Mr Meshacking

Mr Meshacking

Share

15/06/2026

GHOST OF TANVERI
SEHEMU YA KWANZA (01)
***

Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha nje ya kuta kubwa za Black Dome Prison. Radi zilikuwa zikilimulika anga lililo tawaliwa na wingu zito lililotanda usiku huu huku ngurumo nzito zikisikika kwa sauti za mtetemo wa kuogofya ndani ya gereza hilo lenye sifa mbaya kuliko magereza yote nchini Tanveria.

Kwenye jengo namba saba la wafungwa hatari, wanaume zaidi ya mia mbili walikuwa wamesimama kwenye foleni ndefu wakisubiri kupata chakula cha usiku. Askari waliokuwa juu ya mnara wa ulinzi walizungusha taa kali huku bunduki zao zikiwa tayari kwa matumizi muda wowote.

Kelele za wafungwa, na matusi ya hapa na pale vilisikika kwa wingi eneo hilo.

Mwanaume mmoja mwenye mwili mwembamba, macho yake yakiwa ni myekundu, na kovu kubwa shingoni alikuwa amesimama nyuma ya mfungwa mpya aliyekuwa kimya muda wote kwenye foleni hiyo ya chakula.

“Oya… wewe ni mgeni, sio?” mwanaume huyo alihoji kwa sauti ya chini, lakini mfungwa huyo mpya hakujibu chochote.

“Unaonekana mlaini sana, sijui umefikaje hapa,” mwanaume huyo aliendelea kuongea lakini bado hakupata jibu lolote. Alitabasamu kwa dharau na kuongeza,

“Sikiliza brother… hili sio gereza la watu wa aina yako. Humu wamejaa wauaji hatari na magaidi. Sidhani k**a na wewe upo kwenye kundi lolote la watu hawa niliowataja.”
Mfungwa huyo mpya aliendelea kusimama kimya huku macho yake akiwa ameyakaza mbele, kwenye beseni kubwa la chakula.

“Humu ndani kufa ni jambo la muda mfupi sana. Sidhani k**a wewe utaweza kudumu humu.”
Safari hii, mfungwa mpya aligeuza macho yake taratibu na kumtazama jamaa huyo aliyekuwa anaongea bila mpangilio.

“Ni heri ukashughulika na mambo yako, huenda ukayanusuru maisha yako,” mfungwa mpya aliongea kwa msisitizo huku akimkazia macho jamaa huyo.

“Sura yako na maneno yako haviendani kabisa, hivi unadhani unanitisha" Jamaa huyo anaongea kwa msisitizo lakini mfungwa huyu mgeni aliishia kumuangalia tu pasi na kusema lolote

"Ila kwa kuwa umechagua kuwa mkaidi, wacha tuone itakavyokuwa,” jamaa alipiga mkwara, lakini mfungwa huyu mpya hakuonekana kuwa hata na chembe ya uoga.

Foleni iliposogea mbele, alichukua trei yake ya chakula yenye ugali na maharage yaliyochemshwa. Akageuka na kuanza kuondoka zake, akimuacha huyu jamaa akimshangaa huku akiwa na maswali mengi kichwani.

*****

Usiku huo huo wa mvua kubwa, pembezoni mwa jiji ndani ya jumba kubwa la kifahari lililozungukwa na walinzi wenye silaha nzito, magari ya thamani yalikuwa yameegeshwa nje huku kamera za usalama zikiwa zimejaa kwenye jengo hilo.

Ndani ya chumba kikubwa chenye mwanga hafifu, watu watatu walikuwa wamekaa kwenye sofa za thamani wakinywa mvinyo wa gharama kubwa.

Mwanamama mmoja mwenye ngozi ya kahawia iliyong’aa, aliyevalia suti nyeusi ya kifahari alikuwa amekaa kwenye sofa dogo lililopo kwenye chumba hicho, macho yake yakiwatazama kwa bashasha wanaume wawili waliokuwepo ndapi humo, ambao nao walikuwa wamevalia suti zilizowakaa vyema kwenye miili yao.

Mwanamama huyo alijulikana kwa jina la Madam Lucy.
Ndani ya serikali ya Tanveria, wengi walimfahamu k**a msaidizi maalumu wa mkurugenzi wa TISA, Madam Lucy ni moja kati ya watu wanaoogopeka sana hapa nchini Tanveria.

“Kwahiyo ni rasmi?” mmoja kati ya wanaume hao aliuliza huku akiweka glasi yake mezani.

“Mwisho wake umewadia. Hakuna anayejaribu kucheza na sisi kisha akabaki salama. Never!” Madam Lucy aliongea kwa madaha huku tabasamu pana likiutawala uso wake.

“Hakika moyo wangu sasa una amani. Adrian sio mtu wa kawaida. Tunatakiwa tujipongeze kwa kuweza kumdhibiti yule shetani aliye ndani ya mwili wa malaika,” mwanaume mwingine anaongea kwa msisitizo

“Ila ili tujihakikishie ushindi huu, tunapaswa kumuangamiza kabisa huyu mtu, maana hajawahi kutabirika.”

“Sajenti Leo, unadhani Adrian anaweza kutoroka Black Dome?”

“Madam, huyu binadamu sio mwepesi kihivyo,” alijibu Sajenti Leonardo Frederick kwa msisitizo, kisha akaendelea kuongea.

“Namjua vizuri sana Adrian. Ni bora tuchukue hatua mapema kabla mashetani yake hayajaamka. Nadhani wote tunajua kuwa hata kumpeleka huko gerezani ni kwa sababu yeye mwenyewe aliamua kuwa mpole, ila bila hivyo sidhani k**a tungeweza kukabiliana naye. Kwa hiyo, kivyovyote vile, tunatakiwa kumuangamiza Adrian akiwa huko huko gerezani.”

“Sawa Sajenti Leo, hilo swala niachie mimi. Nitahakikisha huyo panya anapotea kwenye uso wa dunia hii,” K**anda Sospeter aliongea kwa kujiamini.

“Hili jambo sasa lipo mikononi mwako, Peter,” Madam Lucy alisema huku akiwatazama wawili hao.

“Ondoa shaka, Madam. Naamini dunia iko mbioni kumsahau kabisa Adrian Dominic,” alisisitiza K**anda Sospeter, na vicheko vikatawala ndani ya chumba hicho huku wakigongeana glasi zao na kunywa mvinyo huo kwa ushindi mdogo walioupata.

ITAENDELEA...

Hakikisha kuwa una like na kufollow page hii ya Story za Jay ili kuweza kusoma story kali na za kusisimuaTHE GHOST OF TANVERIA
BY WIZZY JONES
Contact: +255 785879708

CHAPTER ONE (01)

Hakikisha kuwa una like na kufollow page Mr Meshacking ili kuweza kusoma story kali na za kusisimua.

09/06/2026

Mr Meshacking MAJUTO NI MJUKUU
Dada zangu kuna kitu cha kujifunza hapa!!

Niliolewa na mwanaume mpole sanaaaaaa miaka mitano iliyopita, yani nikisema mpole ni mpole mno, hakunifatilia hata siku moja, hakuniuliza nini wala nini, alinpa uhuru wa kutosha, nikiaga naenda mahali anasema nenda, hata k**a narudi saa

nane usuku atanifata tu maana hakuwa akipenda niendeshe gari usiku hata sikumoja, nikirud na tax ananifokea sana,,,, gari mafuta niliwekewa kila safari, vocha niliwekewa, alinikuta fresh from collage so hata kazi sikuwa nayo, akanitafutia kazi,baada

ya ndoa, nikapata, na nikaanza, kuna kipindi akawa ananiambia niache gari anafeele proud kutembea na mimi kwenye gari, kifupi alinijali sana, sana sana,,,,,,,, sasa ile care yake ndio ninayoikumbuka hadi leo hii, wamama, wadada, wanandoa,

K**a una mwanaume anakujal mshikilie vizuri sana. Si kwamba alikuwa hanithamini, alikuwa ananithamini sana tu, sikuwah kumfumania hata mara moja, ana likuwa muwazi sana kwangu, yani muwaz sanaaa, ofisn kwao walinijua, alipenda

kunitambulisha kila kona,,,, kuna kipindi alienda south kikazi ikawa kila weekend ananitumia nauli naenda, siku zingine anakuja yeye hadi aliporudishwa huku, ni upendo wa ajabu,, Nilichofaidi kwake tu ni kwamba alikwenda kwetu akapaona palivyo, akasema atanisaidia kujenga, alivunja nyumba ile na kumjengea mama yangu kijumba kidogo cha kumtosha mwenyewe, akamuwekea mashamba, hadi leo namkumbuka, kwao yye kazaliwa peke yake, mama yake alifariki wakati amemzaa tuu, akasema anamlea mama yangu k**a mama yake, hana dada wala kaka wa kuzaliwa tumbo moja, wako wa ndugu wengine tu

NATHIBITISHA KWA KINYWA CHANGU, COMPANY ULIYONAYO INAWEZA KUBADILI MSIMAMO NA KUSHUSHA AU KUZIDISHA HESHIMA YAKO,,, company niliyokuwa nayo mimi ilikuwa ni ya kupunguza heshima kwangu na ndio iliyoniponza, staki kuiongelea sana hilo maana wengi rafiki zangu wako humu, ila kifupi tu, nilifanya ujinga mno, naujutia hadi kesho,

Nikiwa na rafiki zangu tuliandaa mtoko kwenda bagamoyo kutembea lakini tukapanga tusiwaambie waume zetu ukweli, tudanganye maana wengi wasingekubali tukapanga safari tukasema uongo kwamba ni safari za kiofisi,( mme wangu hakuwa akinifatilia oficn kabisa) basi nikamwambia ni safar ya kikazi tunaenda bagamoyo, yeye oficn kwake ni boss, so anaweza kuondoka muda wowote bila swali, basi akasema nitakufata, sitawasumbua nitakaa hotelini tu, wewe ukimaliza kikao chenu utanikuta chumbani, nakumbuka siku hiyo nilichukia sanaaa, yani sanaaaa nilichukia nikamwambia hapana tunalala wawili wawili, akasema basi sawa nenda,

Alinipa hela ya kutosha nikaenda na rafiki zangu tulikuwa group ya watu wanne tu, watatu tumeolewa mmoja bado, basi kufika bagamoyo tuli have fun sana almost three days, nikiwa kule nikakutana na kijana mmoja ambae alinipenda sana (admin naficha jina,,,, ila tumpe KELVIN) basi alikuwa kaja na marafiki zake wengine nafikir nao kuhv fun,

Sasa kila jioni tukiiniga buffet tunakutana nae, akaanza kunitongoza nikagoma, akamfata mmoja wa rafiki zangu akaomba namba akapewa, nashangaaa usiku akanipigia simu, nikakataaa, rafiki zangu walinisisitiza sana nimkubali, kijana mzuri, handsome, nikasema no, ninae mme wangu, simtaki huyu,,,,,

Siku naondoka akaja na diary moja nzuri sana kwenye gari yetu, akaniambia unaondoka nikasema ndio unataka nini, akasema don’t be dry like this akanipa diary yake niichukue k**a kumbukumbu, nikakataa nilipofika mjin mr alinifata, akanipokea akaniambia tu mke wangu toka toka uende huko, nimekuwa mpweke sana,, wkati huo sikujua k**a alipiga simu ofisn kuconfirm k**a ni kweli niliondoka,,, akaambiwa nimejaza AD na sio kwamba nimesafiri kikazi,,, kumbe ukweli aliujua, nashangaa mwanaume huyu hakuniuliza chochote akakaa kimya tu, ila aniliona changez, coz tulipokuwa kweny gari alinikuwa ananiangalia sanaaaaaaaa,,, nikimtazama na mimi anageuka anaangalia pembeni,

Nikamuuliza vipi, akasema nilikumiss tu mke wangu,,,, tukafika home nikaoga nilikuwa nimechoka kesho asubuh tukaondoka, kila mtu na gari yake, kufika ofic hro hakuniambia chochote k**a aliwasiliana na mme wangu aliniuliza tu, umepona? Nikasema ndio akasema karibu tena, basi kazi ikaendelea,,,,,,

Baada ya siku nne tu akaja yule kaka hado oficn kwangu na alielekezwa na mmoja wa hao best zangu, alipofika nilishangaa nikamuuliza nini kimekuleta hapa akasema tuongee kwenye gari, basi nikaingia, jamani ni k**a nililogwa naweza sema kweli tena, k**a hamtaamin basi ila naamini ALINIROGA HUYU KAKA, maana alivyokwua akiongea nikaanza kumpenda,,, nilizidi kumpenda kupita kiasi nikaanzak uona uzuri wkae, nikaanza kumcompare na franco wangu, naona huyu amemzidi kila kitu,

✍️K**a umeipenda andika ENDELEA ..

Baadae aliniaga akasepa, tokea pale nikaanza kumpenda kupita maelezo .. ITAENDELEA...

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

Arusha