AFYA FORUM.

AFYA FORUM.

Share

31/08/2023
13/12/2021

UJUE UGONJWA WA KISONONO.

Imeandaliwa na DrGossy352.

Kisonono ni nini?

Kisonono ni maambukizi ya kingono (STI) yanayosababishwa na bakteria ajulikanaye k**a Neisseria gonorrhoea

Ninapataje Kisonono?

Unaweza kupata kisonono kwa kufanya mapenzi kupitia uke, kinyume na maumbile kwa ngono kwa mdomo na mtu mwenye kisonono.

Unaweza kupata kisonono kutoka kwa mtu mwingine hata k**a hawana dalili zozote.

Mwanamke mjamzito anaweza kumwambukiza mtoto wake wakati wa kujifungua. Mtoto anaweza kupata maambukizi ya macho na anaweza kuwa kipofu.

Huwezi kupata kisonono kutoka vyoo vya umma, mabwawa ya kuogelea ya umma ama kuchangamana na watu wengine.

Kisonono inafanya nini kwa mwili wangu?

Kisonono inaweza kuambukiza koo, njia ya haja kubwa, njia ya mkojo, shingo ya kizazi na macho.

K**a isipotibiwa, kisonono inaweza kusababisha maambukizi ya ngozi na vifundo. kisonono inaweza pia kusababisha uti wa mgongo. Uti wa mgongo ni maambukizi yanayozingira ubongo
Kwa wanawake, kisonono inaweza kusababisha maambukizi hatari na kumsababishia mtoto ugumba.
Mwanamke mjamzito anaweza kukiambukiza kichanga wakati wa kujifungua. Kichanga kinaweza kupata maambukizi hatari ya machocho na kinaweza kupata upofu.

Ninatambuaje k**a nina Kisonono?

Watu wengi hajui k**a wana kisonono kwa sababu hawana ishara wala dalili.
Namna pekee ya kuweza kutambua una kisonono ni kupima. Kipimo chenyewe ni kipimo rahisi cha mkojo.
Namna nyingine ni ya kuchukua vipimo kutoka eneo lililoambukizwa na kuona k**a lina maambukizi ya kisonono.

Ishara na dalili za kisonono

Kwa wanaume
• Kusikia k**a kuwaka moto wakati wa kukojoa
• Kutokwa na uchafu katika njia ya mkojo. Uchafu huu unakuwa mara nyingi mweupe ama wa njano
• Kuvimba na kusikia maumivu katika korodani
• Wekundu katika tundu la uume
• Kutokwa uchafu kutoka njia ya haja kubwa au kusikia maumivu.
• Maambukizi ya macho.

Kwa wanawake
• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida katika uke
• Kuvuja damu ukeni
• Maumivu wakati wa kukojoa
• Maumivu kwenye mifupa hasa wakati wa kufanya mapenzi
• Kutokwa uchafu kutoka njia ya haja kubwa na hata maumivu
• Maambukizi ya macho

Ninafanyaje k**a nina Kisonono?

• Daktari wako atakupatia dawa
• Mwambie mpenzi au wapenzi wako kupima. K**a wana kisonono, wanaweza kukupatia kisonono tena ama kumpatia mtu mwingine.
• Daktari wako anaweza kukusaidia kuamua ni nani wa kumwambia kwamba una kisonono. Daktari wako anaweza kukusaidia kuwambia.
• Usifanye mapenzi na mtu yeyote, hata kwa kutumia kondomu, mpaka matibabu yako ya kisonono yatakapokamilika.

Endelea kujifunza mengi na AFYA FORUM.

. we

25/09/2021

Imeandaliwa na:

Dr. .
AFYA FORUM TANZANIA.

Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ni wa hatari sana kwani unaweza kuua katika saa chache tu. Ni ugonjwa unaozuka sehemu mbalimbali ulimwenguni, na katika bara la Afrika umeua watu wapatao 100,000 katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Mlipuko wa kwanza wa meningitis ulitokea Geneva mwaka 1805, na katika bara la Afrika, kumbukumbu zinaonyesha mlipuko wa kwanza ulikuwa mwaka 1840. Imani iliyoenea hapo zamani ilikuwa ni ugonjwa uliotokana na hewa mbaya na kwamba haukuwa ni ugonjwa unaoambukiza.

Kupata tiba ya haraka ni muhimu, lakini pamoja na tiba ya haraka, maambukizi bado huweza kutokea na kuua. Kwa hiyo, kinga kwa kupata chanjo ni ndicho kitu bora zaidi.

Shirika la afya duniani – WHO – limepanga kuutokomeza ugonjwa huu ifikapo 2030.

Meningitis ni uvimbe unaotokea kwenye utando laini (meninges) unaozunguka ubongo na uti wa mgongo. Uvimbe ndani ya ubongo huitwa encephalitis ambao huweza kuwa ni mwendelezo wa meningitis au vikatokea vyote kwa wakati mmoja, hali ambayo huitwa meningoencephalitis. Ikitokea ubongo na uti wa mgongo vyote vikaathiriwa kwa wakati mmoja, neno encephalomyelitis hutumika.

Chanzo Cha Mengitis Ni Nini?


Meningitis huweza kutokea kwa sababu ya maambukizi au bila maambukizi. Kuna virusi, bakteria, fungi, na vimelea wa aina nyingi wanaoweza kuleta meningitis. Magonjwa yanayoweza kusababisha uvimbe mwilini bila maambukizi (k**a systemic lupus erythematosus na Bahcet’s disease) yanaweza kusababisha aseptic meningitis (meningitis isiyotokana na bakteria.) Baadhi ya madawa huweza kusababisha aseptic meningitis, k**a ibuprofen au antibiotic iitwayo trimethoprim-sulfamethoxazole.

Want your practice to be the top-listed Clinic in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Arusha