Q Line Computer
🌿 KUKHITIMISHA JINA LAKO NA NENO 'ASSALAFIY' AU ' AL-ATHARIY K**A VILE KUJIITA ' ABUU KHUZAYMAH ASSALAFIY ' NI UZUSHI NA HALINA ASILI NA NI KATIKA KUISAFISHA NAFSI 🌿
🎇 FATWA YA SHEIKH SWALEH AL-FAWZAAN HAFIDWAHULLAH.
▶️ Swali :
" Baadhi ya Watu anakhitimisha jina lake kwa ' Assalafiy ' au ' Al-athariy ' , je hii ni katika kuitakasa Nafsi au kunawafikiana na Sheria ? .
▶️ Jawabu :
" Kinachotakiwa kwa Mtu ni kufuata Haki , kinachotakiwa kwa Mtu ni kuitafuta Haki na kuitaka Haki na kuifanyia kazi .
Ama kujiita kwamba yeye ni Salafiy au Athariy au mfano wake , hakuna haja ya hili , Allah anajua Subhaanahu wa Ta'ala .
"Sema mnamuelimisha Allah Dini yenu ? Allah anajua yaliyomo Mbinguni na yaliyomo Ardhini na Allah ni Mjuzi wa kila kitu ▪︎
[ Alhujuraat : 16 ]
Basi kujiita Salafiy , Athariy au mfano wa hayo , hili halina ASILI , sisi tunaangalia HAKIKA na wala hatuangalii Kauli wala kujiita wala Madai , anaweza kusema kwamba yeye ni Salafiy na wala sio Salafiy , (anaweza kujiita) Athariy na wala sio Ahariy , na anaweza kuwa Salafiy , Athariy na hajasema kwamba mimi ni Salafiy wala Athariy , kinachoangaliwa ni Ukweli wa majambo na sio majina na wala Madai .
Ni juu ya Muislamu ajilazimishe Adabu pamoja na Allah Subhaanahu wa Ta'ala , pale waliposema Mabedui : Tumeamini , Allah aliwakanusha .
" Wamesema Mabedui tumeamini , sema hamjaamini likini semeni Tumesilimu " [ Alhujuraat : 14 ]
Allah anakanusha juu yao kwamba wanazisifia Nafsi zao kwa Imani, ilihali hawajafikia kiwango hicho , kwa kule kudhania kwao wameingia katika Uislamu , Mabedui wamekuja kutoka Majangwani na wakadai kwamba wamekuwa Waumini moja kwa moja , hapana Wamesilimu wameingia katika Uislamu na pindi wakiendelea na wakajifunza ndio itaingia Imani katika Nyoyo zao pole pole , [ "Na bado haijaingia Imani katika Nyoyo zao" ] na neno ' lammaa' ni kwa kila ambacho kinatarajiwa , yaani itaingia Imani , lakini wewe unadai (Imani) mara ya mwanzo , basi hii ni kuisifia Nafsi , kwa hiyo hakuna Haja ya wewe kusema ' mimi ni Salafy ' mimi ni 'Athary ' mimi ni kadhaa, mimi ni kadhaa ni juu yako kuitafuta Haki na kuifanyia kazi na uitengeneze Nia , na Allah ndie anaejua Subhaanahu hakika ya Majambo "
📕 Chimbuko :
( https://youtu.be/Ivh2bclt3nU )
◀️ السؤال:
" بعض الناس يختم اسمه بالسلفي، أو الأثري، فهل هذا من تزكية النفس، أو هو موافق للشرع؟
◀️ الجواب:
" المطلوب أن الإنسان يتبع الحق، المطلوب أن الإنسان يبحث عن الحق ويطلب الحق ويعمل به، أما أن يتسمى بأنه سلفي أو أثري أو ما أشبه ذلك فلا داعي لهذا، الله يعلم سبحانه وتعالى {قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّهَ بِدِينِكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ} [الحجرات: 16] فالتسمي سلفي أثري أو ما أشبه ذلك هذا لا أصل له، نحن ننظر إلى الحقيقة ولا ننظر إلى القول والتسمي والدعاوى، قد يقول إنه سلفي وما هو بسلفي، أثري وما هو بأثري قد يكون سلفيًا وأثريًا وهو ما قال إني سلفي ولا أثري، فالنظر إلى الحقائق لا إلى المسميات ولا إلى الدعاوى وعلى المسلم أن يلزم الأدب مع الله سبحانه وتعالى لما قالت الأعراب آمنا أنكر الله عليهم {قَالَتِ الْأَعْرَابُ آمَنَّا قُلْ لَمْ تُؤْمِنُوا وَلَكِنْ قُولُوا أَسْلَمْنَا} [الحجرات: 14] الله أنكر عليهم أنهم يصفون أنفسهم بالإيمان وهو ما بعد وصلوا إلى هذه المرتبة، لتَوِّهم داخلين في الإسلام أعراب جاءوا من البادية وادعوا أنهم صاروا مؤمنين على طول لا، أسلموا دخلوا في الإسلام وإذا استمروا وتعلموا دخل الإيمان في قلوبهم شيئًا فشيئًا {وَلَمَّا يَدْخُلِ الْإِيمَانُ فِي قُلُوبِكُم} [الحجرات: 14] وكلمة لمَّا للشيء الذي يتوقع يعني سيدخل الإيمان لكن أنك تدعيه من أول مرة فهذه تزكية للنفس فلا حاجة إلى أنك تقول أنا سلفي أنا أثري أنا كذا أنا كذا عليك أن تطلب الحق وتعمل به وتصلح النية والله هو الذي يعلم سبحانه الحقائق ".
📕 المصدر :
( https://youtu.be/Ivh2bclt3nU )
- YouTube Enjoy the videos and music that you love, upload original content and share it all with friends, family and the world on YouTube.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Avenue De L'Indusrie A Cote De L'INTERBANK Siege;Hotel Amahoro
Rohero