Fikira Pevu Forum

Fikira Pevu Forum

Share

17/04/2026

Bila kukufuru dini ya mtu but the truth remains...and esp for Men, beware of some priests/ baadhi ya Wachungaji waonazunguka kwenye nyumba zenu kufanya maombi sometime hufanya maombi ya ziada na wake zenu...Afu ukimkataza mkeo asiende maombi mnakosana...

15/04/2026

Ukimtongoza shemeji Yako mjane akakataa unafanyaje na unamtaka?

15/04/2026

it ideal to buy a car before you build a house?

18/03/2026

Unapotoa ahadi za uongo msibani, laana ni kwa nani?Afu Mbona Mwanauame akifariki akaacha mwanamke mrembo matanga huarakishwa, ila wewe mwanaume ukifiwa mke ndo unaona machungu yake...

09/06/2024

Nukuu muhimu; Mpendwa msomaji tunapenda kukujulisha kwamba licha ya kwamba simulizi hili linahusu kisa cha kweli, majina ya watu au sehemu zinazotajwa katika hadithi hii hayahusiki wala kumlenga mtu au sehemu yoyote ambayo Kwa njia moja au nyingine huenda ikashabihiana na hadithi hii...

Wahenga walisema 'kua uyaone' ya dunia ya M***a...lakini pia unaambiwa ukistaajabu ya M***a utaona ya filauni. Sijui k**a wewe msomaji wa makala hii umeyaona yapi? Lakini pengine dunia sio mbaya ila hawa viumbe waishio ndani ya dunia ndo wabaya.
Kutokana na hulka na matendo au mwenendo wa binadamu katika dunia ndo maana kuna watu na viatu. Aidha ndo maana tunaimbiana mashairi yenye vina na mishororo yenye vijembe na mafumbo ili mradi kila mmoja alivyotendwa na hawa viumbe wa Adamu. Siku hizi hata nyimbo za Dini hazitungwi tu Kwa kusambaza ujumbe wa wokovu wa Kristo, ila pia zimesheheni maneno ya kwenye khanga maadamu 'fumbo mfumbie mjinga, mwelevu keshang'amua'. Utasikia..'mashimo waliyonichimbia wameangukamo wenyewe..' ' Mitego waliyonitegea inewanasa wenyewe' ama 'walidhani nitaanguka sasa wanashangaa' hawa wanaoimbwa ni kina nani?
Simulizi letu linamhusu dada mmoja kwa jina Sonita, ambaye Kwa ridhaa yake ameona vema kufunguka ya moyoni kwenye jukwaa la fikira pevu kuhusiana na changamoto lukuki ambazo amezipitia katika Maisha yake.
Dada Sonita ni yatima aliyelelewa na mama wa kambo akiwa na ndugu zake wengine wawili. Mama yao, Bi chao alifariki pindi akimzaa yeye kisha ilibidi bibi yao, Malkia Nyembe, k**a alivyofahamika kuwatwaa na kuwalea. Baada ya muda k**a miaka miwili hivi bibi yao pia alifariki kwa ugonjwa wa pumu. Hapo baba yao Mzee Sizimwe hakuwa na budi ila kuoa mke mwingine. Hivyo sonita na nduguze walilelewa na mama yao wa kambo.
Familia ya mzee Sizimwe haikuwa yenye maisha ya juu katika kujikimu kimaisha, baada ya kustaafishwa kutoka shirika la posta na simu mzee Sizimwe alijishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara hasa yaliyokua na kukomaa kwa muda mfupi, k**a vile vitunguu, nyanya, biringanya, bamia, karoti n.k Alikuwa na ustadi wa kukadiria muda mwafaka wa kusia mbegu na kisha kuhamisha miche ili kuendana na musimu wa mvua za Vuli. Sonita na nduguze hawakuwa na amani siku za upanzi kwani walimjua vema baba yao ambaye hakuwa na simile mtu hata angediriki kuwazuia wasiende shule ilimradi wakapande miche shambani. Kazi ya upanzi ilianza macheo hadi machweo na walipotoka shamba walikuwa hoi kutokana na uchovu.Kutokana na umahiri wake aliweza kulima misimu miwili wa mwaka. Kipindi cha uvunaji wafanya biashara toka marikiti walipanga foleni nyumbani kwake kulangua mazao ya biashara na kazi hii ilimpatia umaarufu mkubwa. Wakati alitembelewa na maafisa ugani ambao baada ya kuona alivyokuwa na bidii ya mchwa, walizitenga bustani zake kuwa kituo cha mafunzo ya wakulima wadogo na walimshauri kujiunga na chama cha ustawi wa wakulima wa ugani ambapo baada ya muda mfupi alianza kupokea mikopo ya pembejeo na zana zingine za kilimo.
Jembe halimtupi mkulima, Mzee Sizimwe hakuwa yule wa mwanzo, baada ya alipata mtaji na kufungua duka la jumla bondeni karibu na eneo la gulioni. Hakuwa na ugumu wa kuwasomesha wanaye alioachiwa na marehemu mkewe Bi Chao.

Sijui kwa nini wahenga walisema kwamba mama wa kambo si mama, bila shaka wangelisema mama wa kambo pia ni mama...mama wa kambo wote wangejua kuthamini utu wa watoto wa kufikia ambao huja kuwalea kwa waume zao. Bi Nanje k**a alivyoitwa mama mdogo wao Sonita hakuwa na matatizo makubwa dhidi yao katika mambo k**a lishe au mavazi, lakini alikuwa na shida moja kubwa... hakupenda wasome. Aidha hakujali hali zao kiafya pale walipougua au kuhitaji matibabu na mara nyingi alisema wanajiuguza kukwepa kazi za nyumbani. Licha ya hayo yote alitokea kumchukia sana Sonita baada ya kugundua kwamba alipendwa zaidi na babake...tufatilie zaidi ili upate uhondo wa stori hii unaponiga...

04/06/2024

Home is home...

Hivi wewe unaishi katika upangaji? Je, ushaishi kwenye nyumba ya kupanga ambayo mwenye nyumba hana kauli wala usemi kwa wapangaji wake? Au ametiwa kiganjani na baadhi ya wapangaji ambao mara nyingi huwa wameishi katika nyumba husika kwa muda mrefu kiasi kwamba utafikiri wao ndo wamiliki wenye nyumba?
Ama kwa hakika k**a imekutokea ukajutia kuilipia hiyo nyumba...
Au pengine ulishawahi kulipia nyumba ya kupanga kisha baadaye ukashindwa kuishi kwa amani na bila shaka ukaamua kuhama kabla pesa ya kodi yako kumalizika? Na katika mazingira k**a hayo wenye nyumba alikurudishia pesa zako? Ndo wale wa kusema 'kiendacho kwa mganga hakirudi' maana huwa hawawezi kurudisha pesa hata kwa dawa...
Wenye nyumba wengine hudai pesa ya amana au uchakavu k**a wanavyoipa majina ambapo mpangaji anatanguliza kiasi fulani kabla ya kukubaliwa kupangisha nyumba na ikitokea umeharibu nyumba kwa njia fulani pesa hiyo itagharamia ukarabati. Lakini endapo umeshindwa kuishi hapo kutokana na sababu nyinginezo utaambiwa hadi apatikane mpangaji mwingine ili pesa yako irudishwe mwisho wa siku linakuwa deni sugu.
Baadhi ya wenye nyumba hata hivo huweka maslahi ya pesa mbele ila panapotokea migogoro kati ya wapangaji wallah hawajishughulishi kuitatua au huegemea upande mmoja wa wale wapangaji viherehere ambao mara nyingi hujionyesha wajuaji ama kwa vile wameishi hapo muda mrefu mfano miaka 3 au 5 n.k hivo basi wao ndo wenye sauti kwa mwenye nyumba.
'Kupanga nyumba si dhambi...'anasema dada Sofia ambaye amepangisha nyumba mtaa wa mabatini, 'lakini inahitaji moyo kuvumilia vituko vya wapangaji wenzako...'na wala haimaanishi kwamba unapokwenda mjini na ukapanga nyumba maana yake huna kwenu...! 'Nyumba ni mali isiyohamishika ndo maana hata wenye nyumba pia hujikuta wamepanga.' Au tuseme haimaanishi kwamba ukiwa na gari huwezi kupanda magari ya wengine na ndivyo ilivyo kwenye swala la nyumba.

Dada Sofia anasema hivi majuzi alipigwa na wapangaji wenzake wawili Kwa kumchangia na kumbe Mungu si Athumani katika kipindi cha tafrani ile mumewe alikuwa njiani kurudi nyumbani alipokuta ugomvi umetinga ...kisa alihoji kwa nini mpangaji wa chumba jirani alifua nguo zake na kuzianika hadi mlangoni kwake na kisha yale maji toka kwenye nguo yakawa yanamdondokea mwanaye aliyekuwa akicheza barazani kwenye mlango wake.
Dada huyu anasema wana miezi 3 tu kwenye hiyo nyumba na hao wapangaji wenzie wameishi hapo kwa zaidi ya miaka 3. Anasema walipomjulisha mwenye nyumba hakufanya chochote. Anasema tayari walikuwa wamemjulisha mwenye nyumba kuhusu migogoro ya mambo k**a vile matumizi ya vyoo, sehemu ya maji taka, jalala na sehemu za kuanika nguo lakini hakuwapatia ushirikiano.

Je, wewe msomaji wa makala hii umepanga nyumba unapoishi? Changamoto zipi unazokabiliana nazo?

02/03/2024

why don't you offer lifts to the Men even when it is raining but Men are easy going, if asked for a lift by a woman just gives in, as for women hawezi toa lift Kwa mwanaume...!?

02/03/2024

is for Men, If purchased a property or asset and gave it to your partner or spouse will you revoke it at the point of separation or divorce...or you just let it go..!?

03/02/2024

Unaoimbwa k**a 'Cover'
Siku hizi kumekuwepo nyimbo zinazoimbwa k**a makala au toleo toka Kwa wimbo asilia maarufu k**a 'Cover'. Huu ni wimbo Unaoimbwa k**a zao la wimbo wa Kwanza asilia. Wimbo wa Aina hii hauimbwi na yule msanii au 'artist' wa Kwanza, Ila unaweza kuimbwa na mtu au msanii mwingine katika hali ya kunakiri ule wimbo wa awali, 'Original song'
Sasa ninachotaka kukisema hapa ni hizi 'cover' au nyimbo zinazoimbwa Kwa lengo la kubali maana ya ule wimbo wa awali.

Hivi ni sahihi inapotokea mwimbaji fulani kaimba muziki wa dini au injili kisha baadaye anotokea mtu mwingine anaurudia wimbo huo na kuuwekea maana tofauti kabisa ambayo haihusiani na dini wala injili, hatimaye wimbo k**a huo unaingizwa kwenye soko la muziki na kuvuruga hata Ile taswira ya nyimbo ya mwanzo kwenye jamii.

Kwangu Mimi binafsi nadhani hili ni tatizo katika Tasnia ya muziki. Sijui wewe msomaji Una maoni gani..lakini kubwa zaidi mara nyingi tumeona 'Cover' zinazonakiri nyimbo za injili 'Gospel songs' na kuzibadilisha kuwa za kidunia au kuwa na maana nje ya udini, 'Secular Music' Sijaona hizo nyimbo zinazoitwa 'Cover' zilizoimbwa kwa lengo la Kubadili Muziki wa kidunia kuwa wa dini...!?' Cover songs transformed from Secular to Gospels' Lakini nimeona nyingi ya nyimbo zinazobadilishwa maana kutoka kwenye Dini kwenda kwenye ule muziki wa dunia...na pengine kutumiwa na wanasiasa au kwenye vilabu vya Disco...tafakari

Want your business to be the top-listed Media Company in Spring Valley?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Spring Valley