Majembe12
31/10/2023
NENO LA SIKU
31-10-2023
SOMO:KESHO YAKO I MIKONONI MWA MUNGU
.Iko ivi Mungu anayajua MAHITAJI Yako yote,anazijua haaja zako zote na changamoto zako zote.
Na hakuna hata Moja inayomshinda kwamba hawezi kutatua..kwa maana Mungu wote ni MUWEZA WA YOTE.
👉Lakini ili uzipate baraka zako au MAHITAJI Yako yote lazima ufuate utaratibu wa ki-Mungu, Lazima uguse moyo wake.. kwanza Mungu wetu anapenda kuheshimiwa,kuabudiwa na kusifiwa..na kuaminiwa pia anapenda kutumainiwa..no matter the situation uko nayo..We amini Mungu nimuweza,just put your trust in Him, Don't stop praising and worshipping Him.
👉Binadamu tuko na mawazo yetu Ivo Kuna wakati tunafanya vitu kwa mawazo yetu na mawazo yetu mara nyingi yanatupoteza.. MITHALI 5:5b anasema usizitegemee akili zako mwenyewe,
Ivo Muombe Mungu akupe ufahamu wake na hekima yake ili uweze kutenda na kufanya mambo kwa usahihi ili uifikie kesho Yako kirahisi(yaani OMBA Roho wake akuongoze)
👉Hakikisha katika njia zako zote unamkiri yeye, katika Kila jambo ulitendalo muweke Mungu mbele, Kiri kwamba Mungu ndio ameshika kesho Yako,ndio anazijua hatua zako, ndio Kiongozi wa familia Yako,ndio afya Yako na uzima wako na mengineyo yanayokuhusu haijalishi unauaweza au huyawezi
Ndipo MITHALI 5:6b Naye atanyoosha mapito Yako
Yaani njia zako zitakuwa nyeupe na zimebarikiwa na mbaraka wa Mungu.
BARIKIWA🙏
🌹 JESUS IS LORD ❤️🙏
Click here to claim your Sponsored Listing.