Pastor fide.
10/06/2026
WANAWAKE DODOMA.
Mungu amewapa neema ya kumiliki miji msioijenga , nyumba msizonunua! Baraka yenu inatoka katika kumbu kumbu la torati 6. Je maana yake nini? Na je inatupasa kufanya nini ili tuweze kuona na kupokea tulichopewa siku ya leo?
KUMB 6:10 "Tena itakuwa atakapokwisha Bwana, Mungu wako, kukuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe,
11 na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vimefukuliwa usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba;"
Neno linaimanisha baraka za Mungu hazitokani na nguvu zako peke yako, hayo unayopitia ni kwasababu unategemea akili zako mwenyewe. Mungu anaweza kukupa vitu ambavyo hujavifanyia kazi moja kwa moja. Mungu anaweza kufungua kufungua fursa au mafanikio ambayo yanaonekana kuzidi juhudi zako za kawaida. Ndio mana kuna wakati ukiangalia mali zako wakati mwingine unajiuliza imewezekanaje hauamini k**a ni wewe umetafuta! Ni kwasababu ni Yeye kafanya kwako, zaidi ya akili yako na ufahamu wako .
Unaweza ukawa na kazi na usimiliki chochote, Neno pia linasema asiyefanya kazi na asile kwa nini wewe ufanye kazi bado unalala njaa! Bado umepangisha! Na pengine unalipwa vizuri! Nguvu za utajiri ni Mungu anakupa havitegemeani na unafanya nini! Mama ntilie anaweza akajenga nyumba, banker hana why? Kwa sababu wanategemea akili zao na kazi zao. Ukimtegemea Mungu huwa anafanya zaidi ya fahamu zetu.
*JE MUNGU ANATAKA NINI KWETU?* ILI TUWEZE KUPOKEA HIZI MALI TUSIZOTAFUTA SISI.
1.Mche Bwana Mungu na kuzishika sheria zake na amri zake. Zipi hizo? kutokuabudu miungu wengine. Usiabudu Miungu wengine, usiwe mwizi mwizi, mjanjaja, Mjanjanjanja! Msizini ili mpate msivyotafuta! Wewe mpende kwa moyo wakowote, kwa akili zetu zote, na mawazo yetu. Na mengine mengi.
Unapoumcha Mungu kutakubadilisha The way you think, speak, you act , utakuwa na Mindset of a Believer: mindset of faith.
Atataka familia yakoz watoto wako wote umkabidhi yeye ili adui asipate upenyo kupitia kwako itakuzuilia kupokea.
Tena anasema atawasukumia mbali adui zakoKumb 6:19. "ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, k**a alivyosema Bwana "
adui ni nani! Wale wanaleta Negative Influences, wana wivu, gossipers, criticisers, mockers ili wakutoe hapo. Watakuzuia kupokea baraka hizi kwa hiyo lazima akutenge nao. Katika Matthew 13:25-26. Wapo inasema walipolala adui akawavizi usiku akapanda magugu katikati ya shamba lao la ngano, akaenda zake. Cain out of jealously he killed abel, How many are jealous of you.?
Adui mwingine Nehemiah 4:1-3 “ Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe. "
Watafanya kila jambo usione baraka wala kufikia hatma yako. Tembea na Kumb 6 yote uimbe kinywani kwako utakutana na baraka hii ya ajabu! Mambo ambayo hujawahi kufikiria Mungu anaenda kukupa.
31/05/2026
Hivi unawezaja kuacha kumtegemea Mungu aliyekuumba kwa kusudi ye ndiye anayejua hatima yako halafu ukaanza kumtegemea Mganga wa kienyeji, una akili timamu kweli! Anakuomba kafala ya mmeo ya watoto wako vile uvipendavyo upo tuu humo unawaza hela huku unatembea na maumivu kibao nusu mfu nusu mtu. Hela zenyewe za masharti. Amesema Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Sasa unatafuta faida wapi wewe? Mwanamke amka amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kuwa kinga yake, moyoni mwake kamwacha Mungu. Ingia toba niite tuchome mikoba yako uanze na Mungu. Trust him fully. Wengine mmefilisika mmekata tamaa amka mwamini Mungu k**a fedha ilishapita kwenye mikono yako jua ipo... Mahala mkondo wa maji yanapita hata mvua ikikata miaka 100 siku ikinyesha yatapita hapo, wewe ni mkondo wa i hela zilipita hapo zitapita tena dabo, hata k**a hujawahi shika fedha leo tunatengeneza mikondo zitarudi hapo double. Acha kuwaza fedha ni kitu kidogo kwa Mungu, anachotaka kwako mtegemee tu. Mpe nafasi Mungu.
Aksanteni sana Namanga super kwa kunialika. Tuendelee kuomba hata nyumba kwa nyumba mpaka tunatoboa, hatuwezi kuishia popote tutaishia pale Mungu amekusudia
14/05/2026
Zaburi 125 :1-2 " Wamtumainio Bwana ni k**a mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.K**a milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele."
10/05/2026
KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA.
Utajua unamcha Bwana kwa sababu akili yako haiwezi kuwa ile ile, ufahamu wako hauwezi kuwa uleule. Tabia yako haiwezi kuwa ile ile, lazima vitu viongezeke kwako sio kupungua, ukiona kuwa vile vile au kupunguka. Jua kuna mahali humtii Mungu. Kwa sababu kumcha Mungu ni kumtii na kumtegemea yeye.
Mithali 1:17 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, wapumbavu hudharau hekima na adabu.”
Ukishakuwa na Mungu jikane, itakusaidia ujue Mungu anataka kuwekeza nini ndani yako. Kwa sababu, Mungu hawezi kukaa ndani yako na mambo yako ya kale. Amesema lazima atafanya jambo jipya ndani yako, kwa hiyo akiingia ndani yangu si mimi tena bali ni Mungu, kwa hiyo kila nitakalofanya litangatia ni Mungu anayepaswa kuonekana, k**a ni tabia aonekane Mungu, k**a ni mavazi aonekane Mungu, chochote nifanyacho nitafanya Mungu akionekana.
Using'ang'ane na ufahamu ule ule na akili ile ile. Acha akuonyeshe baada ya yeye kuingia ndani yako, nini anaenda kubadilisha, ndio maana ya kujikana, wewe ufe yeye afufuke ndani yako. La sivyo Utaendelea kumuona Mungu vile vile. Mungu hazoeleki ana jambo jipya kila siku.
Nimekutana na watu wengine wanauliza siku hizi hatukuoni huku na huku. huvai nguo za kubana tena?, huvai vigauni vifupi, kuna mmoja kaniuliza leo. Nikapata na somo la kufundisha, jamani jibu ni ndio kwa sababu game changer Mungu mwenyewe yuko ndani yangu anabadilisha systems. So kaeni kwa kutulia bado mtaona mambo ambayo macho hayajawai kuona wala masikio hayajawahi kusikia, Mungu kabeba chombo chake.
Halafu Mungu hagawani utukufu na Mtu. Akisema hata k**a utachekwa, watakubeza we fanya utukufu ubaki kwake. Ukianza kupima pima na wanachokwambia maana yake unataka kugawa utukufu utashindwa.
Isaya 42:8 a"Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine........
ukaamua kumcha Mungu kweli kweli, ukaongozwa na yeye, ukajikana na kuruhusu yeye awe ndani yako na kufanya anayotaka wewe, huwezi kuwa na akili ile ile. Ukiona unamtumikia Mungu akili ile ile, ufahamu ule ule, ukipewa maagizo unaanza kupima ya Mungu na wanayokwambia watu my friend akili mpya utaisikia mbinguni. Tulia kwanza mche Mungu akupe maarifa.
07/05/2026
Be humble!
Watu wakikuheshimu, wakikupenda wakikuchagua wakakupa zawadi, be humble usiinue mabega juu, usiwadharau yote yamefanyika kwa neema ya Mungu.
Mithali 16:18 "Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko."
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Sakina
Arusha