Rubondofm
Mashindano ya Jaspers Day Msimu wa pili yamezinduliwa rasmi Mkoani Geita yakianza kutimua vumbi kwa michezo ya watoto chini ya umri wa miaka 15.
Faustine Mabeja ni Mdau wa soka Mkoni Geita akizungumzia Mashindano hayo ameyataja kuwa yanatoa chachu kwa vijana kuonesha vipaji vyao.
Kwa upande wake Sebastian Manyasi Kocha wa mpira wa miguu kwenye kituo cha michezo cha KAC cha Katoro amesema mashindano hayo kwa kuwa siyo mara ya kwanza kufanyika yamekuwa yakiwaunganisha kupitia michezo.
Katibu mkuu wa kituo cha michezo cha Jaspers kilichopo Mkoani Geita amesema Mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika kwa makundi matatu ambayo ni watoto chini ya umri wa miaka 13, Miaka 15 pamoja na timu za watu wakubwa.
Mashindano hayo kwa upande wa watu wakubwa yataanza kutimua vumbi tarehe 8 mwezi wa saba mwaka 2026.
29/06/2026
MENEJA MKUU GCU LTD ARIDHISHWA NA MWITIKIO WA WAKULIMA KUUZA PAMBA KUPITIA CHAMA
Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Geita (GCU LTD) Ramadhani Sadiki Sephu, amefanya ziara katika vituo mbalimbali vya ununuzi wa pamba wilayani Geita kwa lengo la kujionea mwenendo wa zoezi la ununuzi wa zao hilo na kuzungumza na wadau mbalimbali.
Katika ziara hiyo, Meneja Mkuu alieleza kuridhishwa na mwitikio mkubwa wa wakulima ambao wanaendelea kuuza pamba yao kupitia GCU LTD, akisema hali hiyo inaonesha imani ya wakulima kwa chama hicho kutokana na huduma bora kinazozitoa.
Katika Ziara hiyo, Meneja Mkuu aliambatana na Mkaguzi wa Pamba kutoka Bodi ya Pamba Wilaya ya Geita Filbert Matondwa, ambapo walisisitiza wanunuzi wote kuendelea kuzingatia viwango vya ubora wa pamba ili kuhakikisha zao hilo linakidhi matakwa ya soko na kuongeza thamani yake.
Kwa upande wao, wakulima waliozungumza wakati wa ziara hiyo walieleza kufurahishwa na huduma zinazotolewa na GCU LTD, hususan malipo ya haraka na kwa wakati, jambo ambalo limewapa motisha wa kuendelea kukiuzia chama hicho pamba yao.
GCU LTD imeendelea kuhimiza wakulima kuzingatia kanuni bora za uzalishaji na utunzaji wa pamba ili kuongeza ubora wa zao hilo na kuinua kipato chao pamoja na kuchangia ukuaji wa sekta ya pamba nchini.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Geita
30101