ELCT Northern Diocese
29/12/2020
Jana tarehe 28/12/2020 ilikuwa siku ya Askofu na WanaDayosisi wa Dayosisi ya Kaskazini wanaoishi kwenye mikoa mingine. Utamaduni huu umekuwa ukifanyika kwa takriban miaka 27 sasa. Mahudhurio ya jana yalikuwa takriban watu 530. Mhe Baba Askofu alitoa taarifa ya maendeleo ya Dayosisi na mipango ya miaka ijayo. Aidha Askofu aliwashukuru sana Wanadayosisi kwa michango yao ya Mali na mawazo ya kuendeleza jamii na Kanisa la Bwana. Kwa mara ya kwanza kikao hicho kilifanyika kwenye Makao makuu ya Chuo chetu Cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kinachojengwa Makuru, Machame. Zifuatazo ni picha za matukio hayo ya jana.
23/11/2020
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amewataka viongozi na waumini wa kanisa hilo kumtegemea Mungu bila kuingiza mambo ya kidunia pindi wanapokutana na changamoto za kimaisha.
Dk Shoo, ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, ametoa wito huo jana tarehe 22 Novemba 2020, katika usharika wa Moshi Mjini, wakati akihubiri kwenye ibada maalumu ya kumuingiza kazini Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo, Mchungaji Deogratius Msanya pamoja na kubariki wachungaji watano.
Mchungaji Msanya ambaye anakuwa msaidizi wa saba wa Askofu katika Dayosisi ya Kaskazini, alichaguliwa Tarehe 18 Agosti 2020 kwenye mkutano mkuu wa 36 wa dayosisi.
Askofu Shoo amesema kunahitajika uhodari mkubwa, umakini, moyo mkuu na kuondokana na woga, katika kuwatumikia watu wa Mungu, kwa kuwa Mungu aliyewaita watu wake, huonyesha njia ya namna ya kutumika na kulifikia kusudi.
Amesema katika dunia zipo changamoto nyingi, ikiwemo za Kiuchumi, kifamilia na hata za kiimani lakini k**a viongozi walioitwa kuliongoza taifa la Mungu, wanapaswa kumtazama aliyewaita, ambaye ana majibu ya changamoto hizo.
"Msitishwe na changamoto za dunia hii, k**a za kiuchimi, kifamilia na hata za kiimani, tambueni yupo Mungu na mtakapomtegemea na kumuita, atawawezesha kuzivuka changamoto zote," amesema Askofu Shoo.
Aliongeza kuwa "Tumtegemee Mungu bila kuweka mchanganyo, maana wapo watu wakiwa kanisani anamkiri Yesu Kristo, akitoka anakwenda kutafuta mchanganyo mwingine. Tutubu na kumtazama Mungu maana hashindwi na jambo lolote".
Askofu Shoo amemtia moyo Mchungaji Msanya na kumsihi asiogope wala kufadhaika kutokana na wajibu aliokabidhiwa, badala yake amtegemee Mungu aliyemuita katika wajibu huo.
"Uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope wala usifadhaike, kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako, na fahamu hukuitwa na mtu bali Mungu mwenyewe na katika yeye utayaweza mambo yote"
Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira. Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Moshi