GLORY KWAYU

GLORY KWAYU

Share

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.--Yohana 10:10

26/05/2026

🇹🇿🇹🇿🎤🌍

20/05/2026

Day 20..

KUISHI KUSUDI LA MUNGU HAPA DUNIANI.

Watu wengi wamekuwa wakitaka kufanya mambo makubwa sana lakini wanakwama,

Wanataka mafanikio makubwa lakini hawajui njia sahihi ni ipi,

Wengi wanafanya mambo ambayo siyo ya kwao,siyo yaliyowaleta Duniani,

Laiti watu hawa wangekaa na kutafuta kujua ni nini maana ya wao kuja Duniani,wasingesema maisha ni Magumu.

Kila mmoja ambaye yupo Duniani ana kazi maalum aliyokuja kuifanya,siyo kwa udogo bali kwa ukubwa.

Siri ya Kufanya Mambo makubwa ni kulijua kusudi la Mungu hapa Duniani,kwa nini upo Duniani,kwa nini unavuta iyo Pumzi?

Hakuna mtu aliyekuja tu kwa ghafla au aliyekuja tu kuongeza namba Duniani,Hapana,

Kuishi kusudi la Mungu hapa Duniani ndiyo mwanzo wa mafanikio yako,ndiyo chanzo cha uwepo au umaana wako hapa Duniani.

Unataka Hekima,Ufahamu na Maarifa ya Mungu ili ukafanyie nini?

Hekima,Ufahamu,Akili na Maarifa ya Mungu ni kwa ajili ya Kutimiza KUSUDI uliloitiwa hapa Duniani.

Tusome kidogo hapa;

Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma?
Yohana 7:15

Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka.
Yohana 7:16

Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
Yohana 7:17

Yesu alipokuja hapa Duniani,hakuishi anavyotaka yeye,aliishi sawa na Mapenzi ya Baba yake,alifanya yale yaliyo Mapenzi ya Baba,hakuja Duniani ili kuishi k**a Dunia inavyotaka bali k**a Baba anavyotaka.

Hakuna maana yeyote ile Kuishi miaka 80-100 na hujafanya kusudi la Mungu,miaka yako yote umeipoteza kwenye mambo ya ujinga.

Maisha ni marahisi sana ulijua kwa nini upo Duniani,Mafanikio makubwa sana ni kuliishi KUSUDI la kuumbwa kwako.

Hii siku itumie kabisa kujifanyia Tathmini tika umeiingia Duniani,Unaishi KUSUDI au unapoteza muda na uyo mwalifu mwenzio?

Mwl.Glory Kwayu
Dodoma-Tanzania.

19/05/2026

Neno ni Silaha….🇹🇿🇹🇿🎤

17/05/2026

Mwanza Mwanza,

Tutakuwa na Ibada ya Mkesha wa Kujazwa Roho Mtakatifu na Nguvu zake tarehe 05/6/2026 badala ya tarehe 22/5/2026.

Kila mmoja chukua Nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya Ibada hii kubwa ambapo Yesu mwenyewe atakuwepo kutuhudumia,

Ishara na Miujiza zitaonekana,waliofungwa na nguvu za giza watafunguliwa,

Kila atakayefika kwenye Ibada hii,atapokea Neno la Maarifa,Atajazwa Roho Mtakatifu na Nguvu zake,

Mahali:Ukumbi wa Vijana Centre Mlango mmoja,
Muda:07:00 Jioni Mpaka 06:00 Asubuhi
Tarehe:05/6/2026

Share na Familia yako,Marafiki zako,Wafanyakazi wenzako kwa ajili ya Ibada hii Muhimu sana.

Mwl.Glory Kwayu
Dodoma-Tanzania

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address

Dodoma
Dodoma