GADI TV
Mwanamke mmoja aitwae Rosemary Willium ambaye ni mmiliki wa kituo cha kutoa huduma kwa Waraibu katika kata ya Sokoni One Jijini Arusha, amedai kuwa kutokana na baadhi ya vijana kuingia kwenye uraibu ngono pamoja na vileweshi, na kupelekea athari mbalimbali za kiafya miongoni mwao, amenzisha kituo hicho maalum cha kutoa msaada wa huduma za uraibu, k**a sehemu ya kutoa msaada kwa jamii yake.
Rosemary akizungumza na GADI TV akiwa kituoni hapo, amesema urahibu wa ngono, k**ari na vileweshi, umekuwa ni mwanzo wa vijana wengi kushindwa kutimiza ndoto zao kwa wakati, hivyo huduma hiyo inaweza kubadili mwelekeo hasi kwa vijana hao.
Bibi anayefahamika kwa jina la Tsino Marmo mkazi wa kata ya Rothia wilaya ya Karatu mkoani Arusha, amedai kuwa amejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kikundi cha watu kutaka kumpokonya kimabavu shamba lake lenye ukubwa wa hekari 10, licha ya Mahak**a kumpa haki ya kumiliki shamba hilo mkoani humo.
Bibi huyo akizungumza na GADI TV, amesema kuwa shamba hilo linalong'ang'aniwa na kikundi cha watu hao ambao ni ndugu zake, alipewa na baba yake mdogo k**a sehemu ya ahsante baada ya kumuuguza baba huyo kwa kipindi cha miaka 23 alipokuwa akigua, huku ndugu wengine wakijiweka mbali naye.
——————————————————————————
🎥 ukiwa na tukio la kihabari usisite kutupigia simu, namba zetu ni hizi 👉🏻 0743 888 555 (WhatsApp & Call)
18/05/2026
Kufuatia tukio la kijana aitwae Alvin Asei (pichani) mkazi wa Kirua Vunjo Magharibi mkoani Kilimanjaro, kujikuta katika hali ya majuto makali baada ya kudaiwa amemuua rafiki wa baba yake, kutokana na tuhuma kuwa rafiki huyo alitaka kwenda kumsemea kuwa amekunywa pombe, Jeshi la polisi mkoani humo limesema kuwa Alvin yupo chini ya ulinzi wa Jeshi hilo kwa hatua nyingine za kisheria.
Ikumbukwe kuwa punde baada ya tukio hilo kutokea Mei 12, 2026, Alvin aliambia GADI TV kuwa alitenda tukio hilo kwa kutumia kifaa cha kukatia majani (Mundo), baada ya marehemu kumjeruhi sehemu ya kichwa kwakutumia fimbo ya mkahawa.
Disclaimer: Disturbing Image!
——————————————————————————
🎥 ukiwa na tukio la kihabari usisite kutupigia simu, namba zetu ni hizi 👉🏻 0743 888 555 (WhatsApp & Call)
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Arusha