imacrobot

imacrobot

Share

10/08/2021

KIPIMO CHA TOZO ZA MATANGAZO KATIKA AKAUNTI ZA MITANDAO YA WATU MAARUFU.
Watu wengi maarufu duniani wamekuwa na kawaida ya kupokea matangazo mbalimbali ya kibiashara toka kwa kampuni au watu binafsi.Matangazo hayo huwekwa katika akaunti zao za mitandao ya kijamii na kuwafikia wafuasi wao.Mara nyingi hapa Tanzania watu wengi wanaangalia wingi wa wafuasi(followers) alionao mtu k**a kigezo kikuu cha mtu huyo kupata biashara nyingi za kupost matangazo.Hiyo inaweza kuwa moja ya sababu lakini je unafahamu kuwa wingi wa followers si kigezo kikubwa sana cha akaunti ya mtu kupata tenda nyingi za kutangaza biashara za watu mbalimbali ?.

ENGAGEMENT RATE, hiki ndio kitu pekee kinachofanya akaunti ya mtu kupendwa na wafanyabishara na kupokea tenda nyingi za matangazo.Engagement rate, hii ni hesabu ambayo inapima kiasi gani wafuasi wako na hata ambao sio wafuasi wako wana shiriki katika post zako unazoweka katika akaunti yako kwa ku-like,kukoment,kushea,kur-reply n.k.
Endapo k**a post zako zinapata ushirikiano mkubwa toka kwa wanaokufuatilia basi hali hiyo inamfanya mtu kuaminiwa kuwa na ushawishi na kupata tenda za matangazo katika akaunti yake.

ENGAGEMENT RATE huwa katika mfumo wa asilimia, endapo k**a akaunti yako itapata asilimia nyingi hii itakufanya kuaminika na kupata biashara nyingi za ku-post katika akaunti yako.
Akaunti zenye ENGAGEMENT RATE kuanzia 3% na kuendelea hizi ndizo mara nyingi hupendwa na wamiliki wa biashara na kuzipa nafasi ya kutangaza biashara zao.
Kwa kutumia ENGAGEMENT RATE tutafahamu ni kiasi gani cha fedha kitahitajika kwa mtu mwenye ushawishi kupost post moja ya tangazo la kibiashara.

Tafadhali follow

10/08/2021

MLIMA MREFU KULIKO YOTE KATIKA MFUMU WA JUA UNAOONGEZA HAMU YA MWANADAMU KUTAKA KWENDA KUISHI MARS.
Bila shaka ukizungumzia mlima mrefu duniani wote tunafahamu kuwa ni mlima EVEREST, mlima ambao ndipo mahali palipo kilele cha dunia, lakini je, umewahi kusikia habari za mlima mrefu kuliko yote katika mfumo wa jua ?๐Ÿ˜ฎ

Ndio, OLYMPAS MONS, ndio mlima mrefu kuliko yote katika mfumo wetu wa jua, yaani, ukianza sayari ya kwanza mpaka ya tisa, OLYMPAS MONS ndio mlima mrefu zaidi wenye urefu wa kilomita 22 ambapo ni mara tatu ya mlima EVEREST.

Mlima huu unapatikana katika sayari ya MARS ambayo ni sayari ya nne kutoka jua lilipo.
Mlima huu ni aina ya volcano ambapo tafiti zinasema kuwa, uliwahi kulipuka takriban miaka 25 iliyopita,na kurusha mawe makubwa katika anga la sayari ya mars.

Wengi wanajiuliza, kwanini mlima huu ni mrefu kiasi hiki, na je, itawezekana kwa mwanadamu kuupanda mpaka kufika juu ya kilele chake ??๐Ÿค”
Mlima huu umekuwa mrefu kutokana na kani ndogo ya uvutano (low gravity)iliyopo mars na pia kuupanda mpaka kufika kileleni ni changamoto kubwa sana kutokana na mawe mengi yaliyopo katika mlima huo.

Kwa sasa tutegemee selfie za kutosha ifikapo mwaka 2022 ambapo kampuni ya space x inatarajia kufanya safari yake ya kwanza,kwenda katika sayari ya mars kwa lengo la kuanzisha maisha hukoo.๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Please like comment and follow our page for more contents๐Ÿ˜€๐Ÿ’ช๐Ÿ‘

NB:picha haina uhusiano na taarifa

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Arusha