AFYA BORA
KUPATA SIKU KUSIKO KWA KAWAIDA KWA MWANAMKE/ABNORMAL UTERINE BLEEDING
Ni kutokwa na damu nyingi zaidi au kupata siku kusiko Kwa Kawaida ya mwanamke kutoka kwenye mfuko wa uzazi. Inaweza kutokea mad wowote katika mzunguko wa mwanamke hata katika siku zake.
Dalili zake:
1. Kupata damu nyingi kupita kawaida yake
2. Kupata siku zake Kwa zaidi ya siku 7
3. Maumivu makali ya tumbo la uzazi/ chini ya kitovu katika kipindi cha kupata hizo damu
4.kupata mabonge ya damu badala ya damu ya kawaida anayopataga siku zote
5. Kuvurugika Kwa mpangilio wa kuona siku zake
6. Kushindwa kupata mimba
7. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
8. Uvimbe kwenye njia ya uzazi
VISABABISHI
1. Mimba.Wakati wa ujauzito mwanamke anaweza kutokwa na damu. Hii sio kawaida ya ujauzito hivyo moone daktari mapema.
2.Uvimbe katika mji wa uzazi/polyps au kwenye cervix
3. Saratani ya mji wa mimba au shingo ya uzazi. Hii huambatana na dalili k**a kushindwa kupata mimba
4. Maambukizi ya shingo ya uzazi/cervicitis
5. Kuvurugika Kwa homoni za kike/hormonal imbalnce
6. Vipandikizi cya kuzuia mimba/intrauterine devices
7. Matibabu Kwa njia ya homoni/hormonal replacement therapy. Hasa Kwa wenye umri ambao siku zao zilishakoma.
UCHUNGUZI
1.Uvimbe kwenye tumbo la uzazi
2. Damu
3. Ultrasound
4. Kuchukua kinyama Kwa ajili ya uchunguzi
5. Vipimo vya homoni
MATIBABU
Hutegemea na kisababishi.
Moon daktari akufanyie uchunguzi na kujadilina nawe juu ya matibabu yanayokufaa.
03/02/2018
CANCER VACCINE EXPERIMENTAL RESULTS
MAJARIBIO YA CHANJO YA SARATANI
Cancer ‘vaccine’ eliminates tumors in mice Activating T cells in tumors eliminated even distant metastases in mice, Stanford researchers found. Lymphoma patients are being recruited to test the technique in a clinical trial.
12/11/2017
Tukiazimisha siku ya kisukari duniani tarehe 14 novemba ni vema kutambua machache kuh6usu ugonjwa huu hatri ambao unaongezeka kwa kasi muongozi mwetu.chalisho hili linapatikani ktk mwanachi.
Ugonjwa wa Kisukari ni miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania.
Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka au kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.
Aina za kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo:
Kisukari Namba Moja
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo k**a beta cells of Islet of Langerhans.
Iwapo tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.
Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi hiyo.
Mashambulizi katika kongosho huweza kufanywa na magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga ya mwili.
Uharibifu katika tezi kongosho hupelekea kukosekana kabisa kwa wa tezi ya insulin au huifanya tezi hiyo kuzalishwa kwa kiwango kidogo.
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano katika maisha yao yoteili waweze kuishi. Ndiyo maana aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM)
2. Aina ya Pili ya Kisukari
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.
Hali hii husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa (physical inactivity).
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake.
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. NNon66 maana aina hii hujulikana pia k**a kisukari kisichotegemea insulin au Non6-Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)
3. Kisukari cha Ujauzito
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito.
Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2-5 ya wanawake wajawazit, ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua.
Hata hivyo, karibu asilimia 20 mpaka 50 ya wanawake wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea nacho hatimaye kuwa aina ya pili ya kisukari maishani.
Kisukari husababishwa na nini?
Visababishi vya kisukari hutofautiana kulingana na aina husika ya kisukari.
1.Visababishi vya6 aina ya kwanza ya kisukari
Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi ya Coxsackie virus type B4.
Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za baadhi ya vyakula (food borne chemi6cal toxins), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng’ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto kuushambulia mwili wenyewe (autoimmune reaction) na hivyo kupelekea uharibifu katika tezi kongosho.
2.Visababishi vya aina ya pili ya kisukari
Kwa ujumla aina hii ya kisukari husababishwa zaidi na mfumo wa maisha na matatizo ya kurithi. Aidha vitu k**a kuongezeka uzito na unene kupita kiasi (obesity) nayo pia huchangia kutokea kwa aina hii ya kisukari.
Sababu nyingine ni pamoja na Kuongezeka umri, maisha ya kivivu na kutofanya mazoezi (physical inactivity).
Click here to claim your Sponsored Listing.