Vibes Code TV
AWALI UJUMBE WA MUWAKILISHI WA WANAWAKE KWALE Zuleikha Juma Hassan KWA M'BUNGE WA MSAMBWENI Hon. Feisal Abdallah Bader
Mheshimiwa Feisal Bader toka aapishwe, jana ndio alianza rasmi kutembelea mawaziri kwa niaba ya wanachi wa Msambweni.
Katika mawaziri wote humu nchini, walio katika sekta mbali mbali, aliamua kumtembelea waziri wa MADINI, Hon John Munyes.
Kulingana na waziri Munyes na niyyah zake na vitendo vyake alivyo onyesha kabla ya kura za juzi za Msambweni, na kulingana na wale viongozi wote walio muunga Feisal Bader mkono katika azma yake ya kuwa mbunge wa Msambweni,na tunavyo wafahamu, hili jambo sio la maajabu. Bila shaka viongozi hao walikuwa wanatafuta mtu wa kumtuma kufanya watakayo wao na sio watakayo wananchi wa Msambweni, kwa mkutano huo wa jana ni dhahiri kuwa wame faulu kwa hilo.
CDA walio enda kuizungumzia ni pesa za wananchi wa Msambweni aina mbili:
1. Walio furushwa kutoka ardhi zao ili kuchimbwe madini na
2. Wanao ishi karibu na sehemu inayo chimbwa madini (kwa sababu wana athirika na vumbi au kelele au changamoto zengine za uchimbaji).
Kwa hesabu zilizoko, toka mwaka 2016 sheria ya Mining Act ilipo pitishwa, fedha hizi kufikia sasa, ni shilingi baina ya shilingi bilioni moja nukta mbili hadi bilioni mbili nukta nne (1,200,000,000 hadi 2,400,000,000) au milioni elfu moja na mia mbili hadi milioni elfu mbili na mia nne.
Waziri wa madini alipeleka kanuni (regulations) za usimamizi na utumizi wa pesa hizi, mwezi Juni 2017, akijua kuwa wabunge hawato kuwa na muda waku kagua na kujadili kanuni hizo kwa vile walikuwa kwenye campaign. Basi baada ya siku 60 hivi, k**a kanuni hazija jadiliwa na wabunge, huwa zina pitishwa kisheria bila pingamizi. Kuonyesha wazi niyyah yao ilikua zipite kanuni hizo bila kuchambuliwa na wabunge.
Hizo kanuni ni mbaya kwa sababu ya kumpokonya nguvu mwananchi wa kawaida muathiriwa wa madini na kuwa viongozi kipao mbele - jambo ambalo ni kinyume na niyyah ya Mining Act (2016).
Waziri Munyes, licha ya mimi kumu andikia barua aregeshe nguvu kwa muathiriwa kuliko viongozi katika hizo kanuni, alikataa kwa sababu hajani jibu barua yangu mpaka leo.
Pia mwaka jana mwezi wa pili alitangaza rasmi wana k**ati wa CDA. Hapi ndani kuna mbunge, gavana na MCA. Pia k**ati hiyo haiku chaguliwa na waathiriwa wote k**a ilivyi andikwa ndani ya kanuni. Wanak**ati wengine walichaguliwa na watu wachache, wengi wao ambao hata sio waathiriwa.
Laku sikitisha zaidi katika k**ati mbili za Kwale County za CDA (Msambweni na Lunga Lunga), Governor Salim Mvurya na bibi yake wamo humo ndani, na hilo ni jambo hali ruhusiwi katika sheria zetu za Kenya, kuwa mtu na mke wake wote wawili wawe ndani ya k**ati moja ya kiserekali.
Kumalizia nataka kusema haya:
1. Namuomba Allah atupe sisi tunao taka haki kwa waathiriwa wa madini, uwezo wa kupata haki hizo na atulinde na maovu yote yanayo pangwa kuendelea kugandamiza waathiriwa ndani ya umaskini. Amin.
2. Namuomba Hon Feisal Bader, asisikize anavyo tumwa na viongozi wengine vile watakavyo wao afanywe k**a kijakazi ama mtumwa wao kufanya mambo ya dhulma. Akifanya hivyo ajue hukumu ya Mwenyezi Mungu ina msubiri pia yeye hapa duniani na akhera pia. Kila anachofanya ahakikishe siku ya kiama anaweza kusimama mbele ya Allah bila wasi wasi akijua aliyo yafanya yote k**a mbunge yalikuwa ya kheri na sio ya shari.
Alaisallahu biahkamil hakimin (Kwani Allah sio muadilifu kuliko mahakimu wote?) - Quraan 95:8
Click here to claim your Sponsored Listing.
Contact the business
Telephone
Website
Address
Ukunda