kushawishi, kudanganya, kuua, na kuharibu.
Lakini maarifa ya Neno yanakupa ufahamu (utambuzi), ujasiri, na faida ya kuenenda kwa hekima na kiroho maishani. Inakuwezesha kuwa na maarifa na imani unayohitaji ili kutembea katika utawala endelevu juu ya Shetani na wajumbe wake wa giza.
Alisema, “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru” (Luka 10:19). Haleluya! Ndiyo, unaye adui, ibilisi; lakini ni adui aliyeshindwa. Yuko chini ya miguu yako. Hauko katika huruma yake; ametiishwa kwenye mamlaka yako katika Kristo. Wewe ni mkuu kwake, kwa maana unazo nguvu [na uweza] wa kumtoa (Mathayo 10:8, Marko 16:17). Tembea katika maarifa haya na utumie mamlaka yako katika Jina la Yesu.
SALA
Mpendwa Baba, ninashukuru kwa nuru ya Neno lako yenye kunipa ufahamu juu ya kweli za kiroho. Ufahamu wangu umeangaziwa kupitia Maandiko, na ninatembea katika hekima, utambuzi, na ushindi. Nina usikivu, nina mizizi katika kweli yako, nikidhihirisha mamlaka na utawala nilio nao ndani ya Kristo juu ya Shetani na ufalme wa giza, katika Jina la Yesu. Amina.
MASOMO ZAIDI:
1 Petro 5:8 AMPC; Yakobo 4:7; Luka 10:18-19
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yohana 20:1-18 & 1 Mambo ya Nyakati 20-22
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Wakorintho 15:50-58 & Muhubiri 3-4
Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”
Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional
Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye https://www.rhapsodyofrealities.org
04/06/2026
RHAPSODI YA UHAKIKA
Alhamisi, June 4, 2026
Mchungaji Chris
MKUU KWA SHETANI NA MIUNDO YAKE
Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama (Mathayo 12:25).
Bwana Yesu alifunua ukweli muhimu kuhusu Shetani, ufalme wake na muundo wake pale alipozungumzia mash*taka ya Mafarisayo waliposema anatoa pepo kwa kutumia Beelzebuli, mkuu wa pepo (mashetani). Katika kuwajibu, Aliwauliza swali jepesi la kustaajabisha: “Awezaje Shetani kumtoa Shetani? (Marko 3:23). Kupitia kauli hii, Bwana alifunua jambo la muhimu kuhusiana na asili ya utendaji kazi wa kishetani.
Bwana Yesu alielezea kwamba ufalme uliogawanyika (uliofitinika) wenyewe kwa wenyewe hauwezi kusimama. Hili linatuambia suala la msingi: Shetani anatenda kazi kwa muundo uliopangiliwa, anao ufalme. Ufalme huu unatenda kazi kwa ushirikiano na vyeo. Makundi ya kipepo hufanya kazi katika mfumo maalumu uliotengenezwa ili kukinzana na makusudi ya Mungu na kuleta uchochezi kwenye masuala yahusuyo dunia hii.
Ufunuo huu hutusaidia kuelewa ni kwa nini Biblia inazungumza kuhusu falme, mamlaka, wakuu wa giza hili, na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Waefeso 6:12). Maneno haya hufafanua juu ya vyeo na mamlaka yaliyo katika ufalme wa giza wa Shetani. Lakini wote wako chini ya miguu yako.
Biblia inasema tumeketishwa pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho, “Juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia” (Waefeso 1:21). Ndani ya Kristo, wewe ni wa Ufalme wa Mungu, ufalme ulio mkuu na wa juu tena wa mbali sana, wenye kutawaliwa na haki, kweli, na mamlaka ya kiungu.
Kwa hiyo, haijalishi hata kuwe na miundo ya namna gani kwenye Ufalme wa Shetani au hata awe na utendaji kazi wa namna gani; wewe ndiwe kinara. Unayo mamlaka. Kupitia Neno la Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu, unasimama thabiti katika ushindi na mamlaka ya Kristo juu ya Shetani, kuzimu, na nguvu za giza.
Hakuna mfumo wa giza unaoweza kushinda dhidi yako au mamlaka ya Ufalme wa Mungu ambamo unatokea. Haupo kwenye himaya [ya mamlaka] yao. Umo kwenye Ufalme wa Mwana wa pendo la Mungu (Wakolosai 1:12-13), ambamo unatawala na kushinda juu ya mambo yote kwa Yesu Kristo. Haleluya!
SALA
Baba Mpendwa, ninashukuru kwa nuru ya Neno lako yenye kunipa kuona katika kweli za kiroho. Ninatembea katika mamlaka ya Ufalme wa Mungu na kusimama imara katika ushindi aliokamilisha Kristo kwa ajili yangu. Kila uchochezi wa giza umetiishwa chini ya mamlaka ya Jina la Yesu, na ninaishi kwa ushindi [na shangilizo] katika kweli yako, katika Jina la Yesu. Amina.
MASOMO ZAIDI:
Marko 3:23-24; Luka 11:20; Wakolosai 1:12-13
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yohana 18:28-19:1-16 & 1 Mambo ya Nyakati 14-16
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Wakorintho 15:29-39 & Mithali 31
Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”
Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional
Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye https://www.rhapsodyofrealities.org
31/05/2026
RHAPSODI YA UHAKIKA
Jumapili, May 31, 2026
Mchungaji Chris

WEMA WA MUNGU
Daudi akasema, Je, hakuna mtu yeyote wa nyumba ya Sauli bado, nipate kumtendea mema ya Mungu? (2 Samweli 9:3).
Katika Agano la Kale, neno lililotafsiriwa "rehema" linatokana na neno la Kiebrania "hesed." Linamaanisha wema, lakini haswa zaidi, ni wema wa agano; wema unaotokana na agano, si katika upendeleo. Mfano wa Daudi na mtoto wa Yonathani, Mefiboshethi, unatupa picha ya wazi na ya vitendo ya jinsi rehema ya agano inavyofanya kazi (2 Samweli 9).
Muda mrefu baada ya kifo cha Yonathani na hata katika utawala wake k**a mfalme, Daudi aliguswa na agano alilokuwa amefanya na Yonathani. Aliuliza swali la makusudi: “…Je, kuna mtu yeyote aliyesalia katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani?” (2 Samweli 9:1).
Daudi hakuwa akiuliza k**a kuna mtu ambaye angeweza kumtambua tu. Neno "onyesha" lililotumika linamaanisha kuthibitisha. Daudi alikuwa akimtafuta mtu ambaye angeweza kuonyesha kwake wema wa agano kwa vitendo na kwa wazi wazi. Kwa kweli, katika mstari wa 3, Daudi aliuita "mema ya Mungu." Ni jambo la kina sana!
Mefiboshethi alikuwa mlemavu wa miguu yote miwili na kiuhalisia alikuwa ametelekezwa na kusahaulika na wengi. Hata hivyo, aliitwa mbele ya mfalme. Lakini alipofika mbele ya Daudi, alianguka kifudifudi kwa hofu. Alitarajia hukumu kutoka kwa mfalme aliyemrithi babu yake, Mfalme Sauli.
Lakini maneno ya kwanza ya Daudi yalikuwa, “Usiogope”; hiyo ndiyo lugha ya huruma kila wakati. Daudi alimrudishia ardhi yote iliyokuwa ya Sauli na kisha akampa kitu kingine kikubwa zaidi: mahali pa kudumu mezani pa mfalme. Huu ulikuwa wema wa agano, ambao Daudi aliuita “wema wa Mungu.”
Kwa nini aliiita kuwa ni wema wa Mungu? Ni kwa sababu fadhili ya agano huonyeshwa kwa mtu ambaye hana sifa au madai yoyote. Mtu huyo hastahili. Rehema ya kweli hutiririka kutoka kwa mkubwa hadi mdogo. Kwa nguvu ya rehema hiyo, yule asiye na kitu huletwa katika ufalme; huinuliwa, huheshimiwa, na kuketi mezani, k**a vile sisi leo tulivyoketishwa pamoja na Kristo. Hii ni nguvu inayobadilisha ya wema wa agano.
Inatukumbusha Maandiko yasemayo: “Humwinua maskini kutoka mavumbini, na kumpandisha maskini kutoka jaani, ili awaketishe pamoja na wakuu, na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha utukufu” (1 Samweli 2:8). Labda kuna mtu anakujia rohoni mwako hata sasa anayehitaji wema wako wa agano; nenda na umwonyeshe huo wema wa Mungu.
SALA
Mpendwa Baba, nakushukuru kwa agano lako la wema na rehema kwangu. Ninapokea wema wako kwa uelewa na shukrani. Ninaishi katika ufahamu wa rehema yako, nikifurahia maisha ya heshima, ushirika, na riziki uliyoniletea, katika Jina la Yesu. Amina.
MASOMO ZAIDI:
Zaburi 36:7; Isaya 54:10 NKJV; 2 Samuelii 9:5-8
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yohana 15:18-16:1-16; 1 Mambo ya Nyakati 5-6
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Wakorintho 14:31-40; Mithali 27
Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”
Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional
Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye https://www.rhapsodyofrealities.org
29/05/2026
RHAPSODI YA UHAKIKA
Ijumaa, May 28, 2026
Mchungaji Chris

NEEMA, REHEMA, NA AMANI
Neema na iwe kwenu, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo (2 Yohana 1:3).
Katika barua kadhaa za kitume, Roho anasisitiza baraka yenye nguvu. Kwa mfano, katika baadhi ya maandishi ya Paulo, anaanza kwa maneno, “neema, rehema, na amani,” k**a ilivyo katika 1 Timotheo 1:2, “Neema, rehema, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Yesu Kristo Bwana wetu.” Anarudia baraka hiyo hiyo katika barua yake ya pili kwa Timotheo na tena kwa Tito.
Mtume Yohana analirudia hili pia: “Neema na iwe pamoja nanyi, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo” (2 Yohana 1:3). Kwa nini mitume walitamka neema, rehema, na amani kila mara? Ni kwa sababu ya umuhimu wake mkubwa katika maisha ya Kikristo.
Maandiko yanaonyesha wanaume na wanawake waliopata neema mbele za Mungu. Kwa mfano, Nuhu alipata neema mbele za Bwana hata wakati hukumu ilipoamuliwa juu ya nchi. Mwanzo 6:8 inatuambia, “Lakini Nuhu alipata neema machoni pa BWANA.” Neema ilimweka kwa ajili ya ulinzi na ushindi. Hii inaonyesha kwamba mtu anapopata neema, rehema hufuata.
Neema, rehema na amani hufanya kazi pamoja. Warumi 5:1-2 huunganisha amani yetu na Mungu na neema ya Yesu Kristo ambamo tunasimama ndani yake: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake….”
Unapopata neema machoni pa Mungu, Yeye hukuhurumia. Waebrania 4:16 inasema, “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Neema ni ule upendeleo wa kiungu unaoachiliwa kwako. Ni kazi ya Mungu katika maisha ya mtu.
Katika Agano la Kale, neno la Kiebrania ni "chen" na linamaanisha neema ya Mungu. Kupitia neema hiyo, kupitia tendo hilo la neema ya Mungu, Yeye hutumia ushawishi wake katika maisha yako ili kuhakikisha kwamba unafanikiwa. Neema yake inafanya kazi akilini mwako, ikikusaidia kufikiria mawazo sahihi. Inaathiri moyo wako na kukuongoza kufanya maamuzi sahihi, zaidi ya uwezo wako wa kawaida au akili ya kibinadamu.
Neema hukufunika, hukuzunguka, hukulinda, na inakulinda ili usifanye makosa. Tembea katika ufahamu huu. Hujaachwa peke yako katika werevu na uwezo wako wa kibinadamu; ushawishi wa mbinguni uko juu ya maisha yako, ukielekeza hatua zako na kukusababisha matokeo yanayozidi uwezo wa asili. Haya ndio maisha ambao Mungu amekupa katika Kristo.
SALA
Mpendwa Baba, nakushukuru kwa neema yako tele, rehema, na amani inayofanya kazi maishani mwangu. Ushawishi wako wa kiungu huongoza mawazo, maamuzi, na matendo yangu, ukiniongoza katika njia ya mafanikio na haki, iliyothibitishwa katika ushindi, katika Jina la Yesu. Amina.
MASOMO ZAIDI:
Waebrania 4:16 AMPC; 2 Timotheo 1:2; 2 Wakorintho 9:8; Tito 1:4
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yohana 14:15-31; 1 Mambo ya Nyakati 1-2
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Wakorintho 14:10-19; Mithali 25
Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”
Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional
Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye https://www.rhapsodyofrealities.org
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Address
Christ Embassy Tanzania, Loveworld Arena Near Songas Ground , Salasala
Dar Es Salaam