Arusha Technical College
Arusha Technical College is a center of excellence that provides a national and international high-level human resource through exemplary competence based Technical Education and training in Tanzania. The institution which has become the Arusha Technical College (ATC), was established in 1978 jointly by the Governments of the United Republic of Tanzania and Germany, under the name of the Technical
26/06/2026
𝗖𝗛𝗨𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗨𝗙𝗨𝗡𝗗𝗜 𝗔𝗥𝗨𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗕𝗜𝗢𝗡𝗜 𝗞𝗨𝗔𝗡𝗭𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗣𝗥𝗢𝗚𝗥𝗔𝗠𝗨 𝗭𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗛𝗔𝗗𝗔 𝗬𝗔 𝗨𝗭𝗔𝗠𝗜𝗟𝗜 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗨𝗛𝗔𝗡𝗗𝗜𝗦𝗜 (𝗠𝗔𝗦𝗧𝗘𝗥'𝗦 𝗗𝗘𝗚𝗥𝗘𝗘 𝗣𝗥𝗢𝗚𝗥𝗔𝗠𝗠𝗘𝗦)
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kiko mbioni kuandika historia kwa kuanzisha programu mbili mpya za Shahada ya Uzamili zitakazowawezesha wataalamu wa sekta ya uhandisi kuendelea na masomo ya juu na kufikia ngazi za juu za uongozi katika taaluma zao.
Hatua hiyo imebainishwa wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau ya mapitio ya mitaala miwili mipya pamoja na uhuishaji wa mitaala mingine mitano ya chuo hicho. Warsha hiyo ni sehemu ya mchakato wa kuhakikisha programu hizo zinakidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya teknolojia.
Akizungumza katika warsha hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Florence Mamboya, alisema lengo la kuandaa kikao hicho ni kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoa maoni kuhusu mitaala hiyo ili kuhakikisha inazalisha wataalamu wenye ujuzi na umahiri unaohitajika katika sekta husika.
Dkt. Mamboya alifafanua kuwa programu hizo mpya za Shahada ya Uzamili ni Uhandisi wa Umeme na Mifumo ya Kujiendesha Kielektroniki (Electrical and Automation Engineering) pamoja na Nishati, Uhandisi na Usimamizi (Energy, Engineering and Management). Alisema maoni yatakayokusanywa kutoka kwa wadau yatawasilishwa NACTVET kwa ajili ya mapitio, hatua ambayo ni muhimu katika kuhakikisha programu hizo zinakidhi viwango vinavyotakiwa na kuwapa wahitimu nafasi ya kusonga mbele kitaaluma hadi kufikia ngazi za usimamizi na uongozi.
Aidha, alibainisha kuwa miongozo ya NACTVET inasisitiza ushirikishwaji wa wadau katika maendeleo ya mitaala ili kuhakikisha wahitimu wanaozalishwa wanakuwa na maarifa na stadi zinazolingana na mahitaji halisi ya soko la ajira.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mitaala wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Laban Kanyonga, amesema kuanzishwa kwa programu hizo za Shahada ya Uzamili ni hatua kubwa na ya kihistoria kwa chuo hicho, ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikitoa mafunzo ya ufundi na teknolojia katika ngazi mbalimbali.
Dkt. Kanyonga anaongeza kuwa baada ya kukamilika kwa hatua za mapitio na kupata idhibati kutoka mamlaka husika, chuo kinatarajia kufikia Novemba 2026 kuanza rasmi kupokea wanafunzi katika programu hizo mpya.
Washiriki wa warsha hiyo, wamepongeza hatua hiyo wakieleza kuwa itaongeza idadi ya wataalamu wabobezi nchini na kutoa fursa zaidi kwa wahandisi kujiendeleza kielimu.
Kuanzishwa kwa programu hizo kunatarajiwa kuimarisha nafasi ya Chuo cha Ufundi Arusha k**a kitovu cha mafunzo ya teknolojia na uhandisi nchini, huku kikichangia kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya uchumi wa kisasa unaotegemea ubunifu, maarifa na teknolojia.
22/06/2026
https://youtu.be/ylJvwQGnnt0?si=YwK72kPGAVXXTP84
Maendeleo ya Ujenzi wa Kiwanda cha Mafunzo na Uzalishaji Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kinaendelea na ujenzi wa Kiwanda cha M...
17/06/2026
Ushirikiano wa Kimkakati: Jinsi TaESA Inavyosaidia Wahitimu Kupata Kazi na Uzoefu Nyd de videoer og den musik, du holder af, upload originalt indhold, og del det hele med venner, familie og verden på YouTube.
17/06/2026
UBUNIFU WA NISHATI SAFI NA TEKNOLOJIA MAHIRI WANG’ARA KATIKA MAONESHO YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA
Mwanafunzi wa Uhandisi wa Mitambo katika Chuo cha Ufundi Arusha Bw Godlisten Joseph ameonesha umahiri mkubwa kupitia ubunifu wa gari linalotumia umeme na nishati ya jua ubunifu huo umeonesha uwezekano mkubwa wa matumizi ya nishati safi katika sekta ya usafiri hivyo kupunguza utegemezi wa mafuta na kuchangia uhifadhi wa mazingira kupitia teknolojia endelevu.
Hayo yanajiri katika Viwanja vya Ufundi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Utafiti Ubunifu na Ujasiriamali yanayoendelea , yaliyooanza Juni 15 na kutarajiwa kumalizika Juni 19 2026.
Kwa upande wa mwanafunzi mwingine David Samwel Sitta alieleza kuwa katika sekta ya afya Mfumo Mahiri wa Tiba ya Mwanga Phototherapy uliendelea kuvutia wageni kutokana na uwezo wake wa kugundua viwango vya bilirubini kiotomatiki na kusaidia utoaji wa huduma za afya kwa usahihi zaidi
Naye mwanafunzi wa Uhandisi wa Mitambo Bi Gladness Tesha alieleza kuwa kifaa cha kuosha mikono kiotomatiki kinachotumia sensa ya maji kilivutia umakini kwa mchango wake katika kuimarisha usafi wa mikono na kupunguza matumizi ya maji kwa njia endelevu
Pamoja na hayo wageni walijifunza kupitia vifaa vya mafunzo ya kiufundi katika sekta ya nishati ikiwemo Kifaa cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Nishati kwa Hewa Iliyobanwa Compressed Air Energy Storage Training Kit pamoja na Kifaa cha Mafunzo ya Nishati Jadidifu Renewable Energy Training Kit vilivyolenga kuongeza uelewa kuhusu teknolojia za nishati mbadala na matumizi yake katika mifumo ya kisasa ya umeme.
15/06/2026
𝗔𝗧𝗖 𝗬𝗮𝗮𝗱𝗵𝗶𝗺𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗠𝘀𝗶𝗺𝘂 𝘄𝗮 𝗧𝗮𝘁𝘂 𝘄𝗮 𝗪𝗶𝗸𝗶 𝘆𝗮 𝗨𝘁𝗮𝗳𝗶𝘁𝗶, 𝗨𝗯𝘂𝗻𝗶𝗳𝘂 𝗻𝗮 𝗨𝗷𝗮𝘀𝗶𝗿𝗶𝗮𝗺𝗮𝗹𝗶
-𝗞𝘂𝗸𝘂𝘇𝗮 𝗨𝗯𝘂𝗻𝗶𝗳𝘂 𝗸𝘄𝗮 𝗠𝗮𝗲𝗻𝗱𝗲𝗹𝗲𝗼 𝗘𝗻𝗱𝗲𝗹𝗲𝘃𝘂
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Shigeki Komatsubara, amesema uwekezaji katika ubunifu, utafiti na ujasiriamali wa vijana ni nguzo muhimu katika kuharakisha maendeleo endelevu ya taifa.
Bw. Komatsubara amesema hayo Juni 15 ,2026 wakati akifungua Msimu wa Tatu wa Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Ujasiriamali katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unaofanyika kuanzia Juni 15 hadi 19, 2026.
Ameongeza kwa kueleza kuwa UNDP itaendelea kuunga mkono ubunifu, maendeleo ya kidijitali na ujasiriamali wa vijana ili kuwasaidia kubadili mawazo yao kuwa suluhisho na biashara zenye tija. Huku akipongeza kiwango cha ubunifu kilichooneshwa na wanafunzi wa ATC, ambapo bunifu nyingi zimeonyesha uwezo wa kutatua changamoto halisi zinazoikabili jamii na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Prof. M***a Chacha, amesema ushiriki wa wanafunzi waliomaliza ATC katika maadhimisho hayo unalenga kuwahamasisha wanafunzi waliopo chuoni kuendelea kuamini katika ndoto zao, kutumia maarifa waliyojifunza kujiajiri na kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii.
Amesema chuo hicho kimeendelea kuibua na kuendeleza mawazo bunifu yenye uwezo wa kutekelezeka, akitolea mfano mradi wa mita janja za maji zinazolipiwa kabla ya matumizi (Water Prepaid Meter) ulioanzishwa chuoni hapo na kufikia hatua ya kutumiwa na mamlaka mbalimbali za maji nchini baada ya kuendelezwa kwa msaada wa kitaalamu na kifedha.
Prof. Chacha ameongeza kuwa chuo kinaendelea na Ujenzi wa Kiwanda cha Mafunzo na Uzalishaji (Industrial Workshop) kitakachokuwa kitovu cha kuzalisha na kuendeleza bunifu za wanafunzi, huku maadhimisho ya wiki hiyo yakitarajiwa kuendelea hadi Juni 19 kwa maonesho ya teknolojia, mijadala ya kitaalamu na shughuli za ujasiriamali zinazolenga kukuza ubunifu na maendeleo kwa vijana.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the university
Telephone
Website
Address
Arusha
Opening Hours
| Monday | 07:30 - 15:30 |
| Tuesday | 07:00 - 15:00 |
| Wednesday | 07:00 - 15:30 |
| Thursday | 09:00 - 15:00 |
| Friday | 07:30 - 15:30 |