Radio5tz
News segment comprises of accurate; soft and hard local, international and national news. Entertainment segment encompasses Blues, Afro vibes and R&B, of both local (African) and international flavors that provide a rare source of relaxation in the hectic world we live in.
25/05/2026
Wananchi wa Jiji la Arusha leo wamekumbwa na changamoto kubwa ya usafiri kufuatia madereva wa daladala kusitisha huduma za usafirishaji katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo, hali iliyosababisha mamia ya wakazi kulazimika kutembea kwa miguu kufika katika shughuli zao za kila siku.
Maeneo ya Mianzini, Sanawari na Ngulelo yalishuhudia idadi kubwa ya abiria wakisubiri usafiri kwa muda mrefu bila mafanikio, huku wengine wakiamua kutembea kutokana na ukosefu wa magari ya usafiri wa umma.
Madereva wa daladala waliohusika katika mgomo huo wameeleza kuwa hatua hiyo imetokana na kile walichodai kuwa ni ongezeko la faini kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), pamoja na kupanda kwa gharama za uendeshaji wa magari, hususan bei za mafuta zinazozidi kuongezeka kila siku.
Aidha, madereva hao wameiomba serikali kupitia mamlaka husika kuruhusu marekebisho ya nauli za daladala kutoka kiwango cha sasa hadi angalau shilingi 1,000, wakieleza kuwa kiwango kilichopo hakikidhi gharama za uendeshaji na kinaendelea kuathiri shughuli zao katika kipindi hiki cha changamoto za kiuchumi.
13/05/2026
Bia namba moja ya mabingwa Tanzania, Safari Lager, imeandika historia baada ya kutangaza udhamini wake wa Kombe la Dunia la FIFA 2026, na kuwa chapa ya kwanza ya bia kutoka Tanzania kupata nafasi kwenye jukwaa kubwa zaidi la mpira wa miguu duniani. Hii ni hatua kubwa inayomilikiwa na kila shabiki wa mpira wa Tanzania ambaye amewahi kuamini!
Kuna jambo kubwa linakuja tarehe 23 Mei – endelea kufuatilia pamoja na kurasa zetu za mitandao ya kijamii ili kugundua jinsi unavyoweza kuwa sehemu ya ukishirikiana na !
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Njiro Block J
Arusha
P.O.BOX15883