Ishi Njozi

Ishi Njozi

Share

Online Courage ipo ii kukupa tumaini na Nguvu.

25/03/2023

HATUA TATU KUTOKA KWENYE DHAHABU,

Hii ni hadithi ya kweli...

Mr Darby alikuwa kwa muda mrefu anatamani kuchimba dhahabu,

Na kutokana na tamaa hiyo alipata homa,

Hatimaye alifanya uamuzi wa kwenda na

KUCHIMBA NA KUWA TAJIRI hakuwahi kuelewa kwamba,

Dhahabu imechimbwa sana kutoka katika akili za watu kuliko kutoka ardhini...

Kazi ikaanza,

Baada ya kuchimba sana na kutumia vifaa vingi,

Vingine ambavyo alisaidiwa na ndugu zake..

Bado aliambulia patupu šŸ˜”,

Darby akiwa na Mjomba wake hatimaye wakafanya uamuzi k**a wa wengi...

šŸƒ KUONDOKA

Wakauza vifaa vyote kwa mtu aliyeonekana wa hali ya chini,

Huyu mtu alifanya Jambo la utofauti,

Alitafuta mtaalamu ambaye alilichunguza eneo na kumwambia.

Dhahabu ipo hatua tatu eneo Darby na mwenzake waliishia,

Baada ya kuchimba HATUA TATU TU!

Dhahabu ilipatikana,

Somo;

Kabla ya kukata tamaa ni vema ukapata ushauri kutoka kwa wataalamu kuhusu Jambo unalotaka kufanya,

Natumaini Umejifunza kitu hapa,

Kumbuka *Njozi Yako Ni Taa Yako*

Mpaka Wakati mwingine,

"Njozi Yako Ni Taa Yako"

Njozi Media

24/03/2023

*Mvuvi mwenye Akili...*

Mwanaume mmoja aliamua kwenda kumu angalia mvuvi,

Akafika na akamuona anaendelea kuvua kaa,

Jambo moja lilimshangaza na kumfanya amuulize mvuvi hivi,

"Mbona haujafunika ndoo hiyo unamoweka kaa?"

Mvuvi alijibu kiufupi,

"Nimeacha wazi kwa sababu wapo kaa wengi ndani ya ndoo"

Mwanaume akashangaa,

"Unamaanisha Nini?"

Ndipo akaeleza kwa undani zaidi,
"Kwa sababu kaa wapo wengi hakuna kaa atakayejaribu kutoka, Maana kila anapotaka kutoka kaa wengine watamvuta na kubaki ndani ya ndoo"

Nimekusimulia kisa hiki kifupi ili nikwambie Hili,

*Aina ya watu ambao unanzungukwa nao,Kwa namna moja au nyingine ndio wanaweza kukuinua au kukushusha*

Kuna msemo ambao unasema,

"Niambie aina ya marafiki ulipnao, nitakwambia hatma yako"

Sasa ikiwa unakaa karibu na sigara Bila shaka hata wewe utavuta sigara pia,

Hata K**a utasema siwezi bado utavuta Moshi wake ambao Ni hatari zaidi,

Ni wakati wa kutafakari ndugu, jamaa na marafiki ambao unakuwa naonmara kwa mara,

Je wanakusaidia kuona unafukia malengo yako?

Au Ni wa kukushusha chini.

Ikiwa unaona unashushwa chukua tahadhari kwa sababu mwishowe hautafika popote,

Kuna kisa kingine tena,

Kwamba mwindaji aliokota yai la tai porini,

Akalichukua na kulipeleka nyumbani kwake akachanganya pamoja na mayai ya Kuku,

Hatimaye lilitotolewa na tai akachanganyika pamoja na vifaranga,

Akiwa tayari mkubwa aliona Kiumbe mwingine tofauti kabisa na Kuku,

Huyu alikuwa akiruka juu Sana kuliko kuku wa kawaida,

Akauliza kwa Kuku Ni kwa Nini ndege yule anaweza ruka vile na sisi hatuwezi,

Aliambiwa "Yule Ni tai na sisi Ni kuku"

Hatimaye tai huyu alikufa akiwa hajajitambua kuwa alikuwa Ni tai.

Hata wewe ili kufika unapotaka kufika Lazima uhalikishe u azungukwa na watu sahihi,

Naamin umejifunza kitu hapa,

Mpaka Wakati mwingine,

"Njozi Yako Ni Taa Yako"

Njozi Media.

23/03/2023

*Kosa kubwa ambalo kila mwenye Njozi anatakiwa kuliepuka.*

"Mdomo wako utakuponza"

Unaelewa Nini unapoambiwa msemo huo?

Leo nitakwambia kosa ambalo wenye Njozi (Ndoto kubwa) wengi hufanya,

Na hatimaye kuchelewa Kutimiza Njozi zao au hata Kutotimiza kabisa,

Haya hebu tuanze,

Karibu kila mtu amepewa mdomo,

Lakini sio kwamba kila wakati na kila sehemu ukiwa na kila mtu unatakiwa kuongea,

Yaani Kufungua mdomo wako...e

Kwa sababu,

Unapokuwa mtu wa kutojua wapi uongee, kwa Nani uongee, na nini uongee waweza pata hasara hizi,

•Kuzuia nafasi yako ya kujifunza zaidi kutoka kwa huyo mtu,

Tambua hili wanaojua Mambo mengi Mara zote hawapendi kusema Sana,

Unapokuwa unaongea Sana wao waweza kaa kimya au kubaki Wanasema,

"Enhee",

"Ilikuwaje?"

"Wachawe!!!"

Na wewe unasema hapa ndipo kumbe yote unayosema yeye anajua,

Ila kwa sababu anapenda kujifunza zaidi ndo maana anakusikiliza,

Na pia kwa kuwa mtu wa kuongea tu,

•Upo hatarini kusema mipango yako kwa watu ambao wanaweza kutumia K**a Silaha dhidi yako,

Unao marafiki, ndugu na jamaa...

Kila mtu ana fikra zake, Mipango yake, na utofauti wake,

Lakini "Kila mtu anataka kuwa na Mafanikio makubwa maishani"

Hivyo unapokuwa na NJOZI kubwa na Ni mtu wa kusema Sana,

Waweza sema Njozi Yako kwa watu ambao wakishatoka hapo kuondoka na kupambana mpaka watimize kabla yako,

"Usiseme Seme"

"Tulia"

Ninakunong'oneza maneno haya kwa sababu Asilimia tisini na Saba hawajui Hili,

Ngoja Ni kuaminishe zaidi,

Watu Hawa,
1.Albert Eisten,

2.Jk.Lowling,

3. Elon Musk,

4. Michael Jordan,

5. Warren Buffet,

Na wengine wengi wote Ni watu ambao sio waongeaji Sana,

Waweza angalia Mafanikio ya kila mmoja Google,

Huu ni ujumbe ambao utasikia Mara chache unaongelewa,

Hivyo Basi chukua hatua Sasa,

Badilika Sasa,

Kwa sababu Huenda asikukumbushe mtu mwingine yeyote,

Nakutakia Siku Njema,

"Njozi Yako Ni Taa Yako"

Njozi Media.

24/01/2023
18/01/2023

*Ikiwa Una HOFU kuhusu Mwaka 2023! Ujumbe huu NI KWA AJILI YAKO,*

Ilikuwa ni wiki ya kwanza tu ya Mwaka 2023 ambapo ilitangazwa kwamba Mwaka huu utakuwa Ni Mwaka mgumu kuliko 2022,

Habari hizi zimetapakaa Mtandaoni,

*HOFU* Inaongezeka kwa wengi.

Huenda unajiuliza "Nifanyeje?"

Ukweli Ni huu...

Mambo yanapokuwa magumu au kuonekana magumu,

1. Ni fursa ya kuongeza umakini kwa kila unachotaka kufanya.

2. Unaandaliwa kuwa imara zaidi.

Hivyo basi badala ya kuwa na hofu ya maisha hasa 2023

Ongeza UMAKINI KWA KILA UFANYALO.

Kwamba Mwaka utakuwa mgumu haimaanishi hauwezi kumbana na kufikia NJOZI YAKO.

Natumaini umejifunza kitu hapa,

Yupo ambaye atakushukuru iwapo utamtumia Ujumbe huu mkumbuke,

Bado tuna endelea na kutoa huduma na kuona huduma yetu inakuwa Bora,

Mpaka Wakati mwingine,

@ Ishi Njozi Media.

Want your restaurant to be the top-listed Restaurant in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address

Mbeya

Opening Hours

Monday 05:00 - 11:00
Tuesday 05:00 - 11:00
Wednesday 05:00 - 16:00
Thursday 05:00 - 11:00
Friday 05:00 - 11:00
Sunday 05:00 - 11:00